- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini Blog
WANYAMA wa wa
kufugwa wao wa aina nyingi sana. Wapo ambao wanafugwa kwa ajili ya kitoweo,
wapo wanaofugwa kwa mapambo, wapo tunaowafuga kama wanyama-kazi, na wapo pia wa
mapambo ambao tunawatumia pia kwa ulinzi.
Ng’ombe, mbuzi,
kondoo, nguruwe, sungura, simbilisi au sili, kuku na jamii zote za ndege, hawa
tunawafuga kwa ajili ya kitoweo.
Maendeleo Vijijini inatambua kwamba, wanyama wanaofugwa kwa
ajili ya wanyama-kazi ni punda na farasi, lakini pia ng’ombe anatumika kama
mnyama kazi kwa kuvuta mikokoteni na kulima kwa kutumia plau pezi, wakati
ambapo farasi anaweza kutumika kwa usafiri huku punda akitumika kubeba mizigo
na hata kuvuta mikokoteni.
Paka anafugwa
kwa ajili ya mapambo, lakini ni mlinzi pia kwa sababu anapambana na wanyama
wadogo waharibifu, hususan panya.
Sungura nao wapo
wanaofugwa kwa mapambo na wapo wanaofugwa kwa nyama na mambo mengine.
Mbwa ndiye
mnyama ambaye kwa asilimia kubwa anafugwa kwa ajili ya ulinzi, japo mara chache
hufugwa kwa mapambao kutegemeana na aina ya mbwa mwenyewe.
MaendeleoVijijini leo inazungumzia kuhusu aina mbalimbali za mbwa, hususan wenye uwezo
mkubwa na akili kuliko jamii nyingine.
Unaweza kushangaa,
lakini wanyama hawa ni werevu na aina zifuatazo zinawaelezea kwa kina zaidi;
1 - BORDER
COLLIE
Mbwa jamii ya Border
Collie walianza kufugwa kwa nia ya
kukusanya na kuchunga kondoo katika eneo la milima la mpaka wa Scotland na
England. Mbwa hawa wanafahamika kutokana na mtazamo wao, yaani macho, ambao
huutumia kulinda kundi la kondoo.
Kondoo wenyewe
wakiwaona tu wanatulia kwa namna wanavyowatazama.
Mbwa hawa wana
nguvu nyingi, stamina, na wana bidii ya kazi, mambo yanayomfanya awe mbwa bora
zaidi kwa ajili ya kuchunga, na ndiyo maana anaitwa mbwa mchungaji; mpaka sasa
bado anatumiwa kuchunga kondoo katika mashamba makubwa na ranchi za wanyama
ulimwenguni.
Maendeleo Vijijini inatambua kwamba, mbwa wa jamii ya
Border Collie aliyefunzwa kwa kiwango kikubwa na mwenye akili pia anaweza
kushiriki katika mashindano na michezo ya wanyama, kama utiifu, kuruka,
kukimbi, kukimbiza mpira na mashindano mengine kama hayo.
Kwa ujumla, mbwa
jamii ya Border Collies wana maumbo ya kati na ngozi ya rangi mbalimbali,
japokuwa rangi nyeupe na nyeusi ndiyo maarufu. Mbwa dume wa jamii hii ana urefu
wa kati ye sentimeta 48 hadi 56 wakati jike ana urefu wa kati ya sentimeta 46
na 53.
Mbwa wa jamii ya
Border Collies ndio wanaotajwa kuwa na akili kuliko wote duniani na imekuwa ni
jamii maarufu kama mbwa wa mapambo kutokana na kufundishika kufanya mambo
mbalimbali.
Mbwa hawa wanaweza
kuishi kati ya miaka 10 na 14, ingawa wastani wao ni miaka 12. Chanzo kikuu cha
vifo vyao ni saratani (23.6%), umri mkubwa (17.9%) na matatizo ya ubongo
(9.4%).
2 – POODLE
Mbwa wa jamii ya
Poodle wako kundi la mbwa wa kawaida na wamegawanyika katika makundi matatu au
manne ambayo ni Standard Poodle,
Medium Poodle, Miniature Poodle na
Toy Poodle. Wanapatikana katika
rangi mbalimbali.
