- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
MADIWANI
wa halmashauri ya Manispaa ya Tabora wamepewa muda wa siku 14 kurejesha
viwanja vyote walivyojimilikisha kiyume na utaratibu.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa wilaya ya Tabora Komanya Eric Kitwala alipokuwa akizungumza na Madiwani, Wakuu wa Idara na Vitengo na Watendaji wa halamashauri ya manispaa hiyo.
Alisema
manispaa hiyo inakabiliwa na migogoro mingi ya ardhi isiyoisha ambayo
kwa kiasi kikubwa imesababishwa na baadhi ya watumishi na madiwani wa
halmashauri hiyo kujimilikisha viwanja vingi kinyemela na kinyume na
utaratibu.
Alisema
kitendo cha diwani au mtumishi yeyote aliyepewa dhamana ya kusimamia
maendeleo ya wananchi kutumia wadhifa wake kwa maslahi binafsi ni kwenda
kinyume na maadili ya utumishi.
‘Natoa
siku 14 kwa madiwani wote waliojimilikisha viwanja kinyume na utaratibu
katika maeneo mbalimbali ya manispaa hii kujisalimisha, la sivyo sheria
itachukua mkondo wake’, alisema.
Kitwala
alisisitiza kuwa amedhamiria kumalizia migogoro yote inayohusiana na
mambo ya ardhi katika wilaya yake na kwa kuanzia ametenga siku ya Ijumaa
ya kila wiki kuwa siku maalumu ya kusikiliza malalamiko ya wananchi na
kuyatafutia ufumbuzi.
Aliwataka
wananchi wote wenye malalamiko ya viwanja kufika ofisini kwake wakiwa
na vielelezo husika ili aweze kumaliza mgogoro huo, aliagiza wataalamu
wa idara husika kufika ofisini kwake siku ya kusikiliza malalamiko ya
wananchi ili haki itendeke.
Aidha
aliagiza Wakuu wa Idara na Watendaji wote kutokaa Ofisini bali waende
vijijini kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na kusikiliza kero
za wananchi kwa kuwa kila siku amekuwa akipokea meseji za malalamiko ya
wananchi.
Diwani
wa Kata ya Ndevelwa (CCM) Seleman Juma Maganga ambaye ndiye Msemaji wa
madiwani wote wa CCM alimshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kuwaletea
DC mwenye maono makubwa ya maendeleo.
Aliwataka
wataalamu wa manispaa hiyo kuwajibika ipasavyo na kujiepusha na uzembe
wa aina yoyote ile ili kwenda na kasi ya Mkuu wao mpya wa wilaya
vinginevyo atawawajibisha.
Comments
Post a Comment