- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua
Majalada ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Kongwa alipofanya ziara
kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi katika
halmashauri za mkoa wa Dodoma
Na Munir Shemweta,
DODOMA
NaibuWaziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula ameshangazwa na halmashauri za
wilaya ya Mpwapwa na Kongwa mkoani Dodoma kushindwa kuwafikisha katika Mabaraza
ya Ardhi na Nyumba wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi pamoja na baadhi yao
kupelekewa ilani za madai.
Dk Mabula ameziagiza
halmashauri hizo mbili kuhakikisha zinawafikisha wadaiwa hao katika Mabaraza ya
Ardhi kwa hatua zaidi ambapo alielezea kuwa huko maamuzi yake ni mawili ambapo
mdaiwa anatakiwa kulipa ama kunyanganywa miliki yake kufidia deni.
Naibu Waziri wa Ardhi
alitoa agizo hilo jana alipozitembelea wilaya hizo mbili ikiwa ni mfululilzo wa
ziara zake kutembelea halmashauri mbalimbali kwa nia ya kuhamasisha ukusanyaji
maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi.
Kwa mujibu wa Dkt Mabula,
halmashauri hizo zina wamiliki wengi wa viwanja wasiolipia kodi ya ardhi na
hivyo kuzifanya kudai kiasi kikubwa cha fedha lakini idara za ardhi zinashindwa
kuwachukulia hatua jambo linaloikosesha serikali mapapto.
Naibu Waziri wa Ardhi
alisema, halmashauri ya wilaya ya Kongwa inadai jumla ya shilingi milioni 152
kutoka kwa wamiliki wasiolipa kodi huku ile ya Mpwapwa ikidai milioni
128,013,696.90.
Afisa Ardhi Msaidizi wa
Halmashauri ya wilaya ya Kongwa Anjelina Ndemera alisema halmashauri yake
pamoja na kuwa na madeni kutoka kwa wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi lakini
haikuweza kutoa ilani za madai kwa wadaiwa hao.
Kwa upande wa wilaya ya
Mpwapwa, Mkuu wake wa Idara Anderson Mwamengo alisema halmashauri hiyo ina
wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi mia tatu na thelathini ambao
wameandikiwa na kukabidhiwa ilani hizo.
Dkt Mabula alisema, pamoja
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kuhimiza suala
la kulipa kodi na Wizara ya Ardhi kujitahidi kusaidia suala hilo lakini
halmashauri hazifanyi jitihada zozote katika kukusanya maduhuli ya Serikali
kupitia kodi ya ardhi.
‘’Kila siku inaelezwa
pelekeni ilani za madai ya kodi ya ardhi kwa wamiliki lakini hakuna ufuatiliaji
wowote unaofanywa na watendaji wa sekta ya ardhi jambo linalorudisha nyuma
jitihada za serikali ya awamu ya tano kukusanya maduhuli ya serikali.
Naibu Waziri wa Ardhi
aliziagiza halmashauri hizo mbili kufikia tarehe 31 Machi 2019 watendaji wake
wa sekta ya ardhi wawe wamewafikisha katika Baraza la Ardhi wadaiwa wote
waliopelekewa ilani za madai.
Aidha, Dkt Mabula ameitaka
idara ya ardhi kuhakikisha orodha ya wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi
waliopewa ilani za madai inafikishwa katika kila kikao cha kamati ya Uchumi na
Mazingira vya kila robo mwaka ya Baraza la Madiwani katika kila
halmashauri lengo likiwa kuitaka kamati husika kuelewa suala hilo na kufanya
ufuatiliaji.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoa
maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri (wa pili kushoto),
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpwapwa Paul Sweya na Mkuu wa Idara ya
Ardhi Anderson Mwamengo alipofanya ziara kuhamasisha ukusanyaji
maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi katika halmashauri za mkoa wa
Dodoma.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza
katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kongwa alipokutana na watendaji wa sekta ya
ardhi katika wilaya hiyo wakati wa ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya
serikali kupitia kodi ya ardhi katika halmashauri za mkoa wa Dodoma.
Baadhi
ya watendaji katika wilaya ya Kongwa wakiwepo wale wa sekta ya ardhi
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline
Mabula alipofanya ziara kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia
kodi ya ardhi katika halmashauri za mkoa wa Dodoma.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoa
maelekezo baada ya kukagua masijala ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya
Kongwa alipofanya ziara kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia
kodi ya ardhi katika halmashauri za mkoa wa Dodoma. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza
na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa (hawapo
pichani) alipofanya ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali
kupitia kodi ya ardhi, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri,
wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpwapwa Paul Sweya na kushoto ni
Kamishna Msaidizi wa Ardhi kanda ya Kati Ezekiel Kitlya.
Mkuu wa
Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi, akimuongoza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula kuelekea Masijala ya Ardhi katika
halmashauri ya wilaya ya Kongwa alipofanya ziara kuhamasisha ukusanyaji
maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi katika halmashauri za mkoa wa
Dodoma. Katikati ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt. Omar
Nkullo.
Comments
Post a Comment