- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi kuhusu matukio ya
utekwaji na kuuliwa kwa watoto katika Mkoa wa Njombe, ambapo aliwaasa wananchi
kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi katika juhudi za kukomesha matukio hayo.Picha na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri akizungumza na
wananchi kuhusu matukio ya utekwaji na kuuliwa kwa watoto katika
Mkoa wa Njombe, ambapo aliahidi kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi na Usalama
kukomesha matukio ya utekaji na kuuliwa kwa watoto.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkazi wa Njombe, Alex Msupilo akimuuliza maswali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni(hayupo pichani), juu ya hatua zilizochukuliwa na Serikali kukagua
leseni za waganga wa tiba asilia ambao wamekua wakitajwa kufanya tiba
chonganishi zinazopelekea kutokea kwa matukio ya utekaji na kuuliwa kwa watoto
katika mkoa huo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika kikao kidogo kilichohusisha Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Njombe na baadhi ya wananchi lengo ikiwa ni
kujadili juu ya matukio ya utekaji na kuuliwa kwa watoto mkoani hapo.Picha na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MASAUNI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA NJOMBE KUHUSU UTEKWAJI NA
MAUAJI YA WATOTO
Comments
Post a Comment