- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wadau wa
habari kutoka taasisi na vyombo mbalimbali vya habari nchini wameomba kukutana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ili kuimarisha
mahusiano mema wakati ambao taifa linaelekea kwenye uchaguzi mdogo mwaka huu
pamoja na uchaguzi mkuu hapo mwakani.
Pamoja na
mambo mengine, wadau hao waliazimia hilo juzi kwenye warsha ya kuwajengea uwezo
viongozi wa vyombo vya habari ili kuangalia na kuripoti kwa weledi habari za
uchaguzi, iliyofanyika jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Aprili 15, 2019
ikiandaliwa na taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la
Tanzania kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani.
Akisisitiza
hilo, Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka taasisi ya Internews, Wenceslaus Mushi
alisema wadau wa habari pamoja na maafisa kutoka NEC ni vyema wakakutana kwenye
warsha ya pamoja na kujengeana weledi namna kila upande unaweza kutimiza
majukumu yake kwa mujibu wa sheria katika kipindi cha uchaguzi na hivyo kuondoa
mkanganyiko ambao wakati mwingine hujitokeza ikiwemo waandishi wa habari
kuzuiliwa kuingia kwenye vyumba vya kupigia kura.
Mkurugenzi
wa taasisi ya MISA Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa alisema juhudi zitaendelea
kufanyika ili kuwakutanisha wadau wa habari pamoja na wasimamizi wa uchaguzi
ili kuimarisha mahusiano hatua itakayosaidia kila upande kutimiza vyema
majukumu yake na hivyo kuwa na uchaguzi wa amani.
Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka taasisi ya Internews, Wenceslaus Mushi akizungumza kwenye warsha hiyo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akifuatilia kwa umakini majadiliano kwenye warsha hiyo.
Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika (V.O.A), Dkt. Mwamoyo Hamza akiwasilisha mada kuhusu aina ya maswali waandishi wa habari wanapaswa kuwauliza wagombea wakati wa uchaguzi. Alisema waandishi wa habari wanapaswa kuuliza maswali yanayojibu mahitaji ya wananchi na kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi ya kuwachagua viongozi wanaowataka.
Mshauri wa masuala ya Habari kutoka TMF, Dastan Kamanzi akiwasilisha mada kwenye warsha hiyo, akisisitiza waandishi wa habari kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi/kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Mkurugenzi wa taasisi ya "Tangible Initiatives For Local Development Tanzania", Geline Fuko akiwasilisha mada kwenye warsha hiyo ambapo alisisitiza vyombo vya habari kutoa fursa sawa kwa wanawake na makundi maalumu ikiwemo watu wenye ulemavu katika kuripoti habari za uchaguzi.
Mtaalamu wa masuala ya Mitandao ya Kijamii, Innocent Munggy akiwasilisha mada kuhusu matumizi sahihi ya mitandao hiyo hususani wakati wa uchaguzi ambapo alihimiza taasisi mbalimbali ikiwemo MISA Tanzania kutoa tuzo kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ili kuhamasisha matumizi sahihi.
Mhariri kutoka kampuni ya Mwananchi Communication, Bakari Machumu akichangia mada kwenye warsha hiyo.
Baadhi ya watendaji kutoka MISA Tanzania wakiwa kwenye warsha hiyo.
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo.
Comments
Post a Comment