Featured Post

RADIO 5 YA LOWASSA YAFUNGIWA ARUSHA, MAGIC FM NAYO NDANI!

Robert Lowassa, mmiliki wa kituo cha radio cha Radio 5 kilichoko jijini Arusha

SERIKALI kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye imevifungia kwa muda usiojulikana vituo vya Radio 5 ya Arusha inayomilikiwa na Robert Lowassa, ambaye ni mtoto wa mwanasiasa Edward Lowassa, na Magic FM ya Dar es Salaam kwa sababu za uchochezi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Waziri Nape amesema kuwa vituo hivyo kwa nyakati tofauti zilitangaza habari ambazo ndani yake zina uchochezi. “Adhabu hii ya kuvifungia kwa muda vituo hivyo viwili inaanza leo (Agosti 29 2016) hadi pale kamati itakapomaliza kazi yake,” alisema Nape.
Aidha, amesema kuwa ameiagiza Kamati ya Maudhui ya vyombo vya habari kuviita vyombo hivyo na kuvihoji kwa kina kisha kumshauri hatua zaidi ya kuchukua.

Comments