Mradi wa reli mpya ya kisasa nchini
Kenya SGR umesababisha hasara ya $100m (£76m) katika kipindi cha mwaka
wa kwanza wa operesheni zake , kulingana na wizara ya uchukuzi nchini
humo. Mradi huo uliofadhiliwa na serikali ya China ambao
unaunganisha mji wa pwani wa Mombasa na Nairobi ulifadhiliwa kwa mkopo
wa kima cha $3bn kutoka kwa benki ya China ya Exim katika kipindi cha
miaka 15. Serikali ya Kenya ilipinga madai kwamba bei ya ujenzi wa mradi huo wa reli iliongezwa, haiwezi kudumishwa na haifai kiuchumi. Reli
hiyo ya SGR ni miongoni mwa miradi muhimu ilioahidiwa na rais Uhuru
Kenyatta katika uchaguzi wake, ukizinduliwa mwezi mmoja kabla ya
uchaguzi wa urais uliopita.
Huku treni za abiria zikijaa mara kwa
mara, waziri wa uchukuzi James Macharia aliambia kamati ya bunge kwamba
ilikuwa vigumu kuwarai wenye mizigo kusafirisha mizigo hiyo kupitia reli
kutoka kwa barabara. Mipango
ya kuanza kulipa deni hilo inatarajiwa kuanza mwaka ujao, na iwapo reli
hiyo itashindwa kujilipia deni hilo basi huenda walipa kodi wa Kenya
wakalazimika kulipa deni hilo. Wanauchumi wanakadiria kwamba China sasa inamiliki asilimia 70 ya deni la Kenya. Hatahivyo serikali inatumai kwamba reli hiyo itaanza kupata faida katika kipindi kijacho cha fedha.
Tanzania yaanza kujenga reli ya kisasa
Nchini
Tanzania Rais wa Tanzania John Magufuli aliweka jiwe la msingi la
ujenzi wa awamu ya kwanza ya mradi mkubwa wa reli ya kisasa ya Standard
Gauge ambayo hapo baadae itaunganisha nchi za Rwanda na Burundi pia. Lakini
katika awamu hii ya kwanza, ujenzi utakuwa wa reli yenye urefu wa
kilomita takribani 300, ambayo itatoka jijini Dar es Salaam na kuishia
mkoa wa jirani wa Morogoro. Ni reli ya kisasa, na ya kwanza
Afrika Mashariki na kati itakayokuwa na uwezo wa kupitisha treni
zitakazoendeshwa kwa nguvu ya umeme. Reli hiyo itajengwa kwa awamu
ya kwanza na kampuni kutoka nchi mbili, uturuki na Ureno kwa gharama
ya takriban dola bilioni 1.2 za Kimarekani. Reli hiyo itakuwa na
uwezo wa kubeba treni yenye kuvuta mabehewa 100 na kubeba mzigo wa mpaka
tani 10000 kwa mkupuo sawa na uwezo wa Malori 500 ya mizigo. Mradi huu utaleta ahueni kwa wasafiri wa Dar es Salaam mpaka
Morogoro ambpo wataweza kusafiri kwa mwendo kasi kwa saa 2 na dakika 50
pekee Rais wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli katika sherehe
hizo amesema kuwa Tanzania itanufaika kutokana na Mradi huu kwa
maendeleo ya uchumi, Hivi sasa Serikali ya Tanzania inaelekeza
jitihada zake za ujenzi wa reli wa awamu ya pili yenye urefu wa
kilometa 336 kutoka Morogoro mpaka Dodoma yalipo makao makuu ya nchi na
tayari serikali ya Uturuki imeonyesha nia ya kushirikiana na Tanzania
kujenga sehemu hiyo.
Comments
Post a Comment