NAIBU
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akizungumza na Mhandisi
wa Maji Korogwe Mji Joseph Mcharo kabla ya kumsimamisha kazi kulia ni
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe Godwin Gondwe.
NAIBU
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto akizungumza na
watendaji wa Halmshauri ya Korogwe Mji wakati wa ziara yake
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akimsikiliza kwa
umakini Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe Godwin Gondwe wakati wa ziara
yake.
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amemsimamisha
Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Wilaya Korogwe Mji Joseph Mcharo kwa
kutumia force accout kwenye mradi wa zaidi ya Milioni 700 bila ya kibali
toka Wizara hiyo.
Agizo la kusimamishwa kwa Mhandisi huyo
alilitoa jana wakati akikagua mradi miwili ya maji ya Mtonga ambao
umetumia zaidi ya milioni 700 na msambiazi ambao umetumia zaidi ya
milioni 600 ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya mkoa wa Tanga ambayo
ilianza juzi wilayani Handeni.
Alisema mradi huo ulitakiwa
kutumia kiasi cha shilingi Milioni 500 na wataalamu hao wakaubadilisha
na kuufanya uwe wa milioni 700 ingawa bado unaendelea kusuasua jambo
ambalo linaonyesha ubadhirifu wa fedha za Serikali
Akiwa kwenye
mradi wa Mtonga baada ya kumalizika kuukagua alitilia mashaka na ndipo
alipoamuru mhandisi huyo kumpatia maelezo ya kina kuhusiana na mradi huo
lakini pia hakuridhika na maelezo hayo na kuagiza kuwa atapeleka
wataalamu kutoka wizara ili kuweza kuhakiki thamani ya fedha na ubora
mrai huo.
“Kwa kweli mimi hapa sijaridhika na utekelezaji wa
mradi huu unaonekana upo chini ya kiwango na ucheleweshwaji huku
wananchi wakiendelea kupata tabu hivyo nitatuma wataalamu kutoka
wizarani waje kuhakiki mradi huo”Alisema
Baada ya ukaguzi wa
mradi huo Naibu Waziri huyo aliambatana na viongozi mbalimbali wa
halmashauri ya Korogwe mji kuelekea kwenye mradi wa Msambiazi ambako
kunajengwa tenki kubwa la mradi utakaosambaza maji kwa wananchi.
Akiwa
huku ndipo alipomuuliza mhandisi gharama za mradi ambapo alisema zaidi
ya milioni 600 zimetumika kwa kutumia mfumo wa mkandarasi na kupelekea
mradi huo kufikia kwenye hatua za mwisho jambo ambalo limeibua maswali
mengi kwa Naibu Waziri na kuamua kuchukua uamuzi huo.
“Ndugu
zangu haiwezekani mradi wa zaidi ya milioni 700 kutumia force account
kinyume na taratibu za wizara huku mradi wa milioni 600 ukitekelezwa
kupitia mkandarasi ni wazi kwamba kuna ubadhirifu unaendelea hapa na
mimi sitakubali”Alisema.
Baada ya maelezo hayo Naibu Waziri
aliamua kumsimamisha mkandarasi huyo kwa kigezo miradi inayotumia chini
ya milioni 200 ndio inapaswa kutumia force acounti tofauti na
alivyofanya mhandisi huyo huku akimdanganya kwamba anakibali kutoka
wizarani.
Awali akijib u hoja za Naibu Waziri huyo Mhandisi wa
Maji Halmashauri ya Korogwe Mji Joseph Mcharo alidai anakibali cha
wizara kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa mtonga kutumia force acounti
ndipo Naibu Waziri huyo alipoamua kupiga simu wizara kupata
ufafanuzi.
Naye
kwa upande wake Mkurugenzi wa Halamshauri ya Korogwe Mji Jumanne Shauri
alionekana kushindwa kujibu maswali ya Naibu Waziri jambo ambalo
liliibuka mabishoni baina yao kabla ya Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe
Godwin Gondwe kumtaka Mkurugenzi akiri mapungufu yaliyojitokeza kwenye
mradi huo.
Mradi wa Mtonga ambao Naibu Waziri Aweso aliitulia
mashaka ni wa kusambaza tenki,mabomba na sehemu maalumu kwa ajili ya
mtambo wa kutibia na kusafisha maji eneo la mradi husika
Comments
Post a Comment