Featured Post

PLATINI ATAKA TIMU 40 KOMBE LA DUNIA


RAIS wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) Michel Platini anataka fainali za Kombe la Dunia zipanuke kutoka timu 32 za sasa hadi 40.
Nyota huyo wa zamani wa Ufaransa mwenye miaka 58 amependekeza hayo baada ya rais wa FIFA kwamba nchi nyingi kutoka Afrika na Asia zinaweza kufuzu kwa migongo ya zile za Ulaya.
"Badala ya kuziondoa baadhi ya nchi za Ulaya, tunatakiwa tuwe na timu 40 kwenye Kombe la Dunia. 
"Tunaweza kuongeza mbili kutoka Afrika, mbili kutoka Asia, mbili kutoka Amerika na moja kutoka Ulaya. Naunga mkono wazo hili moja kwa moja."
Fainali za kwanza za Kombe la Dunia 1930 zilihusisha timu 13, idadi ikapanda hadi 16 miaka minne baadaye na 24 mwaka 1982, na ongezeko la timu 32 mwaka 1998.
Ulaya ina nafasi 13 katika utaratibu wa sasa, wakati Afrika ina nafasi tano, Asia nafasi nne pamoja na moja ya mtoano.
Wazo la Platini la kuwa na timuj 40 linamaanisha kutakuwepo na makundi nane yenye timu tano kila moja kwenye fainali za Kombe la Dunia ambalo linakinzana na mfumo wa sasa wenye makundi nane yenye timu nne kila moja.
Wazo hilo linaweza kutekelezwa katika fainali za mwaka 2018 nchini Russia na kwa mujibu wa Platini, mashindano hayo yataongezwa siku tatu zaidi.
"Soka inabadilika na sasa tuna vyama 209," alisema Platini, ambaye anatarajia kuchuana na Blatter kwa nafasi ya urais wa FIFA mwaka 2015.
"Kuna nchi nyingi, sasa kwa nini tuzipunguze? Arobaini ni idadi ambayo siyo mbaya.
"Kutakuwa na siku tatu zaidi za mashindano na mnawafurahisha zaidi watu."  
CHANZO: BBC

Comments