- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mwandishi Wetu, Shinyanga
ZAIDI ya 500 wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga akiwemo katibu mwenezi wa kata hiyo
wamehamia Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kile walichodai wananyimwa uhuru na
viongozi wa Chama hicho ngazi ya juu.
Wanachama hao ambao walikuwa wamesimika mizizi katika kata
hiyo na kuisababishia kata hiyo kuchukua nafasi zote kuanzia ngazi ya kijiji
hadi kata wametambulishwa jana kwenye mkutano wa hadhara kilichofanyika kata na
kusema kuwa walipokuwa kwenye chama hicho walinyimwa uhuru na kupewa masimango .
Wamesema baada ya kukisababishia ushindi chama hicho ngazi
zote wamedharauliwa na kugeuzwa kuwa madaraja na kupewa masimango na viongozi
wa ngazi za juu hali ambayo wamedai wameshindwa kuvumilia wameamua kurudi CCM
kwenye Chama cha wakarimu.
Akizungumza kwenye kikao hicho aliyekuwa muenezi wa kata
Chadema Jastin Mwasiga alisema ameamua kuhama chama kwa sababu chama chake
kimemnyima uhuru, kina masimango na
unyanyasaji mkubwa hivyo ameona ahamie chama cha CCM cha watu wakarimu.
"Kwa kweli mimi binafsi nimeamua kuhamia CCM kwa sababu
chadema tumegeuka madaraja ya kuvukia hatuthaminiwi na huku ndiyo tulisaidia
viongozi wote kuanzia kwa mwenyekiti wa serikali za mitaa mpaka kwa diwani,
tukapata ushindi mkubwa"alisema Mwasiga.
"Kwa kweli mimi nilisaidia sana kupata ushindi chadema
lakini viongozi hawakulitambua hilo
nimenyanyasika sana na nimevumilia sana na sasa nimechoka nimeona nirudi CCM tushirikiane kupata ushindi naamini
awamu hii Masekelo itachukua nafasi zote kwa sababu najua mbinu za ushindi tutashirikiana
kwa pamoja kuanzia leo uenezi wangu wa chadema umekoma"aliongeza.
Hamza Hamis ambaye alikuwa mwanachama wa Chadema amesema
ameamua kurudi CCM kwa kuwa chama hicho kilikua cha wazazi wake, kwani ameona
kinafaa tofauti na chadema alikokimbilia bila kujua kama kuna matatizo au kuna
unyanyasaji wa kuburuzwa.
Kwa upande wake katibu muenezi wa kata hiyo Mashimba Kadama
aliwataka wanachama wa CCM wasikae wakajisahau kwa kujua kwamba chadema
imeisha, lengo la kila mwanachama
alete wanachama wajiunge na CCM na
kuirudisha kata iliyochukuliwa na wapinzani.
"Wanachama wenzangu tusikae tukajisahau kwa kusema
chadema imeisha tunatakiwa kuhakikisha wameisha kabisa hata mmoja, kwa mfano
unaweza ukauwa nyoka lakini bila kumsigina kwenye kichwa atakuwa hajafa hivyo
tunatakiwa kuwasigina kabisa hadi kichwa tuhakikishe hapa masekelo hawapo
wapinzani"alisema Kadama.
Naye katibu wa CCM kata Petro Kolimba alisema wamefurahi kwa
kujiunga kwa hao wanachama kwa nyakati tofauti kwa sababu wamegundua nyubani
kuna ukarimu wanakaribishwa na sasa waliorudi CCM kutoka vyama vya upinzani
ndani ya miezi sita ni zaidi ya 500 awali walikuwa wanachama 950.

Comments
Post a Comment