- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NA MWANDISHI WETU, DODOMA
HALMASHAURI ya Rungwe,
mkoani Mbeya, imeagizwa kurejesha sh. milioni 438.6 ambazo walitumia kinyume na
utaratibu kwa kujenga maabara ya shule za sekondari.
Maagizo hayo
yalitolewa jijini Dodoma jana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za
Serikali za Mitaa (LAAC), Abdallah Chikota.
Alitoa agizo hilo baada
ya kamati yake kufanya mahojiano na halmashauri hiyo kuhusu hoja za ukaguzi za
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha
2016/17.
Chikota ambaye pia ni
Mbunge wa Nanyamba (CCM), alisema fedha hizo zilikuwa kwa ajili ya kulipa
wakandarasi waliokuwa wakitekeleza miradi mbalimbali.
“Fedha hizi sehemu
kubwa ni za wakandarasi, huko waliko wanalalamika na kuipaka matope Serikali
kwamba hailipi madeni wakati hii halmashauri imezitumia kwa matumizi mengine,” alisema
Chikota.
Kutokana na hali hiyo,
aliagiza fedha hizo zirejeshwe ili wakandarasi walipwe ili kupunguza
manung’uniko huku akitaka malipo yanapofanyika vielelezo viwasilishwe ofisi ya
CAG kwa ajili ya uhakiki.
Alieleza kuwa, kwa kuwa
fedha hizo zimetumika kinyume na utaratibu, deni hilo lilipwe ndani ya mwaka
huu wa fedha 2018/19 hususani ifikapo Juni, 2019.
Chikota alisema
Kamati hiyo imebaini kuna ucheleweshaji wa utekelezaji miradi ya maji ikiwemo
mradi wa masoko ambao kamati ilipotembelea iliona kuna kusuasua.
Alimwagiza Katibu
Tawala wa Mkoa (RAS) kuunda timu maalumu ya ufuatiliaji miradi ya maji katika halmashauri
ya hiyo na kwamba baada ya kamati kufuatilia na kubaini kuna kulegalega
itaandaa taarifa, itawasilishwa ofisi ya CAG kabla ya Desemba 30, mwaka huu.
“Halmashauri hii kwa
miaka mitatu iliyopita ina deni kubwa la fedha za Mfuko wa Wanawake na Vijana,
inadaiwa zaidi ya sh. milioni 576.9, pia inadaiwa sh. milioni 43 za fedha ambazo
ni asilimia 20 ya mapato ya ndani yanayorejeshwa kwa vijiji,” alisema na
kuongeza.
“Tunataka mtuandikie
barua ambayo itaonesha mkakati wa kulipa deni hili hadi litakapoisha, akati wa
kutoa mikopo hii ifuate muongozo uliowekwa kwa vikundi vya wanawake na vijana,”
alisisitiza.
Akizungumzia kitengo
cha ukaguzi, Chikota alisema kamati imeagiza kuwezeshwa kwa kitengo cha ukaguzi
cha halmashauri hiyo ili kitimize majukumu yake ipasavyo.
Aliongeza kuna,
changamoto ya uwepo wa uhakika wa vyanzo vya mapato vinatoa kiasi gani na mara
nyingi Serikali imekuwa ikiagiza yafanyike makadirio kwa kila chanzo cha
mapato.
“Kamati inaagiza
Halmashauri ya Rungwe kwa kushirikiana na Ofisi ya RAS ifanye tathmini ya
vyanzo vya mapato ili bajeti ijayo yawekwe makisio ambayo yanakaribiana na
uhalisia,” alisema.
Awali akijibu hoja za
wajumbe wa kamati hiyo, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Loema Peter alikiri
kuwa walikopa fedha hizo, kuzitumia kujengea maabara tatu kwa shule zote za
sekondari wilayani humo.
Alisema wameanza
kulipa fedha hizo ambapo mwaka uliopita walipeleka Wakala wa Barabara Mijini na
Vijijini (TARURA) sh. milioni 50 kwa ajili ya kulipa wakandarasi.
KYELA
YARUDISHWA
Wakati huo huo, Kamati
hiyo imeshindwa kufanya mahojiano na Halmashauri ya Wilaya ya Kyela kutokana na
vitabu vyao kuwa na dosari mbalimbali ikiwemo katika fedha za elimu bure ambapo
mchanganuo wa matumizi ya fedha hizo hazipo vizuri.
“Ukiangalia
mchanganuo wa matumizi waliouleta kwa matumizi ya sekondari wanasema wametumia
sh. milioni 792.4 kwa mwaka huo lakini ukiangalia kwenye kitabu chao wameonesha
matumizi ya sh. milioni 163.4, sasa sh. milioni 510 hazijaoneshwa zimetumika
kwa shughuli zipi,”alisema Chikota.

Comments
Post a Comment