- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Askari wa (KWS) Edwin Koech, akiwa na
mbwa Ram wakati wa mafunzo
Ugunduzi mpya ambao umetajwa kuwa utawapa mbwa uwezo zaidi
wa kuwanasa walanguzi utaanza kutumiwa hivi karibuni.
Mfumo huo utawawezesha mbwa kunusa pembe za ndovu na bidhaa
zingine haramu za wanyama pori zilizofichwa kwenye kontena kubwa kwa kutumia
hewa maalum.
Mfumo huo unafanyiwa majaribio kwenye bandari ya Mombasa,
ambayo inatajwa kuwa kubwa zaidi kwa kupitishia pembe za ndovu barani Afrika.
Kulingana na ripoti moja, zaidi ya kilo 18,000 za pembe
zilishikwa bandarini humo kati ya mwaka 2009 na 2014.
Mbwa wakipewa mafunzo
Kuzalisha kiwango kama hicho, ripoti hiyo inasema kuwa zaidi
ya ndovu 2,400 huenda waliuawa na ndicho kiwango tu kilichopatikana.
Mfumo huu utakuwa wenye manufaa makubwa katika kupunguza
bidhaa za wanyama pori walio katika hatari ya kuangamia zinazopitia bandarini
humo kwenda nchi za ng'ambo.
Uwezo mkubwa wa mbwa wa kunusa unamaanisha kuwa wanaweza
kunusa hata kiwango kidogo cha pembe kwenye kontena kubwa ya futi 40.
Magenge ya ulanguzi yanazidi kutumia mbinu ngumu kuficha na
kusafirisha bidhaa haramu za wanyama pori.
Ram. mbwa wa kunusa wa shirika la
wanyamapori nchini Kenya wakati wa mafunzo mjini Mombasa
Licha ya kuchukua muda mrefu mfumo huu umefanikisha katika
upatikanaji mara 26 ndani ya miezi 6 na kuzipa mamlaka habari muhimu kuhusu
mitandao ya wahalifu ambayo hupata mamilioni ya pesa kila mwaka kutokana na
biashara haramu.
Mfuko wa wanyama pori duniani WWF unakadiria kuwa ni faru
weusi 25,000 waliosalia, na zaid ya 1000 waliuawa na wawindaji haramu nchini
Afrika Kusini pekee mwaka huu.
Wakati huo huo makundi wa kulinda wanyama yanakadiria kuwa
ndovu 55 wanauawa kila siku kutokana na pembe zao.



Comments
Post a Comment