- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Ndugu Theobald
Maingu Sabi (kushoto) ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe
26, Machi 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki
ya NBC Ndugu Theobald Maingu Sabi ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
huyo amefika ofisini kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kujitambulisha akiwa
ameongozana na Meneja mahusiano na Serikali Bw. William Kalaghe pamoja na Afisa
Masoko wa NBC Bi. Neemarose Singo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
NBC Ndugu Theobald Maingu Sabi, Afisa
Masoko wa NBC Bi. Neenarose Singo pamoja na Meneja wa Mahusiano na
Serikali Ndugu William Kallaghe (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo
ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja
na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Ndugu Theobald Maingu Sabi
(kushoto) mara baada ya mazungumzo ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Comments
Post a Comment