- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu wa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisondoko ambacho ni miongoni mwa vijiji vilivyomo ndani ya Pori la Akiba la Mkungunero katika wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma ambapo ameagiza wananchi hao wasibughuziwe hadi hapo maamuzi yatakapotolewa juu ya hatma yao. Wengine ni kmati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya hiyo pamoja na Maafisa wa kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Kulia ni Mkuu wa wilaya hiyo, Sezaria Makota.
Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amezionya na kuzitaka Taasisi za
Uhifadhi kuacha tabia ya kuwabughudhi wananchi wanaoishi katika vijiji na
vitongoji 366 vilivyokutwa ndani ya Hifadhi katika maeneo mbalimbali nchini
mpaka hapo maamuzi ya Kamati ya Mawaziri saba iliyoundwa kushughulikia suala
hilo itakapokamilisha kazi iliyopewa na kuwasilisha ripoti kwa Mhe. Rais.
Hatua hiyo ni
kufuatia malalamiko kutoka kwa baadhi ya
wananchi wakiwemo wakulima na wafugaji
wanaoishi katika vijiji na vitongoji hivyo kudai kuwa wamekuwa
wakisumbuliwa na mifugo yao kukamatwa
mara mara kwa madai ya kukutwa imeingia ndani ya Hifadhi.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha
Kisondoko ambacho ni miongoni mwa vijiji vilivyomo ndani ya Pori la Akiba la
Mkungunero katika wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Mhe. Kanyasu amezitaka
taasisi hizo kufuata na kuzingatia
maelekezo yaliyotolewa na Serikali kuhusu wananchi wanaoishi katika
maeneo hayo.
Aidha, Mhe. Kanyasu
ametumia fursa hiyo kuwaonya wananchi
ambao wamekuwa wakivamia maeneo mapya ya Hifadhi kwa kisingizio cha kauli aliyoitoa Mhe. Rais
kuacha mara moja na kwamba yeyote
atakayekamatwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
"Wananchi ninao
walenga ni wale tu ambao walikuwa wakiishi Hifadhini kabla ya kauli ya Rais aliyoitoa mwanzoni mwa
mwaka huu" Alisisitiza.
Hata hivyo, Mhe Kanyasu
amebainisha kuwa Kamati ya Mawaziri saba iliyoundwa na kuzunguka nchi nchi
nzima imebaini kuwa kuna zaidi ya vijiji 820 ambavyo vimo ndani ya Hifadhi
mbali ya vile 365 vilivyobainishwa awali na kuwasihi wananchi wasiendelee kuvamia maeneo mengine.
Mhe. Kanyasu ameowanya baadhi ya askari wa
wanyamapori wanaoomba rushwa Kutoka kwa
wafugaji pindi wanapokamata mifugo yao
ili waweze kuiachia waache mara moja tabia hiyo akisisitiza kwamba askari yeyote atakayethibitika atachukuliwa
hatua kali za kinidhamu kwa mujibu wa Sheria za utumishi wa Umma.
Mkuu wa wilaya ya
Kondoa, Mhe. Sezaria Makota amewataka
wananchi hao kuendelea kuwa walinzi wa maeneo hayo huku wakisubili hatma ya
taarifa ya kamati ya Mawaziri saba itakayotolewa hivi karibuni.
" Baada ya taarifa
hiyo mtajua hatma yenu na kama hapa mtabaki
au mtahamishwa na kama mtahamishwa tutajua tutawapeleka eneo gani kwa ajili ya
malisho na kilimo." Alisema.
Akizungumza kwa niaba ya
Wananchi, Mwenyekiti wa kijiji cha Kisondoko, Ismail Said amemueleza Naibu
Waziri huyo kuwa baadhi ya askari wa wanyamapori wamekuwa wakikamata mifugo yao
na kuomba rushwa na pale makubaliano yanaposhindikana huondoka na mifugo yao.
Amesisitiza kuwa vitendo
hivyo vimekuwa vikichochea chuki baina ya wananchi na askari hao jambo
linalorudisha nyuma jitihada za Uhifadhi nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Sezaria Makota akizungumza na wananchi wa kijiji cha
Kisondoko kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.
Constantine Kanyasu katika kijiji
ambacho ni miongoni mwa vijiji vilivyoomo ndani ya Pori la Akiba la
Mkungunero katika wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma ambapo ameagiza wananchi hao
wasibughuziwe hadi hapo maamuzi yatakapotolewa juu ya hatma yao.
Baadhi
ya wananchi wa kijiji cha Kisondoko wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii alipokuwa akizungumza nao kuhusu mifugo yao kukamatwa mara kwa mara na
askari wanyamapori wa Pori la Akiba la Mkungunero katika wilaya ya Kondoa
mkoani Dodoma.
Diwani
wa kata ya Kisondoko, Mhe. Ismail Juma akizungumza na wananchi wa kijiji cha
Kisondoko kabla ya kumkaribisha Mkuu wa wilaya
Mhe. Sezaria Makota katika kijiji ambacho ni miongoni mwa vijiji
vilivyoomo ndani ya Pori la Akiba la Mkungunero katika wilaya ya Kondoa mkoani
Dodoma. (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)
Comments
Post a Comment