Maendeleo Vijijini inajua kwamba, mbwa hawa wanashika nafasi
ya pili kwa kuwa na akili nyingi nyuma ya Border Collie, lakini jamii hii wana
uwezo mkubwa wa kushiriki michezo mingi ya wanyama pamoja na shughuli
mbalimbali, wana
Toy Poodles walishinda
mashindano ya "Best in Show" mwaka 1966 na 1982. Standard Poodles walishinda
katika miaka ya 1955, 1985, 2002 na 2014.
Asili ya mbwa
hawa inatatiza ingawa inaelezwa kwamba ni Ujerumani ambako walikuwa
wakijulikana kama Pudelhund. Neno Pudel linatokana na lugha ya Kijerumani
likimaanisha ‘kumwaga’, na neno Hund (maana yake mbwa). Wengine wanasema
asili yake ni Ufaransa kutokana na mbwa aina ya Brbet ambaye inawezekana
alipandishwa na jamii ya mbwa kutoka Hungary. Huko Ufaransa wanafahamika kama
retriever kutokana na kutumiwa kutafuta vitu majini na wanajua kuogelea.
Mbwa wakubwa,
yaani Standard Poodle, ni wawindaji wakubwa na wanaweza kuwinda hata
ndege, wanaweza kuruka kwenye mashina ya miti na kadhalika. Wana akili sana
kiasi kwamba wanapoelekezwa wanaelewa mara moja.
Katika maandiko
na tafiti mbalimbali ambazo MaendeleoVijijini inazo, mbwa wa jamii hii waliwahi kutumiwa hata kwenye vita
kuanzia karne ya 17, na wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia walitumika pia hasa
kwenye majeshi ya majini.
Katika kipindi
cha miaka 20 iliyopita huko Amerika ya Kaskazini, mbwa wa jamii ya Standard
Poodle wamerejeshwa kwenye kazi yao ya mwanzo kabisa kama wawindaji wa bata na
ndege.
Umri wa kuishi
wa mbwa hao ni kati ya miaka 11.5 hadi 12. Vyanzo vikuu vya vifo vyao ni
saratani (30%), uzee (18%), GDV (6%), na magonjwa ya moyo (5%).
3 - GERMAN SHEPHERD / ALSATION
Mbwa wa jamii ya German Shepherd (Kijerumani: Deutscher Schäferhund) ni jamii ya mbwa wa maumbile ya kati na
makubwa wanaofanya kazi ambao asili yao ni Ujerumani.
Awali huko
Uingereza walijulikana kama Alsatian. Tangu ilipoendelezwa mwaka 1899,
jamii ya Mbwa Mchungaji wa Kijerumani - German Shepherd – walikuwa wakitumika
kuchunga kondoo.
Tangu wakati
huo, kutokana na nguvu zao, akili, uwezo wa kufundishika, na utii, mbwa hawa
wanapendwa ulimwenguni kote kwa ajili ya kazi mbalimbali, ikiwemo kuwasaidia
walemavu, kutafuta na kuokoa, polisi na majeshi pia yanawatumia sana. Ndio wanaotumiwa
hata kukamata dawa za kulevya, mabomu na kadhalika.
Mbwa
Wachungaji wa Kijerumani wana maumbo ya kati na makubwa. Kimo chao ni kati ya
sentimeta 60 – 65 kwa madume na sentimeta 55-60 kwa majike wakati uzito wao ni
kati ya kilogram 30 – 40 kwa madume na kilogram 22 – 32 kwa majike.
4 - GOLDEN RETRIEVER
Golden
Retriever mi jamii ya
mbwa wakubwa wanaofugwa kama mbwa wa bunduki – gun dogs – kwa ajili ya kutafuta
na kukamata mabata maji na ndege wakati wa uwindaji, na waliitwa watafutaji kwa
sababu ya uwezo wao wa kuwakamata ndege bila kuwadhuru na kuwapeleka kwa
wahusika.
Mbwa hawa
wanapenda sana kuogelea majini na ni rahisi kuwafundisha misingi na mbinu za
hali ya juu.
Mbwa hawa ambao
wanajiamini sana, wana uwezo wa kuishi kati ya miaka 11 na 12.
Asili ya mbwa
hawa ni Scotland katikati ya karne ya 19. Wakati huo uwindaji wa kanga ulikuwa mchezo
maarufu kwa matajiri wa Uskochi.
