- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali
Watu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Lusius Mwenda (kushoto) akiwa
ameongoza na Watumishi zaidi ya 50 wa Wizara hiyo wakipanda kilima kwenda kuangalia
michoro ya miambani katika kituo cha Utalii cha Kolo kilichopo wilayani
Kondoa mkoani Dodoma jana ikiwa lengo la ziara hiyo ni kuhamasisha utalii wa
ndani kwa Watumishi wa Serikali. Wa pili ni Mkuu wa Kituo cha Kolo, Zuberi
Mabie.
Mkuu wa Kituo cha Utalii, Kolo chenye
michoro ya miambani, Zuberi Mabie akiwa na watumishi wa Wizara ya Maliasili na
Utalii akiwaonesha michoro ya miambani katika kituo cha Utalii cha Kolo
kilichopo wilayani Kondoa mkoani Dodoma jana ikiwa lengo la ziara hiyo ni
kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watumishi wa Serikali.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali
Watu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Lusius Mwenda (katikati) akiwa
kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara hiyo walipotembelea katika
kituo cha Utalii, Kolo kilichopo wilayani Kondoa mkoani Dodoma jana ikiwa
lengo la ziara hiyo ni kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watumishi wa Serikali.
Mkuu wa Kituo cha Utalii, Kolo chenye
michoro ya miambani, Zuberi Mabie akizungumza na watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakati walipotembelea
kituo cha michoro ya miambani, Kolo
kilichopo wilayani Kondoa wakati
walipotembelea katika kituo hicho ikiwa la lengo la ziara hiyo ni kuhamasisha
utalii wa ndani kwa Watumishi wa Serikali.
Afisa Utalii wa Wizara ya Maliasili
na Utalii, Nina Kisando akiwa anatelemka kutoka kwenye kilele cha mlima baada
ya kuona michoro ya miambani Kolo ambacho ni kivuto cha Utalii cha aina yake.
Baadhi ya Maafisa wakiwa wameongozana
na Mtalii wa ndani wakiwa wanatelemka
kutoka kwenye kilele cha mlima baada ya kuona michoro ya miambani Kolo ambacho
ni kivuto cha Utalii cha aina yake.
Baadhi ya watumishi wakifurahia mara
baada ya kuteremka kwenye kilele cha mlima baada ya kuona michoro ya miambani
Kolo ambacho ni kivuto cha Utalii cha aina yake.
Baadhi ya michoro ya miambani Kolo
ambacho ni kivuto cha Utalii cha aina yake.
Baadhi ya Wanawake wa kimila wakiwa
wanaingia kwenye pango kwa ajili ya kufanya tambiko wakati wakati Watumishi wa
Wizara ya Maliasili na Utalii walipotembelea kituo cha michoro ya miambani, Kolo kilichopo
wilayani Kondoa wakati walipotembelea
katika kituo hicho ikiwa la lengo la ziara hiyo ni kuhamasisha utalii wa ndani
kwa Watumishi wa Serikali.
(PICHA NA LUSUNGU HELELA-MNRT)
NA LUSUNGU HELELA-DODOMA
Mkurugenzi wa Utawala na
Raslimali Watu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Lusius Mwenda ametoa
wito kwa watumishi wa Serikali kuwa mstari wa mbele kutembelea vivutio
vya utalii vilivyopo nchini kwa ajili ya kujifunza mambo mapya ikiwa
pamoja na kupumzisha akili.
Pia amewataka watumishi hao kujenga
utamaduni wa kutembelea vivutio hivyo ili waweze kuona na
kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo wanaweza kuanza
kuzifanya kwa ajili ya kujiingizia kipato ikiwa ni njia mojawapo ya
kuanza kujiandaa kwa ajili ya kustaafu.
Amefafanua kuwa kila mtumishi
wa Serikali anatakiwa kuanza kujiandaa kwa ajili ya kustaafu kuanzia ile siku
ya kwanza aliyoajiriwa.
