- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akizungumza wakati akikagua
mfumo katika ofisi za ardhi halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma
alipofanya ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya
ardhi.
Na Munir Shemweta, BAHI
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Dk Angeline Mabula amekutana na changamoto kubwa zinazoikabili
halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma kiasi cha kushindwa kuwabana
maafisa ardhi katika halmashauri hiyo.
Akiwa katika ziara yake ya kuhamasisha
ukusanyaji maduhuli ya Serikali kupitia sekta ya ardhi katika halmashauri
mbalimbali nchini jana, Dk Mabula aliikuta halmashauri ya Wilaya ya Bahi
ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu wa bajeti na
uhaba wa magari.
Naibu waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akizungumza na watendaji wa
sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Bahi mkoani Dodoma alipofanya
ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi.
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bahi Mwanahamisi Munkunda, na wa tatu kushoto ni
Mkurugenzi wa Halamashauri ya Wilaya ya Bahi, Leo Mavika.
Hali hiyo imesababisha halmashauri hiyo
kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo kama vile kukusanya maduhuli ya
serikali kupitia sekta ya ardhi, kuwapelekea wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi hati
za madai, kupima na kupanga viwanja pamoja na kwenda kutatua migogoro ya ardhi.
‘’Sekta ya ardhi ni idara nyeti sana ambayo
inaweza kuingizia seriali mapato mengi lakini kama haitawezeshwa kufanya kazi
ipasavyo kwa kupatiwa rasilimali fedha na vifaa kama magari basi itashindwa
kutekeleza majukumu yake na hivyo kuifanya serikali kukosa mapato kupitia sekta
hiyo.’’ Alisema Dk Mabula
Mkuu wa Idara ya Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya
Bahi Chediel Mrutu alimwambia Naibu Waziri Mabula kuwa, idara yake hajawahi
kupatiwa fedha za mgao wa ndani na bajeti yake kwa mwaka ni milioni mbili na
laki tano na kubainisha kuwa kiasi hicho wakati mwingine hakipatikani
chote. Kwa mujibu wa Mrutu idara yake haina gari la kuwawezesha kufanya
shughuli za ardhi ambazo wakati mwingine hutakiwa kwenda umbali mrefu
kushughulikia masuala ya ardhi.
Kufuatia hali hiyo Dkt. Mabula alitaka kufahamu
kiasi cha fedha za mgao inazopata idara nyingine kwenye halmashauri hiyo
kufuatia katika ziara zake kubaini idara ya ardhi kutengwa na kupewa kiasi
kidogo cha fedha ukilinganisha na halmashauri nyingine ambapo kwa upande wa
Bahi hakuna tofauti jambo lililomfanya kuishiwa nguvu na kusema halmashauri
hiyo inahitaji kusaidiwa.
Dk Mabula alisema kiasi cha milioni mbili na
laki tano inazopata halmashauri kwa mwaka haiwezi kufanya kitu kwa idara kama
ya ardhi yenye majukumu mengi jambo lililoifanya kukusanya milioni saba tu hadi
kufikia desemba mwaka jana huku ikiwekewa malengo ya milioni 47.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi
mkoani Dodoma Mwanahamisi Munkunda akizungumza wakati wa ziara ya Naibu waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula kuhamasisha
ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi.
Alisema kwa hali waliyo nayo halmashauri ya
Wilaya ya Bahi haiwezi kufikia asilimia hamsini ya malengo ya serikali na
kuagiza ofisi ya Kamishana Msaidizi Kanda kuangalia namna itakavyoweza
kuisaidia idara ya ardhi angalau iweze kutatua baadhi ya changamoto.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bahi Leo
Mavika alisema halmashauri yake inakabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji
mapato ambapo alisema kwa sasa inajitahidi kuhakikisha kiasi kidogo
kinachopatikana kinagawanywa kwenye idara zote za halmashauri huku idara ya
ardhi ikipewa kipaumbele kutokana na umuhimu wake na kuongeza kuwa halmashauri
hiyo kwa sasa ina magari mawili tu jambo linalowawia vigumu kutekeleza majukumu
ya kila siku.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mwanahamisi Munkunda alisema
ili halmashauri yake iweze kutoka ilipo mikakati madhubuti inahitajika ili
kuondokana na hali hiyo ambayo imekuwa ikiwakatisha tama watumishi kutokana na
kushindwa kutekeleza majukumu ipasavyo kutokana na changamoto zinazowakabili.
Mkuu wa Idara ya Ardhi
katika halmashauri ya Wilaya ya Bahi mkoa wa Dodoma Chediel Mrutu akitoa
maelezo kuhusiana na sekta ya ardhi wakati wa ziara ya Naibu waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula kuhamasisha ukusanyaji
maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi.
Comments
Post a Comment