- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akiingia katika jengo la Wizara
ya Viwanda na Biashara wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi katika Mji
wa Serikali Mtumba mkoani Dodoma, katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la
Nyumba Dkt Sophia Kongela na kushoto ni Mkurugenzi Dkt Maulid Banyani.
Na Munir Shemweta, DODOMA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline
Mabula amechochea kasi ya ujenzi wa ofisi za serikali katika eneo la Mtumba
mkoani Dodoma unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Kasi hiyo inatokana na ziara za mara kwa mara zinazofanywa na
Naibu Waziri huyo wa Ardhi katika eneo hilo kwa nia ya kuhakikisha ujenzi wake
unakamilika katika muda uliopangwa.
Akiambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa
.Dkt Sophia Kongela pamoja na Mkurugenzi wa Shirika Dkt Maulid Banyani jana,
Naibu waziri Mabula alijionea maendeleo makubwa ya ujenzi huo ambapo sasa
umefikia hatua ya kuezeka.
Mbali na kufikia hatua hiyo, kazi nyingi katika ujenzi huo
zinaenda kwa pamoja kama vile kuweka njia za umeme, tiles, utengenezaji
madirisha ya nondo pamoja na mashimo ya choo jambo linaloonesha
Shirika limejipanga kukamilisha kazi mapema tofauti na makampuni mengine ya
ujenzi yanayofanya kazi kwenye eneo la Mtumba.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akiangalia tiles katika jengo la Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba mkoani Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa Dkt Maulid Banyani.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akipita katika moja ya maeneo ya ujenzi wa ofisi katika Mji wa Serikali wa Mtumba mkoani Dodoma alipokwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi zinazosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).Wanaomfuatia kwa nyuma ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba Dkt Sophia Kongela na Mkurugenzi Dkt Maulid Banyani.
Kampuni ya Ujenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa katika eneo hilo
la Mtumba inajenga majengo ya ofisi nne za Wizara ya Ardhi Nyumba na
Maenendeleo ya Makazi, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Nishati pamoja
na Wizara ya Fedha na Mipango.
Akizungumza baada ya kukagua kwa mara ya pili ujenzi wa
ofisi hizo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Mabula
alisema kasi inayooneshwa na Shirika la NHC katika ujenzi huo ni ishara tosha
kuwa shirika hilo kupitia kampuni yake ya ujenzi lina uwezo mkubwa wa kujenga
majengo kwa haraka na yenye viwango.
Alisema, hata kama ujenzi wa ofisi zinazosimamiwa na shirika hilo
katika eneo la Mtumba utachelewa kidogo lakini ucheleweshaji huo utatokana na
MHC kutaka kujenga majengo ya uhakika na yenye ubora unaotakiwa.
Dkt Mabula ameendelea kutoa sifa kwa Ofisi ambazo majengo yake
yanasimamiwa na shirika la Myumba la Taifa kutokana na ukaribu inaouonesha
katika kipindi chote cha ujenzi kwa nia ya kuwa na majengo yanayokidhi mahitaji
ya Wakala wa Ujenzi Tanzania (TBA) na ofisi husika kwa kuwa mawazo ya pande
zote yatakuwa yamejumuishwa katika kutekeleza ujenzi huo.
Meneja wa Mradi wa Ujenzi
wa Ofisi za Serikali kutoka Shirika la Nyumba la Taifa Haikameni Mlekio
akimuonesha Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline
Mabula, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba Dkt Sophia Kongela na
Mkurugenzi wa NHC Dkt. Maulid Banyani maendeleo ya ujenzi katika ujenzi wa
ofisi katika Mji wa Serikali Mtumba mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akiangalia shimo la choo
katika wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi za Serikali katika Mji wa
Serikali Mtumba mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akiangalia moja ya vyumba
katika ofisi zinazojengwa katika Mji wa Serikali Mtumba mkoani Dodoma wakati
akikagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi hizo.
Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akiangalia madirisha ya
nondo ambayo yako tayari kupachikwa wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa
ofisi za serikali katika eneo la Mtumba. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la
Nyumba la Taifa Dkt Maulid Banyani.
Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akiingia katika eneo la
jengo la Wizara ya Fedha na Mipango alipowasili kukagua maendeleo ya ujenzi wa
ofisi zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa katika Mji wa Serikali Mtumba,
kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya NHC Dkt Sophia Kongela na wa pili kushoto ni
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa Dkt Maulid Banyani.
Comments
Post a Comment