- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
MASAUNI AFANYA ZIARA MKOANI GEITA, AKAGUA UJENZI WA KITUO KIPYA CHA POLISI, GEREZA NA UJENZI WA NYUMBA 100 ZA ASKARI
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati),
akionyeshwa na Mkuu wa Gereza Chato, Joseph Busumabu, maeneo mbalimbali
ya Gereza hilo ambalo tayari linahifadhi wafungwa na mahabusu na pia
linaendelea kupanuliwa kwa kujengwa majengo mapya zaidi. Kushoto ni Mkuu
wa Wilaya ya Geita, Shabaan Ntarambe. Masauni alifanya ziara katika
Mkoa wa Geita kwa kukagua ujenzi wa Kituo cha Polisi Chato, ujenzi wa
Gereza Chato na baadaye kukagua ujenzi wa nyumba 100 za askari polisi
ambazo zimeanza kujengwa mjini Geita. Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulamboakimuonyesha Naibu Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), Kituo kipya
cha Polisi mjini Chato ambacho kipo katika hatua ya mwisho kukamilika. .
Masauni alifanya ziara katika Mkoa wa Geita kwa kukagua ujenzi wa Kituo
cha Polisi Chato, ujenzi wa Gereza Chato na baadaye kukagua ujenzi wa
nyumba 100 za askari polisi ambazo zimeanza kujengwa mjini Geita.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akitoka
kukagua ujenzi wa Gereza Chato, mkoani Geita, ambalo licha ya kua tayari
Gereza hilo jipya limenza kuhifadhi wafungwa na mahabusu lakini
linaendelea kupanuliwa kwa kuongezwa majengo zaidi. Kushoto ni Mkuu wa
Wilaya ya Chato, Shaaban Ntarambe, na kulia alyevaa sare, ni Mkuu wa
Gereza hilo, Joseph Busumabu. Masauni alifanya ziara katika Mkoa wa
Geita kwa kukagua ujenzi wa Kituo cha Polisi Chato, ujenzi wa Gereza
Chato na baadaye kukagua ujenzi wa nyumba 100 za askari polisi ambazo
zimeanza kujengwa mjini Geita.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimpa
maelekezo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo, mara
baada ya kumaliza kukikagua Kituo Kikuu cha Polisi cha Wilaya ya Chato
(nyuma pichani) ambapo ujenzi wake upo katika hatua ya mwisho
kukamilika. Masauni alifanya ziara katika Mkoa wa Geita kwa kukagua
ujenzi wa Kituo cha Polisi hicho, ujenzi wa Gereza Chato na baadaye
kukagua ujenzi wa nyumba 100 za askari polisi ambazo zimeanza kujengwa
mjini Geita.
Mkuu
wa Wilaya ya Chato, Shaaban Ntarambe, akimuonyesha Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) eneo la
pembezoni mwa Ziwa Victoria ambalo linaweza kufaa kujengwa Kituo cha
Polisi cha Wanamaji katika eneo hilo ili kuweza kuimarisha ulinzi zaidi.
Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo. Masauni
alifanya ziara katika Mkoa wa Geita kwa kukagua ujenzi wa Kituo kipya
cha Polisi Geita, ujenzi wa Gereza Chato na baadaye kukagua ujenzi wa
nyumba 100 za askari polisi ambazo zimeanza kujengwa mjini Geita.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa nyumba 100
za askari polisi zinazojengwa nje kidogo mwa mji wa Geita. Masauni
alisema ujenzi wa nyumba hizo utapunguza ukosefu wa nyumba kwa askari wa
mkoa huo mpya, hata hivyo nyumba zaidi ya elfu moja zinatarajiwa
kujengwa mkoani humo. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli
Mwabulambo. Masauni alifanya ziara mkoani humo kwa kukagua ujenzi wa
Kituo kipya cha Polisi Chato, ujenzi wa Gereza Chato na baadaye kukagua
ujenzi wa nyumba hizo 100 kwa ajili ya makazi ya askari polisi.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi, akimpa maneno ya
kumuagaNaibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(kushoto) mara baada ya kufanya mazungumzo naye ofisini kwake, jana.
Mkuu wa Mkoa huyo alimuambia Masauni wanashirikiana vizuri na vyombo
vilivyopo ndani ya Wizara yake na hali ya ulinzi na usalama ipo vizuri
mkoani humo. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Selestine Gesimba.
Masauni amemaliza ziara yake mkoani humo, ambapo alifanya ukaguzi wa
ujenzi wa Kituo kipya cha Polisi Chato, ujenzi wa Gereza Chato na
baadaye kukagua ujenzi wa nyumba 100 za askari polisi ambazo zimeanza
kujengwa mjini Geita. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Comments
Post a Comment