Featured Post

SERIKALI YAWATOA HOFU WATANZANIA KUHUSU UPATIKANAJI MAFUTA YA NDEGE



Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam ili kujionea hali ya upatikanaji wa mafuta ya ndege baada ya kugundulika baadhi ya shehena ya mafuta hayo yaliyoingizwa nchini yalikuwa yamechanganyika na mafuta ya petroli.


Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam ili kujionea hali ya upatikanaji wa mafuta ya ndege baada ya kugundulika baadhi ya shehena ya mafuta hayo yaliyoingizwa nchini yalikuwa yamechanganyika na mafuta ya petroli.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongozana na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam eneo yalipo matanki ya mafuta ya kampuni ya GAPCO ili kujionea hali ya upatikanaji wa mafuta ya ndege baada ya kugundulika baadhi ya shehena ya mafuta hayo yaliyoingizwa nchini yalikuwa yamechanganyika na mafuta ya petroli.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni wa Kampuni ya Oryx Energies Godifrey Fernandes akimuonesha Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo baadhi ya maeneo yanapohifadhiwa mafuta wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam.

Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo (wa pili mtasari wa kwanza kulia) akiongozana na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta eneo la “Deport” ya PUMA wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta katika leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya madereva wanaosafirisha mafuta ndani na nje ya nchi leo jijini Dar es salaam.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
28/05/2016
Serikali imewatoa hofu na kuwahakikishia Watanzania na abiria wanaotumia usafiri wa anga nchini kwamba mafuta ya ndege yapo ya kutosheleza matumizi kwa muda wa siku 14 wakati shehena nyingine za mafuta hayo zinaendelea kuingia nchini.
Hayo yamesememwa na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo alipofanya ziara leo jijini Dar es salaam kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta ili kujionea hali ya upatikanaji wa mafuta ya ndege nchini baada ya kugundua baadhi ya shehena ya mafuta hayo yaliyoingizwa nchini yalikuwa yamechanganyika na mafuta ya petroli.
“Mafuta ya ndege yapo na ndege zitaendelea kufanya safari kama ratiba zao zilivyopangwa na Watanzania msiwe na wasiwasi, tumejiridhisha, mafuta yanatosheleza kwa muda wa siku 14 wakati hatua ya shehena nyingine kuingia nchini zinaendelea” alisema Prof. Muhongo.
Ziara hiyo ya Waziri Prof. Muhongo inafuatia kugundulika kwa mafuta ya ndege yaliyoingizwa nchini mapema mwezi Mei mwaka huu, ambayo hayafai kwa matumizi yaliyokusudiwa kutokana na kuchanganywa na mafuta ya petroli.
Aidha, Prof. Muhongo ameitaka kampuni ya Sahara Energy Resources yenye makao yake makuu nchini Nigeria ambayo ndio ilioingiza mafuta hayo nchini, kusimamisha shughuli zake mara moja hadi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi.
Imeonekana si mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kuingiza mafuta machafu nchini, hatua iliyomfanya Waziri huyo kuchukua msimamo huo wa Serikali hadi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi.
Akizungumzia hatua hiyo na hali ya mafuta nchini, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Uingizaji Mafuta kwa Pamoja nchini, Michael Mjinja amesema kuwa mafuta ya ndege yapo na yanatosheleza kwa wiki mbili kuanzia sasa.
Mjinja aliongeza kuwa wanakuhakikisha uhaba wa mafuta hayo hautokei tena nchini ambapo wanaendelea kushirikiana na kampuni ya Total na SP Rwanda ambazo hadi sasa ndio zenye mafuta safi yanayokubalika kwa matumizi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TIPER iliyoko eneo la Kigamboni jijini Dar es salaam, Stephane Gay amesema kuwa kampuni yake ina nafasi ya kutosha ya kuyahifadhi mafuta yote ambayo hayastahili kutumika ili matanki na mitambo ya kampuni zote zilizopata mafuta hayo yafanyiwe usafi upya tayari kwa kuweka mafuta safi yanayoingia nchini.
Ziara ya Waziri Prof. Muhongo imehusisha kutembelea matanki ya kampuni tano za mafuta ikiwemo Puma, GAPCO, Oil Com, TIPER pamoja na Kampuni ya Oryx Energies.




Comments