- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Japhet Hasunga ( wa pili kushoto)
akioneshwa mpaka kati ya Pori la Akiba la Burigi na eneo la wananchi
katika eneo la Nyungwe na Ofisa mwenye wadhifa wa Mkuu wa Hifadhi aliyeteuliwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kusimamia
Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi kuwa Hifadhi za Taifa, Damian Saru
(wa kwanza kulia) wakati Naibu Waziri huyo
alipotembelea jana mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua
ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika
mapori hayo, Watatu kushoto ni
Mkuu wa wilaya ya Biharamulo, Sada Malunde.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Japhet Hasunga ( wa pili kushoto)
akioneshwa mpaka kati ya Pori la Akiba la Burigi na eneo la wananchi
katika eneo la Nyungwe na Meneja wa
Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi kuwa Hifadhi za Taifa ,
Bigilamungu Kagoma ( wa kwanza kushoto)
wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea
jana mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu
mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa
na TANAPA katika mapori hayo, Watatu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya
Bihalamulo, Sada Malunde.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na baadhi ya Watumishi wa
Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi na kuwa Hifadhi za Taifa wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea jana kwenye mapori hayo katika
ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera
kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika mapori hayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe.Japhet Hasunga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya kamati
ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Bihalamulo pamoja na baadhji ya watumishi wa
TAWA na TANAPA wakati Naibu Waziri huyo
alipotembelea jana mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua
ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika
mapori hayo, Watatu kushoto ni
Mkuu wa wilaya ya Biharamulo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.
Japhet Hasunga (wa pili kushoto)
akioneshwa eneo la Ziwa Burigi katika eneo la Nkonje na Meneja
wa Mapori ya Akiba matano
yaliyopandishwa hadhi kuwa Hifadhi za Taifa, Bigilamungu Kagoma (wa kwanza kushoto) wakati Naibu Waziri
huyo alipotembelea jana mapori hayo
katika ziara yake ya siku tatu mkoani
Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA
katika mapori hayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Japhet Hasunga akisaini kitabu cha
wageni i katika eneo la Nyungwe wakati
Naibu Waziri huyo alipotembelea jana
mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu
mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa
na TANAPA katika mapori hayo, Watatu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya
Bihalamulo, Sada Malunde.
Baadhi ya mafuvu ya wanayamapori katika
Pori la A kiba la Burigi katika eneo la Nyungwe.
(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-WMU).
NA LUSUNGU HELELA-KAGERA
Bodi ya Wadhamini ya Hifadhi ya Taifa
Tanzania (TANAPA) imeidhinisha na kuruhusu matumizi ya bajeti ya mpito ya
kiasi cha shilingi 3.9 bilioni zitumike kwa ajili ya kuimarisha uhifadhi,
uendelezaji utalii pamoja na ujenzi wa miundombinu katika Mapori ya Akiba
matano yaliyopandishwa hadhi na kuwa Hifadhi za Taifa.
Hatua hiyo imekuja kufuatia tangazo
la Serikali la kuyapandisha hadhi Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi,
Kimisi, Ibanda na Rumanyika kuwa Hifadhi za Taifa kupitia kwa Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Hamisi Kigwangalla wakati alipokuwa
akihitimisha bajeti ya Wizara mwezi Mei mwaka huu Bungeni mjini
Dodoma.
Ofisa Mwenye Wadhifa wa Mkuu wa
Hifadhi, Damian Saru amesema hayo jana mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili
na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga wakati alipotembelea mapori ya
Biharamulo, Burigi na Kimisi ( BBK) ikiwa ni ziara yake ya kikazi ya
siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji
iliyofikiwa na TANAPA katika mapori hayo.
Alitaja fedha hizo kuwa zimeshaanza
kutumika katika kuimarisha ulinzi, kujenga miundo mbinu ya utalii na Utawala,
kuainisha mipaka , kusimamia mchakato wa kupandisha hadhi mapori
Damian Saru, Ofisa mwenye wadhifa wa
Mkuu wa Hifadhi aliyeteuliwa na TANAPA, aliwasilisha taarifa hiyo pamoja na
kumweleleza Naibu Waziri huyo hatua za utekelezaji zilizofikiwa katika mapori
hayo.
Alimweleza kuwa askari 58 wameshafika
kwenye mapori hayo matano kwa ajili ya kuongeza nguvu.
Mashine ya kutengeneza barabara 'Motor
Grader moja imeletwa kwa sjiki ya kutengeneza barabara.
Pia, Alimweleza Naibu Waziri huyo
ikiwemo vitendea kazi ikiwemo ndege moja magari manne, mahema silaha, GPS
vimeletwa katika mapori hayo kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi.
Kufuatia utekelezaji huo, Mkuu mwenye
hadhi ya Mkuu wa Hifadhi alitaja mafanikio yaliyopatikana katika kIpindi kifupi
cha utekelezaji maagizo hayo kuwa katika kipindi cha wiki mbili pamoja na
ng'ombe 41 kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.
Pia, alitaja idadi ya watuhumiwa 12 wa
ujangili wamekatwa.
Aidha, Saru alitaja aina za vifaa
vilivyokatwa kuwa ni mitumbwi mitatu, mkaa gunia mbili pamoja na baiskeli
zopatazo 10.
Kwa upande wake, Naibu Waziri ,
Mhe.Hasunga ameridhishwa na hatua ya TANAPA kwa ushirikiano na Mamlaka ya
Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa nzuri waliyoifanya.







Comments
Post a Comment