5 - DOBERMAN
PINSCHER
Mbwa
jamii ya Doberman Pinscher wana maumbile makubwa ya kati na walianza
kufugwa mwaka 1890 na Karl Friedrich Louis Dobermann, mtoza
ushuru wa Ujerumani. Meno yake ni marefu na kama watang’ata basi wanaleta
madhara makubwa.
Mbwa
wa kawaida wa jamii hii ana urefu wa kati ya sentimeta 69 hadi 72. Dume mara
nyingi huwa na uzito wa kilogram 40 hadi 45 na jike kilogram 32 hadi 35.
6 - SHETLAND
SHEEPDOG
Shetland
Sheepdog, au Sheltie,
kama jina lao lilivyo, ni mbwa wachungaji. Jina la asili la mbwa hawa ni Shetland
Collie, lakini hili likaleta mkanganyiko miongoni mwa wafugaji wa mbwa jamii
ya Collie wakati huo, hivyo jamii hii ikaitwa Shetland Sheepdog.
Kulingana
na tafiti mbalimbali ambazo MaendeleoVijijini inazo, mbwa hawa wadogo kwa maumbile wana akili, wanabweka sana,
wanafurahishhah, wana nguvu na wanafanya kazi kwa nguvu. Jamii hii ilitambuliwa
rasmi la klabu maarufu ya jamii za mbwa ya The
Kennel Club mnamo mwaka 1909.
Historia
yake ya awali haijulikani vizuri. Japokuwa kinachojulikana ni kwamba mbwa wa
Sheltie ni kutoka katika uzao wa Collie. Sheltie ni uzao wa mbegu ya mbwa jamii
ya Scottish
Collie na King Charles Spaniel. Iliendelezwa kwa nia ya
kuchunga kondoo katika Kisiwa cha Shetland, ambako fukwe zake zenye miinuko
zimesababisha kuwepo kwa wanyama wengine wadogo.
Lakini
leo hii Sheltie ni mbwa wanafugwa kwa ajili ya ulinzi shambani na kama wanyama
wa mapambo. Awali walikuwa wadogo sana wakiwa na kimo cha inchi 8 hadi 12
kutoka mabegani kabla ya kuwapandisha na jamii ya Collie kupata jamii ya sasa.
Kwa
ujumla, mbwa wa jamii ya Sheltie wana uzito wa kilogram 5 hadi 11. Madume yana
urefu wa sentimeta 37 na majike 36.
Sheltie
wana uwezo mkubwa wa akili na wanashika nafasi ya sita kati ya jamii 132 za
mbwa duniani.
Japokuwa
ni wafupi, lakini wanaweza kuruka hata kwenye ukuta wa urefu wa meta moja na
nusu na wanashiriki katika michezo mbalimbali ya mbwa.
7 - LABRADOR RETRIEVER
Mbwa wa jamii ya Labrador Retriever, ambao pia wanafahamika tu kama Labrador, wako
katika kundi la mbwa watafutaji na wachunguzi. Jamii hii ya mbwa ni miongoni
mwa mbwa maarufu Marekani na Uingereza.
Kutokana na
uwezo wao, Labrador wanafundishwa kuwaongoza wasioona katika nchi nyingi,
lakini pia wanatumiwa na polisi katika sehemu mbalimbali kwa ajili ya kunusa
vitu vya hatari zikiwemo dawa za kulevya na kadhalika.
Awali
mbwa wa Labrador Retriever walifahamika kama St. John's water dog, mbwa wa St. John, au
Lesser Newfoundland. Wakati mbwa hao walipopelekwa England katika eneo la
Labrador ndipo wakaitwa Labrador Retrievers kwa sababu walitumika kuzamia na
kutafuta vitu kwenye Bahari ya Labrador.
Mbwa
wa Labrador wana maumbile ya kati na makubwa, huku madume yakiwa na uzito wa
kati ya kilogram 29 na 36 na majike kilogram 25 na 32. Kimo chao ni kati ya
sentimeta 57 na 62 kwa madume na sentimeta 55 na 60 kwa majike.
Mbwa
hawa ni wakali wanapowajibika, lakini ni wapole kwa ujumla wake, wanapenda
kutembea na wana asili ya kuchunguza sana, ndiyo maana ni rahisi kuwafundisha
hata kutafuta vitu mbalimbali. Wanatumika kwenye majeshi ya majini na nchi
kavu. Wanaweza kufuatilia na kuwachunguza wanamagendo.
