- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mnangagwa aapishwa kuwa Rais wa Zimbabwe
Emmerson Mnangagwa
ameapishwa kuwa Rais wa Zimbabwe siku moja baada ya mshindani wake mkuu
Nelson Chamisa kutangaza kukataa matokeo ya uchaguzi.
Mapema Jumapili waangalizi wa uchaguzi kutoka Marekani walisema nchi hiyo imekosa utamaduni wa uvumilivu wa demokrasia.Siku ya Ijumaa mahakama ya kikatiba ilikataa madai ya upinzani kuwa udanganyifu ulifanyika ikisema kuwa hakukuwa na ushahidi.
Uchaguzi huo wa mwezi Julai ulikuwa wa kwanza tangu kiongozi wa miaka mingi Robert Mugabe aondolewa madarakani mwaka uliopita.
Mnangagwa aapishwa kuwa Rais wa Zimbabwe
Siku mbili baada ya uchaguzi huo watu 6 waliuawa
kwenye ghasia kati ya jeshi na wafuasi wa muungano wa upinzani MDC,
unaodai kuwa kiongozi wa upinzani Nelson Chamisa alikuwa ameibiwa
ushindi wake.Saa kadhaa kabla ya Mnanganwa kuapishwa taasisi ya kiamataifa ya Marekani inayohusika na masuala ya Demokrasia ilisema mfumo wa Zimababwe haukuruhusu vyama vya kisiasa kutendewa kwa njia iliyo sawa na watu hawakuruhusiwa kupiga kura kwa njia huru.
Nelson Chamisa amekataa matokeo



Comments
Post a Comment