Featured Post

MICHORO YA KALE KOLO WILAYANI KUONDOKA HATARINI KUPOTEA



NA MWANDISHI WETU, KONDOA
MICHORO  ya kale iliyopo katika hifadhi ya Kolo wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma, ipo hatarini  kufutika kutokana na matumizi mabaya yanayotumika kwenye mila za matambiko yaliyopo katika mapango hayo.

Mkuu wa Kituo cha Michoro ya Miambani cha Kolo, Zuberi Mabie, alitoa kauli hiyo wakati  akizungumza na watumishi wa wizara ya Maliasili na Utalii walipotembelea kwenye  michoro hiyo ya watu wa kale iliyopo Kolo wilayani humo .
"Baadhi ya jamii wanaofanya matambiko hayo ya kimila kukosa elimu juu ya umuhimu wa michoro hiyo ya kale iliyopo kwenye hifadhi hiyo inayotambulika karibu duniani kote," alisema.
Akibainisha mkuu huyo wa kituo alitaja matumizi hayo ni pamoja na baadhi ya jamii wanaonde kutambika wamekuwa wakifanya uchafunzi wa mazingira kwakumwaga pombe za kienyeji kwenye kuta za michoro hiyo ya kale wanazo endanazo.
“Baadhi ya jamii wamekuwa walifanya matambiko na wamekuwa wakija na   pombe za kienyeji, na  matambiko yao wamekuwa wakimwanga pombe hizo kwenye michoro  na kusababisha kuacha alama za pombe, vitendo hivi vinaweza kusababisha michoro hiyo kufuatia," alisema Zuberi.
Vile vile alisema, ukataji miti hovyo katika Hifadhi ya Michoro hiyo, maji ya mvua, uchungaji wa mifugo, vumbi na jua, inasababisha uharibifu wa michoro  hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu Lusius Mwenda, aliwataka Watanzania kutumia hifadhi hiyo ya Kolo kwa manufaa ya kuiletea taifa uchumi kutokana na michoro ambayo imekuwa kivutia kwa ajili ya utalii wa ndani.
Mweda alisema michoro hiyo iliyopo ambayo inasadikiwa kuchorwa na jamii ya kabila la Wasandawe na Warangi, imekuwa kivutio ambacho kwa watu wengine wanaweza kujifunza na kufahamu historia ya babu zetu hao wa kale.
Hata hivyo, alisema kuwa kutokana na kuimarika kwa barabara ya kutoka Dodoma hadi Babati hifadhi hiyo imekuwa na ongezeko la watu wanaotembelea kutoka 200 waliokuwa wakifika kwa kipindi mwezi mmoja huko nyuma hadi kufikai 400 kwa hivi sasa.

Comments