Wana
uwezo mkubwa wa kunusa na ndiyo maana hata polisi huwatumia kunusa harufu ya
vvitu mbalimbali, ikiwemo dawa za kulevya, kutambua wanamagendo, wezi, magaidi
na kadhalika.
Mbwa
hawa wanaweza uwezo wa kuishi kati ya miaka 10 na 12.
8 – PAPILLON - KIPEPEO
Mbwa
jamii ya Papillon ni wadogo kutoka jamii ya mbwa wanasesere wa Continental
Toy Spaniel. Pamoja na udogo wao, lakini mbwa hawa ambao ni jamii ya zamani
sana wana akili. Papillon ni jina la Kifaransa ambalo maana yake ni ‘kipepeo’
na Wafaransa, ambako ndiko iliko asili ya mbwa hao, walimwita hivyo kwa jinsi
alivyo mdogo.
Mbwa
hawa daima ni marafiki na wanapenda kutembea sana. Hawana aiba na wana nguvu. Japokuwa
ni mbwa mwenye urafiki, lakini lazima kumwangalia anapokuwa na watoto, kama
ilivyo kwa mbwa wengine, kwa sababu akichokozwa ni balaa.
Mbwa
huyu, pamoja na udogo wake, lakini ana uwezo wa kuishi hadi miaka 17.
9 –
ROTTWEILER
Rottweiler ni jamii ya mbwa mwenye umbile la kati
na kubwa ambaye asili yake ni Ujerumani ambako walijulikana kama Rottweiler
Metzgerhund, ambayo
maana yake ni mbwa wachinjaji wa Rottweil, yaani Rottweil butchers' dogs, kwa
sababu mojawapo ya kazi zao ilikuwa kuchunga ng’ombe na mifugo mingine na
kuvuta mikokoteni yenye nyama kwa ajili ya kupeleka sokoni.
Hii iliendelea
hadi katikati ya karne ya 19 wakati wa ujio wa reli ambapo sasa kazi yao
ikabakia kuchunga mifugo.
Kwa sasa mbwa
hawa wanatumika kama watafutaji na waokoaji, mbwa waongozaji kwa wasioona, mbwa
walinzi na mbwa wa polisi
Mbwa wa umbile
la kawaida ana urefu wa sentimeta 61 hadi 69 kwa dume, wakati jike ni sentimeta
56 hadi 63, na wana uzito wa kilogram kati ya 50 na 60 kwa dume na kilogram 35
na 48 kwa jike.
Usicheze na mbwa
hawa, kwa sababu licha ya utii, ukakamavu, welekevu na jitihada ya kazi, lakini
ni wakali. Ukimwamuru tu, kazi imekwisha.
Kama mfugaji wa
mbwa jamii ya Rottweiler hatakuwa makini, anaweza kusababisha madhara makubwa
kwa jamii na ndiyo maana wengi wanafugwa hata na majeshi ambako wanaweza
kuwadhibiti.
Mbwa hawa wanaweza
kuishi kati ya miaka 8 hadi 10.
10 -
AUSTRALIAN CATTLE DOG
Australian
Cattle Dog (ACD),
au Cattle Dog, ni mbwa mchunga ng’ombe ambaye asili yake ni Australia ambako
alifugwa maalum kwa kuchunga ng’ombe katika maeneo ambayo ni vigumu binadamu
kupita kwa urahisi.
Mbwa hawa wana
maumbile ya kati, wana nguvu, wakakamavu na wana akili huku wakipendelea zaidi
kuwa huru, siyo kufuatwa fuatwa.
Wanaitikia vyema
kwenye mafunzo, hasa kama mafunzo hayo yanavutia na magumu.
Awali walifugwa
kwa ajili ya kuchunga kwa kuwang’ata ng’ombe. Ni mbwa walinzi wazuri kwa
familia kwa sababu wanaweza kumwelewa kila mtu ndani ya familia, ambapo kama
itatokea mwanafamilia yuko hatari, wanaweza kutokea kusaidia.
Mbwa hawa
wanaweza kuishi kati ya miaka 12 hadi 14.
NI JUU YAKO,
UNATAKA KUFUGA MBWA WA AINA GANI KATI YA HAWA.





















































Comments
Post a Comment