- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Na
MWANDISHI WETU
RAIA
19 wa China na Watanzania sita, wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka ya uhujumu uchumi.
Washtakiwa
hao wanashtakiwa chini ya vifungu vya Sheria ya Uhamiaji, chini ya Sheria ya Watu
wasio raia wa Tanzania na Uhujumu Uchumi.
Mbele
ya Hakimu Mkazi, Huruma Shaidi, washtakiwa hao walitajwa kuwa ni Bo Song, Liu
Yunley, Chen Chao Hui, Fu Zeng, Wu Hai Quing, Ke Qiu Fang na Frederick
Kumalija.
Wengine
Jing Jing Lin, Ku Liao, Yan Yan Geng, Chen Ying Gong, Salim Mahsein Al-Amry,
George Elikana, Fatuma Songoro, Bhoke Mwita, Kelvin Ponela, Chen Gwandi, Lin
Ben, Rui Guo, Lin Xiangqui, Chen Fa, Wan Li, Robert Mkini na Revocatus Mugisha.
Akisoma
hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali,
Patrick Mwita, akisaidiana na Shedrack Kimaro alidai kuwa, kati ya Juni Mosi, 2017
na Mei 18, 2018 walitenda kosa la kwanza, ambapo wanadaiwa siku hiyo, chini ya Sheria
ya Watu ambao siyo raia wa Tanzania, walitoa taarifa za uongo kwa lengo la
kupata kibali cha kufanya kazi nchini.
Katika
shtaka la pili imedaiwa kuwa, siku na mahali hapo hapo, washtakiwa wote kwa
makusudi, huku wakijua kuwa ni kosa, walitoa taarifa za uongo kwa Kamishna wa Kazi
kwa lengo la kupata vibali vya kufanyia kazi.
Iliendelea
kudaiwa kuwa, katika shtaka la tatu, mshtakiwa Bo Song alijihusisha na kazi
nchini bila ya kuwa na Paso ya kuishi nchini.
Katika
shtaka la nne, washtakiwa Kumalija, Mwita, Songoro, Ponela, Mkini na Mugusha
wanadaiwa kuwa kati ya Juni Mosi, 2017 na Mei 17, 2018 ndani ya Jiji la Dar es
Salaam, walimsaidia raia wa China, Bo Song kujihusisha na kazi katika Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania huku wakijua kuwa hana kibali cha kuishi nchini wala
kufanya kazi.
Katika
shtaka la tano, washtakiwa wote wanadaiwa kuandaa, kusimamia na kusaidia kutoa
taarifa za uongo kwa dhumuni la kujipatia kibali cha kufanya kazi na kuishi
nchini.
Katika
shtaka la mwisho, washtakiwa wote kinyume na sheria ya uhujumu uchumi,
walijihusisha na makosa ya udanganyifu kwa kuonyesha kwamba walikuwa na vibali
vya kuishi nchini Tanzania kutoka Idara ya Uhamiaji na vibali vya kufanya kazi
kutoka kwa Kamishna wa Kazi nchini huku wakijua kuwa siyo kweli.
Hata
hivyo, washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa
Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.
Aidha,
Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) aliwasilisha hati ya kuzuia dhamana dhidi
ya washtakiwa kwa ajili ya maslahi ya nchi na washtakiwa.
Wakili
wa utetezi, Peter Kibatala, alipinga hati hiyo na kudai hati hiyo ya DPP
haizuii mahakama kuangalia na kutoa uamuzi.
Aidha,
amedai kuwa, hati hiyo haionyeshi ni jinsi gani maslahi ya nchi wala watuhumiwa
yatakavyoathiriwa.
Wakili
wa Serikali, Mwita alipinga hoja hizo na kudai, kwa mujibu wa sheria ya kesi za
uhujumu uchumi, DPP akiweka hati, mahakama haina mamlaka ya kuhoji kibali hicho.
Baada
ya mabishano ya kisheria, Hakimu Shaidi, alisema atatoa uamuzi dhidi ya
washtakiwa kama wapate dhamana ama la Juni 14, 2018.

Comments
Post a Comment