Featured Post

LOWASSA, MBOWE, MNYIKA WALIPOKAMATWA JANA

By Suzan Mwillo, Mwananchi
Dar es Salaam. Viongozi wa Chadema jana walikamatwa na polisi na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano.
Akizungumzia kukamatwa kwa viongozi hao Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema waliokamatwa na polisi kwa ajili ya mahojiano ni Edward Lowassa, Freeman Mbowe, John Mnyika, Dk Vincent Mashinji na  Said Issah                        
“Tulikuwa kwenye kikao cha Kamati Kuu kilichojumuisha wajumbe na wabunge kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya chama. Jumla ya wajumbe walikuwa 170. Tukiwa kwenye kiako walikuja watu wanasema tunatakiwa polisi kwa sababu tumekiuka agizo la lilitokataza mikutano.”
CHANZO: MWANANCHI

Comments