- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
OTTAWA, CANADA
Canada imepitisha sheria rasmi kwa nchi nzima inayoruhusu
matumizi ya bangi.
Sheria hiyo hatimaye ilishinda kwa kupata kura za ndiyo 52
zinazoruhusu matumizi ya bangi hadharani,huku kura 29 za maseneta zikisema
hapana.
Sheria hiyo inasimamia udhibiti,usambazaji na uuzaji wake.
Kwa sheria hiyo sasa raia wa Canada wataruhusiwa kununua na
kutumia bangi kihalali kuanzia mapema mwezi Septemba mwaka huu.
Kumiliki bangi ilikuwa ni kosa kisheria tangu mwaka 1923
lakini matumizi ya bangi kama dawa yaliruhusiwa kisheria tangu mwaka 2001.
Kutokana na kupitishwa kwa sharia hiyo sasa itawachukua
majimbo, Manispaa na mamlaka takribani wiki kati ya nane hadi 12 kutengeneza
masoko mapya ya kuuza bangi.
Lakini pia muda huu kabla ya kuanza kutumika kwa bangi
rasmi,utatumika na Polisi kuandaa mifumo mipya ya kisheria.
Kwa mjibu wa sheria hii mpya mtu ataruhusiwa kuagiza bidhaa
hii ya bangi kwa mfumo wa kimtandao kutoka kwa wasambazaji wanaotambulika
kisheria.
Watu nchini Canada ni baadhi ya watumiaji wakubwa wa bangi
duniani.
Watu wazima wataruhusiwa kumiliki hadharani hadi gram 30 ya
bangi kavu hadharani.
Umri unaoruhusiwa kununua na kutumia bangi umepitishwa kwa
mjibu wa sharia hiyo kwamba ni kuanzia miaka 18,lakini baadhi ya majimbo
yamependekeza umri wa kuanzia miaka 19. Ni
Ni kwa nini Canada
ifanya hili sasa?
Sheria hiyo inahitimiza ahadi ya kampeni ya Bw Tudeau,
kioongozi wa chama cha Liberal.
Waziri huyo mkuu amesema kuwa sheria za miaka mingi za
Canada zinazoharamisha matumizi ya bangi hazina maana kwa kuwa watu nchini
Canada ni baadhi ya watumiaji wakubwa wa bangi duniani.
Kura za maoni zimekuwa zikionyesha kuwa watu wengi nchini
Canada wanaunga mkono hatua hiyo.
Hatua ya kuhalalisha matumizi ya bangi kwa burudani nchini
Canada yanakuja wakatoi nchi za dunia zinahalalisha bangi inayotumiwa kwa
kiwango kikubwa duniani.
Comments
Post a Comment