- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa
Halotel, Mhina Semwenda (katikati), akiwaelekeza wakazi wa Kijiji cha Timbolo
namna ya kutumia huduma za mtandao wa Halotel wakati wa ziara ya waandishi wa
habari kutembelea miundombinu ya kampuni hiyo.
Wakazi wa kijiji cha Timbolo, Wilaya ya Arumeru mkoani
Arusha, wamepongeza jitihada za mtandao wa simu wa Halotel kwa kufikisha
mawasiliano kijijini hapo baada ya kuhangaika kwa muda mrefu kupata huduma za
Mawasiliano ya uhakika jambo ambalo limechangia kwa ukuaji wa shughuli za
kiuchumi kwa wakazi wa kijiji hicho hususani huduma jumuishi za fedha (financial
inclusion).
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa kijiji hicho, Bw. Samwel
Kivuyo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoka
vyombo mbalimbali walipokwenda kutembelea katika kijiji hicho ili kuona na
kujifunza shughuli mbalimbali za kimaendeleo ambazo zimechangiwa na mtandao huo
kuwekeza katika maeneo ambayo awali hayakuwa na huduma za mawasiliano ya uhakika.
"Halotel wamesaidia sana kufikisha huduma jumuishi za
kifedha kwa wananchi masikini wa kijiji hiki ambao awali walikuwa wanataabika
na kupitwa na huduma hizo hivyo kulazimika kutembea kilometa nyingi kufuata
huduma za kifedha, kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kijiji hicho, Samwel Kivuyo.
Baadhi ya wanakijiji wa kijiji hicho katika kata ya
Sambasha,wameelezea kufurahishwa na huduma ya Halopesa,ambapo wamesema,imekuwa
rafiki kulinganisha na huduma kama hizo zinazotolewa na kampuni
nyingine,kufutia Halotel kutotoza makato pindi mtumiaji wa huduma hiyo akituma
pesa kwenda mtandao huo.
“Kwa kweli ukiwa na huduma za Haloteli, unafurahia kupata
muda wa maongezi wa kutosha, data ndiyo siwezi kuelezea, yaani ni huduma rafiki
sana kwa sisi hasa wa huku kijijini ambao kipato chetu ni cha chini. Alisema, Rehema
Joshua, mkazi Kijiji cha Timbolo, Kata ya Sambasha, Wilaya ya Arumeru, Mkoa wa
Arusha.
“Sisi kama wananchi wa Timbolo tunashukuru kwanza kabisa
jitihada za serikali kwa kuiwezesha kampuni ya
Halotel kuweza kuweka minara ya
mawasiliano katika kijiji chetu ili wananchi waweze kupata huduma za
mawasiliano katika maeneo yao na kusaidia wananchi kutumia huduma za
mawasiliano katika kujiendeleza kiuchumi kwani hapo awali hatukuwa na huduma ya
mawasiliano ya uhakika.”
Mpaka sasa hali ya mawasiliano katika kijiji chetu ni nzuri,
watu wamepata ajira kufuatia kuanzisha biashara za huduma za kifedha kwa njia
ya simu pamoja na kuongeza uzalishaji wa mazao ya mboga mboga ambayo ni kazi
kuu ya wanakijiji wetu, kwani mara ya kwanza mawasiliano na wafanyabiashara
wengine yalikuwa ni magumu ila sasa tuna uhakika wa wateja kwa sababu
tunawasiliana nao moja kwa moja na hata upokeaji wa malipo umekuwa ni rahisi.
Alisema Kivuyo na kuongeza.
“Tunafurahi sana kuwa na mradi wa mawasiliano katika kijijj
chetu kwa sababu miundo mbinu ya
mawasiliano iliyojengwa na Halotel .Katika kijiji chetu imesaidia wananchi
kuimarisha usalama katika maeneo mbalimbali ya kijiji chetu kwani imekuwa
rahisi kupeana taarifa mbalimbali katika kijiji chetu. Alisema
Aidha Mwenyekiti huyo alibainisha kuwa hadi sasa changamoto
inayowakabili kijijini hapo ni Ukosefu wa umeme katika kijii hicho jambo ambalo
linatatiza shughuli za maendeleo kwa baadhi ya wananchi.
“Tunaomba Wakala wa umeme vijijini(REA) watusaidie kupata
umeme hasa katika kitongoji cha Meduti
na Murerian ili wananchi waweze kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo
na kijamii,ikiwemo kilimo, uchomeleaji
wa vyuma, shuleni, vituo vya afya ili
wananchi waweze kuboresha maisha yao na kujiongezea kipato katika kijiji hicho kilichoanzishwa
mwaka 1972 chenye wakazi 4638 na jumla
ya kivitongoji vinne ambavyo ni Oltingidi, Madukani, Meduti na
Muterian”,alisema mwenyekiti huyo.
Baada ya kuzungumza na mwenyekiti huyo wa kijiji cha
Timbolo,kuhusiana na kadhia hiyo ya umeme,waandishi walimtafuta mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry
Muro,kutaka kufahamu namna serikali
inavyoweza kuwasadia wananchi hao,ambao tayari wameshafanya jitihada za
kufungiwa mfumo wa umeme majumbani mwao.
“Kwakweli nawapongeza wananchi hao wa kijiji cha Timbolo,kwa
jitihada zao na serikali inafurahishwa mno na ana ya wanachi wanaopenda
kujiletea wenyewe maendeleo,na nimemtaka mwenyekiti wa kijji cha Timbolo,
Samwel Kivuyo,aje wakati wowote ofisni kwangu akiwa na wawakilishi watatu wa
wanakijiji waje tuzungumze na kumaliza mara moja kadhia hiyo ya umeme,” alisema
Mkuu wa Wiayaya Arumeru, Jerry Muro.
Wakati huo huo mkuu wa
Idara ya Mawasilianno,Kampuni ya Halotel Tanzania, Mhina Simwenda
alisema kuwa kampuni ya Halotel Tanzania ipo mkoani Arusha kwa ajili ya kuongea
na wateja,kusikiliza maoni kutoka kwao, kujua wanahitaji nini, kujua
changamoto walizonazo ili waweze kuboresha huduma zao kwa wateja.
“Ukiangalia kijiji cha Timbolo ndiyo chenye mafanikio mazuri
katika suala la mawasiliano na sisi kama Halotel Tanzania tunaishukuru serikali
ya kijiji cha Timbolo kwa kuunga mkono juhudi za kampuni yetu ili tuweze kuleta
huduma za mawasiliano hapa kijijini,” alisema, Semwenda.


Comments
Post a Comment