Featured Post

ASASI YA FEDHA YAWAKUMBUSHA WANACHUO UMUHIMU WA KUWEKA AKIBA


Mkurungezi mtendaji wa Asasi ya Fedha Jafari Selemani akisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa warsha iliyofanyika katika Chuo cha Kilimanjaro Insitute college  na kuwakutanisha wanavyuo zaidi ya mia 2 hapa jijini Dar es salaam ambapo alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuwa na tabia ya kuweka akiba na kujiandaa na maisha ya uzee ambapo Moto wa asasi hiyo ni "UHURU WA KIFEDHA NI WAJIBU WAKO " kulia kwake ni mtaalamu wa biashara na mhamasishaji wa vijana Fasili  Boniface   mapema mwishoni wa wiki iliyopita.
Mhamasishaji wa vijana Mussa Mashauri akitoa mada kuhusu Vijana na Utendaji kazi katika warsha hiyo iliyoandaliwa na Asasi ya Fedha iliyofanyika katika chuo na Kilimanjaro Insitute college na kuwakutanisha wanachuo zaidi ya 200 toka chuo cha UDSM,Ustawi wa jamii, Teku , St Joseph na Kilimanjaro Insitute college na kushoto kwake ni Murungezi Mtendaji wa KONCEPT na Mhamasishaji wa Vijana Krantz Mwantepele mapema mwisho wa wiki iliyopita.
Mmoja wa wanachuo waliohudhuria warsha hiyo akiuliza swali kwa mwongoza Mada Musa Mashauri.
Mtaalamu wa Biashara na Mhamasishaji wa vijana Fasili Boniface akiongoza mada kuhusu "Siri za jinsi ya kupata Ajira " katika warsha hiyo iliyoandaliwa na Asasi ya Fedha mapema mwishoni mwa wiki iliyopita katika chuo cha Kilimanjaro Insitute college na kukutanisha wanachuo zaidi ya mia 200 hapa jijini Dar es salaam..
Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT na mhamasishaji wa vijana Krantz Mwantepele akisitiza jambo wakati akiongoza mada kuhusu "Siri za uhuru wa kifedha na fursa ambazo zipo nchini vijana wanaweza kujiajili na kutengeneza thamani kwa  jamii inayowazunguka ,katika warsha iliyofanyika mapema mwishoni mwa wiki iliyopita katika chuo cha Kilimanjaro Insititute college,
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakisiliza kwa makini mada toka kwa Mkurungezi  Mtendaji wa Koncept Krantz Mwantepele mapema mwa wiki iliyopita.
Mkurungezi Mtendaji wa Koncept akiongoza washiriki wa warsha hiyo kula kiapo kuwa wanaamini nguvu ya mafanikio ipo ndani yao na ni wajibu wao kutafuta fursa na kutimiza ndoto zao
Mkurungezi wa Asasi ya Fedha Jafari selemani akitoa neno la kufunga warsha hiyo iliyofanyika katika chuo cha kilimanjaro na kukutanisha zaidi mia mbili kutoka vyuo vya UDSM , TEKU, USTAWI WA JAMII , ST JOSEPH NA KILIMANJARO INSITUTE COLLEGE mapema wiki iliyopita katika chuo cha Kilimanjaro Insitute college .

Comments