Amesema watumishi walio wengi mara
baada ya kustaafu hali zao za kiuchumi huteteleka kwa vile katika kipindi
cha utumishi wao walikuwa hawatembelei maeneo tofauti na yale
waliyoyazoea kwa ajili ya kujifunza na kukutana na watu tofauti.
Ametoa Rai hiyo jana katika kituo cha
utalii Kolo kilichopo wilayani
Kondoa mkoani Dodoma alipokuwa ameongozana na Watumishi zaidi ya
50 kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii , Ikiwa ni moja ya jitihada za Wizara
hiyo kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watumishi wa Serikali kwa kuanza na
Watumishi wa Wizara yenye dhamana.
Kivutio cha Utalii, Kolo kipo ni kivutio mashuhuri sana kwa michoro yake ya miambani
kwa vile inafanana na michoro ya Afrika Kusini na kimebeba tamaduni za
waafrika.
" Tunataka Watumishi muwe
mabalozi wazuri kuanzia kwenye ngazi ya familia hadi ngazi ya taifa kwa
kuhamasisha jamii kuona umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo maeneo
ya kihistoria ambavyo yamesheheni chimbuko la tamaduni zetu pamoja na
harakati za binadamu katika kupambana na mazingira yake." alisema
Akizungumzia kuhusu lengo la ziara
hiyo, Bw.Mwenda amesema ziara hiyo ya siku moja imejikita kuhamasisha Utalii wa
ndani kwa kauli mbiu " Utalii wa ndani unaanza kwako na kwangu"
Aidha, Amesema Wizara ya Maliasili na
Utalii inaandaa utaratibu maalum wa kuwawezesha watumishi wengine wa Wizara
nyingine pamoja na taasisi za serikali waanze kutembelea vivutio vya utalii ili
kujenga utamaduni kwa watumishi wa Umma kutembelea vivutio vya utalii nchini
kwa ajili ya kujifunza na kufurahia maisha.
Awali, Mkuu wa Kituo cha Kolo, Zuberi
Mabie alieleza kuwa Kolo ni kivutio cha Utalii cha aina yake chenye michoro ya
miambani iliyochorwa na jamii ya Wasandawe miaka 10,000 hadi miaka 6,000
iliyopita.
Amesema eneo hilo ni miongoni mwa
maeneo manne ya Idara ya Mambokale yaliyopo katika orodha ya Urithi wa dunia
Alisema inaonesha kuwa kabla ya
ugunduzi huo watu walikuwa wanaweka kumbukumbu ya kuchora vitu na matukio
waliyokuwa wanayaona katika mazingira yao.
Akizungumzia kuhusu idadi ya watalii
wanaotembelea, alisema kila mwezi hupata watalii zaidi ya 200 kutoka ndani na
nje ya nchi.
Kwa upande wake, Afisa Utalii, Heda
Chale mara baada ya kutembelea kituo hicho alisema ameifurahia safari hiyo na
amejifunza vitu mbalimbali ikiwa pamoja na kujionea madhari ya aina yake katika
kivutio hicho.
Naye, Mhifadhi Mkuu wa Mambo Kale,
Wiliam Mwita alitoa wito kwa jamii kutembelea vituo vya maeneo ya
kihistoria yaliyotapakaa nchi nzima ili jamii iweze kujifunza historia ya
binadamu pamoja na mapambano yake katika kuyamudu mazingira.
Pia, Alitoa wito kwa Wawekezaji
kuchangamkia fursa ya kuwekeza kwenye vivutio vya Mambokale kwa vile nafasi
zipo wazi lengo likiwa ni kuviendeleza kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.
Amesema maeneo hayo yanahitaji uwekezaji
wa nguvu ili kuyafanya yawe na mvuto ili kuwavutia wageni kutika nje na pia
Watanzania
Kivutio cha Utalii Koli kipo kilomita
150 kutoka jiji la Dodoma na ni michoro ya kwanza kwa bara la Afrika kutokana
na uwingi wake na kutapakaa kwake katika eneo kubwa.









Comments
Post a Comment