- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NA MWANDISHI
WETU, DODOMA
BAJETI Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019, ambayo ni ya tatu kwa Serikali ya
Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, itasomwa bungeni Mjini
Dodoma leo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango.
Mwenyekiti
wa Bunge, Mussa Zungu, aliyasema hayo bungeni Mjini Dodoma jana muda mfupi
kabla ya kuhitimisha shughuli za Bunge kwa siku hiyo.
“Bajeti
Kuu ya Serikali itasomwa kesho (leo), saa kumi jioni, asubuhi kutakuwa na
mpango wa maendeleo,” alisema.
Aliongeza kuwa, viongozi mbalimbali mashuhuri wakiwemo Mabalozi ambao wanaziwakilishi nchi zao nchini, watakuwepo bungeni na kuwataka wabunge wa vyama vyote kuwepo bungeni bila kukosa.
Aliongeza kuwa, viongozi mbalimbali mashuhuri wakiwemo Mabalozi ambao wanaziwakilishi nchi zao nchini, watakuwepo bungeni na kuwataka wabunge wa vyama vyote kuwepo bungeni bila kukosa.
Alisema baada ya hotuba hiyo,
wabunge wanaweza kwenda kuungana na familia na ndugu zao ili kusherehekea
sikukuu baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Akiwasilisha mapendekezo ya
Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/19 kwa wabunge Machi 13, mwaka huu, Dkt. Mpango
alisema bajeti hiyo inatarajia kukusanya na kutumia sh. trilioni 32.476, ikiwa
ni ongezeko la sh. bilioni 764 ukilinganisha na bajeti ya mwaka 2017/18.
Mpango alitaja vipaumbele vya
bajeti hiyo kuwa ni Mradi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Stiegler’s Gorge
katika Mto Rufiji kitakachozalisha megawati 2,100, ujenzi wa reli ya kisasa
(SGR), kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, kilometa 300 na Morogoro hadi
Makutupora kilometa 336 na uboreshaji wa Shirika na Ndege Tanzania (TTCL).
Pia kuna ujenzi wa bomba la
kusafirisha mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga, uzalishaji wa makaa
ya mawe na umeme Mchuchuma na Liganga, uendeshaji wa shamba la miwa, ujenzi wa
Kiwanda cha Sukari Mkulazi, mkoani Morogoro, uboreshaji bandari za Tanga, Dar
es Salaam na Mtwara.
Pia bajeti hiyo inatarajiwa
kupunguza bei ya vitu mbalimbali vikiwemo vinywaji baridi na vyakula ambapo
ongezeko la kodi linategemewa kuwepo kwenye vinywaji vikali pamoja na sigara.
Bajeti hiyo Kuu ya Serikali ya
Tanzania inatarajiwa kusomwa kwa wakati mmoja na bajeti za nchi zote wanachama
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Comments
Post a Comment