Featured Post

HAWA NDIO MBUZI WA MAZIWA JAMII YA SAANEN



 Beberu la Saanen
Jike la Saanen

 

Na Daniel Mbega
Mbuzi jamii ya Saanen ni wakubwa na ndio watulivu zaidi kati ya jamii za mbuzi wa maziwa. Saanen ama Holstein ni mbuzi wazuri zaidi kwa maziwa ambao wanatoa maziwa mengi sana ingawa yana mafuta kidogo kulingana na maziwa ya mbuzi wengine. Wastani wa mafuta ni asilimia 2.5 hadi 3.5.

Mbuzi jike wa Saanen anaweza kutoa wastani wa paundi 1,900 za maziwa kwa mwaka. Kwa kawaida jike mkubwa anaweza kuwa na uzito wa kilogram 65 wakati beberu anaweza kuwa na uzito wa kilogramu 77.
Utawatambua mbuzi hao kutokana na umbile lao kubwa na tabia ya upole na utulivu, huku ngozi zao zikiwa laini na rangi ya maziwa na nyeupe. Masikio yao yamesimama kuelekea mbele.
Mbuzi hawa hawapendi sana jua na wanazalisha maziwa mengi katika mazingira ya baridi. Kama unawafuga kwenye maeneo ya joto kama Pwani, ni vyema kuwatengenezea vivuli vya kutosha.
Mbuzi hawa ni wapole na wafugaji wanawapenda kwa tabia hiyo kwa sababu ni wepesi kuwahudumia hata na watoto.
Asili ya mbuzi jamii ya Saanen ni kwenye Bonde la Saanen kusini mwa Canton Berne, Uswisi. Mwaka 1893 maelfu kadhaa ya mbuzi hawa walitolewa kwenye bonde hilo na kusambazwa Ulaya. Kati ya mwaka 1904 na miaka ya 1930, takriban mbuzi 150 wa Saanen walisafirishwa kupelekwa Marekani kutokea Uswisi.

Ikiwa una maoni au ushauri, usisite kunipigia au kunitumia ujumbe wa simu au whatsapp kupitia namba 0656 331974 au nitumie barua-pepe: maendeleovijijini@gmail.com.

Comments