Featured Post

MBUZI WA MAZIWA JAMII YA OBERHASLI NI BORA KAMA ALPINE



 Hili ni beberu la mbuzi jamii ya Oberhasli
 Jike la Oberhasli
Majike wa Oberhasli
Mbuzi hawa jamii ya Oberhasli wanafaakwa maziwa na ni jamii ya Alpine ambao wanapatikana kwa wingi nchini Uswisi ambako ndiko asili yao. Ni miongoni mwa jamii za mbuzi wa maziwa ambao wanaweza kumletea faida kubwa mkulima.
Zamani wakijulikana zaidi kama Swiss Alpine kutokana na asilia yao kuwa kwenye Milima ya Alps hasa katika wilaya ya Oberhasli katika eneo la Bernese Oberland katikati ya Uswisi, mbuzi hawa wanafahamika kutokana na tabia ya upole. Rangi ya ngozi ni udongo mwekundu lakini wana mabaka meusi, ingawa baadhi ya majike ni weusi kabisa.
Mbuzi jike mkubwa ana uzito wa kilogramu 54 wakati beberu ana uzito wa kilogramu 68. Kimo cha jike ni sentimeta 71 wakati dume ni sentimeta 76.
Jike wa Oberhasli anaweza kuzalisha wastani wa lita 726 kwa mwaka za maziwa yenye wastani wa asilimia 3.6 ya mafuta.
Kama unataka kuwafuga mbuzi hawa, ni vyema ukamtafuta ofisa mifugo aliye jirani nawe ili akuelekeze namna ya kuwapata.
Kwa makala mbalimbali za kuhusu ufugaji wa mbuzi, endelea kuperuzi kwenye mtandao huu wa www.maendeleovijijini.blogspot.com.

Comments