- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NA
PETER KIMATH, MOROGORO
WIZARA
ya Ardhi, Nyumba na Makazi kupitia Programu ya Kuwezesha Umilikishaji Ardhi (LTSP) wametoa mafunzo kwa mabaraza ya ardhi
ya vijiji ili kuweza kuwajengea uwezo na hatimaye kumaliza migogoro ya ardhi
inayoanzia ngazi ya chini.
Akizungumza
katika ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika Kata ya Kiberege na
kuhusisha vijiji vinne vya kata hiyo, Ofisa Ardhi Mwandamizi kutoka Wizara ya
Ardhi, Frank Mizikuntwe, alisema mafunzo hayo yatatolewa katika mabaraza ya ardhi
ya vijiji vyote vya Wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi ambapo ndipo upo
mradi wa LTSP kwa sasa.
Mizikuntwe
alisema, mafunzo hayo ya uwezeshaji ni kutekeleza mfumo ambao upo katika mradi
wa LTSP unaolenga kupima na kutoa hati lakini pia kuna kipengele cha utatuzi wa
migogoro ya ardhi
Alisema
walishaanza kutoa mafunzo katika mabaraza ya Ardhi ya kata na sasa zoezi hilo
linaendelea katika Wilaya za Ulanga na Malinyi na baada ya kuona hivyo imebidi
pia watoe mafunzo kwa mabaraza ya vijiji kutokana na huko kimsingi kuwa na
migogoro mingi inayohitaji usuluhishi itakayopelekea migogoro kutokwenda ngazi
ya juu.
Afisa
huyo mwandamizi Wa Ardhi alisema mafunzo hayo yatakuwa na awamu Mbili ambapo
awamu ya kwanza itaanza kwa vijiji 37 na baadae wataendelea katika vijiji kadri
vingine na kubainisha kuwa hali ya migogoro ya Ardhi katika Wilaya hizo bado ni
mbaya.
Kuhusu
kuongeza baraza la Ardhi la wilaya tokana na hivi sasa baraza Mona kuelemewa na
kesi nyingi toka Wilaya hizo tatu,Mizikuntiwe alisema awali baraza moja
lilitosheleza tokana na muundo wa Wilaya Mbili ila tokana na migogoro kuwa
mingi wameamua kutoa mafunzo kwa mabaraza na wakiona migogoro ibaendelea
wataangalia utaratibu Wa kuanzisha baraza lingine ila wataangalia uwezo Wa
kibajeti.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba katika Wilaya za Kilombero,
Ulanga na Malinyi, Roginus Rugarabamu, alisema mafunzo hayo ni muhimu kwani
migogoro mingi ya chini inatakiwa itatuliwe na wananchi wenyewe na siyo kufika
katika baraza lake.
Rugarabamu
alisema, wajumbe wa mabaraza wakipatiwa mafunzo na kuelewa wajibu wao wa
kusuluhisha migogoro itakuwa tiba kubwa kwa wananchi na kudai kuwa kwa sasa
kuna kesi 1,400 zinazoendela katika baraza lake na katika kesi hizo asilimia 80
zimekatiwa rufaa toka mabaraza ya kata.
Awali
akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, James Ihunyo, alisema
mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka baada ya kukithiri migogoro mingi ya ardhi
katika wilaya hizo na kusema kuwa migogoro mingi ni ya kutengenezwa.
Ihunyo
alisema, mabaraza mengi yanatoa maamuzi kimaslahi na kuwataka wajumbe kutoa haki
itakayosaidia kupunguza mrundikano wa kesi katika Baraza la Wilaya na
kusisitiza kuwa kama mjumbe anaona hawezi kazi aache na serikali inafuatilia
kwa karibu wale wanaofanya kazi kimaslahi zaidi.
Comments
Post a Comment