- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NA ALOYCE NDELEIO
Yeyote yule
aliyesoma somo la Fizikia lazima akubali kuwaalikutana na majina ya
wanasayansi wa mwanzo kabisa na ambao wameuweka uhai wa somo hilo katika
duniani hii na miongoni mwa wanasayansi hao ni Isaac Newton.
Newton katika
maisha yake alivumbua kanuni mwendo tatu lakini ambayo imekuwa ikiegemea
au kupenyeza katika nyanja nyingine ambayo ni kanuni mwendo ya tatu.
Kwa lugha ya
Kiingereza inasema, “Action and reaction
are equal and opposite in direction” au “ For every action, there is an
equal and opposite reaction” ambayo kwa tafsiri isiyo rasmi ni 'Kila tendo
na mjibizo wake huwa na nguvu sawa na mwelekeo tofauti'.
Kinachozungumzwa
hapo ni mwendo na nyanja inayohusiana na shughuli za kisayansi na hususan
kwenye nyanja ya Fizikia lakini mwendo huo pia unaweza kuingiza kwenye maisha
ya kila siku ya mienendo mingine ya maisha ya jamii kiuchumi kisiasa na
kijamii.
Katika uwanja wa
siasa kumekuwepo shughuli au mienendo mingi na hususan tangu kuingia kwa mfumo
wa siasa za vyama vingi hapa nchini na hadi sasa ni zaidi ya miaka 17 chaguzi
zilipoanza kuhusisha vyama vingi vya siasa.
Ukiondoa uchaguzi
wa kwanza uliofanyika mwaka 1995 uchaguzi wa mwaka 2010 unaweza kuelezwa
kuwa ulikuwa na ukinzani mkubwa ikilinganishwa na chaguzi nyingine za mwaka
2000 na 2005.
Kimsingi hapa ni
kuibuka kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambacho kilizoa majimbo
mengi na hata kuwaangusha baadhi ya wakongwe waliogombea kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
Lakini jambo
jingine lililojidhihirisha ndani ya chama hicho ni kutoa fursa kwa vijana ambao
waligombea kwenye majimbo na kupata ushindi wa kishindo ndani ya majimbo hayo.
Chadema baada ya
uchaguzi kimepata fursa ya kuunda Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni ambapo
kiongozi wake ni mwenyekiti wa chama hicho na Mbunge wa Jimbo la Hai,
Freeman Mbowe.
Katika mazingira
hayo ni kwamba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linajumuisha kambi
mbili za chama tawala na kambi ya upinzani.
Hivyo kila kambi
inawajibika kuhakikisha kuwa kile inachokisema kina manufaa kwa jamii kwa
sababu pande zote zinawakilisha wananchi ambao ni walipa kodi.
Kila upade umekuwa
ukiwakilisha hoja zake au matakwa yake yanayolenga kuleta maendeleo kwa
wananchi katika kile kinachofahamika kama ilani za vyama.
Hakuna hoja ambazo
zimekuwa zikiwakilishwa zikiwa kinyuime na mahitaji ya jamii ila katika
utekelezaji chama kilicho madarakani ndicho kimekuwa na jukumu la kushika
usukani.
Hata hivyo
umekuwepo udhanifu kuwa hoja au maoni yanayotolew ana kambi ya upinzai yamekuwa
hayatekelezwi na kwamba kinachotekelezwa ni hoja za upande mmoja wa chama
tawala tu.
Udhanifu huo si
sahihi kwani kila jambo ambalo limekuwa likifanyika halijatoka upande mmoja tu
bali ni kutoka pande zote.
Rejea zinaweza
kuwa katika kampeni za uchaguzi ambapo suala la elimu bure lilikuwa limeelezwa
na na vyama vyote na hata hivyo limetekelezwa na serikali iliyopo madarakani.
Jingine ni kufufua
baadhi ya taasisi zilizokuwa zimedhoofu au kufa ili ziweze kutumika kwa manufaa
ya umma wote. Mfano ni kulifufua Shirika l ndege Tanzania ATCL ambalo
limepewa kipaumbele na uongozi wa Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe
Magufuli ikiwa ni pamoja na kununua ndege za bombardier na ndege kubwa ya
Dreamliner 787.
Yapo mambo mengi
zikiwepo huduma za jamii kuanzia maji, sekta za kilimo, mifugo,
maliasili, miundombinu, uvuvi na madini.
Hata hivyo katika
eneo ambalo limekuwa likipigiwa kelele ni suala la kodi nalo ndilo lililopewa
kipaumbele kikubwa na hata kuongeza chachu katikauwajibikaji jambo
ambalo limeonesha kuwepo kwa ufanisi.
Lakini jambo moja
ambalo limekuwa likipiga kelele zaidi ni kutowajibika kwa baadhi ya watendaji
wa serikali ambako kulikuwa kunaisababishia serikali hasara.
Katika eneo hilo
kumekuwepo kuwajibishwa kwa viongozi ambako kumejipatia msamiati wa utumbuaji
wa majibu.
Lakini bila
kuegemea upande wowote kinachojidhihirisha ni kwamba mlengwa katika
hoja zinazotolewa na pande zote ni mwananchi bila kuangalia masuala ya itikadi.
Hata kama ilani
inayotekelezwa ni ya chama kilichopo madarakani na hata kama inadaiwa kuwa
chama kilichopo madarakani kinatekeleza moja ya ilani iliyokuwa ya chama
kingine hiyo haiwezi kuwa ni hoja.
Hoja ni kwamba
kinachotekelezwa kinakidhi maslahi ya umma wote bila kujali chimbuko la ilani
ni sehemu gani.
Hali hiyo
inayoweza kuwa ni udhanifu imekuwa haiangalii kwamba mambo yanafanyika kwa
kuzingatia fikra za watu pamoja na tathmini za kujenga kwa maslahi mapana.
Kama jambo
linakidhi matakwa ya umma na limetoka upande usio na mamlaka ya
kiutendaji na kwamba mamlaka hiyo imelitohoa, na kuliingiza katika
utekelezaji kwa kuwa ni jema inasadifu kuwa kuna kutegemea katika kauli
zenye manufaa kwa umma.
Hapo ndipo kauli
mwendo ya Newton inaingia kwamba pande zote zina mchango katika kushughulikia
maslahi ya umma licha ya kwamba zipo tofauti za kiitikadi au mwelekeo baina
yake.
Kinachofanya hali
hiyo isionekane mara nyingi ni mtazamo unaofanyika katika misingi ya propaganda
unaokuwa umeegemea upande mmoja. Hilo ni sawa kwani kwa mtazamo huo ni
miongoni mwa mikakati inayolenga kujiimarisha.
Lakini ufanisi
unapochukuliwa kwa mtazamo wa kanuni mwendo ya Newton, haiyumkini taswira
itakayojengeka ni kwamba, pande zote ni washirika katika utekelezaji wa
mahitaji kama si matakwa ya jamii.
Pamoja na hali
yote hiyo ni wazi kuwa utekelezaji wa ilani hakuna hata moja ambayo inaweza
kuelezwa kuwa ni kikwazo katika mikakati yote ya maendeleo.
Kama kuna fikra za
aina hiyo inasadifu kusema ni fikra mfu.
Hali hiyo
inamaanisha kuwa kanuni mwendo ya Newton katika mwenendo mzima wa ulingo wa
siasa ni wazi 'Kila tendo na mwitiko wake huwa na nguvu sawa lakini mwelekeo
huwa ni tofauti’
CHANZO: TANZANITE



Comments
Post a Comment