- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
MADRID,
HISPANIA
ZINEDINE Zidane
amesema anaachia ngazi Real Madrid siku tano baada ya kuwaongoza kushinda Ligi
ya Mabingwa Ulaya.
Zidane
aliisaidia Real kushinda mechi 104 kupata sare mechi 29, na kujipatia asilimia
69.8% ya ushindi mbali na mataji tisa.
Zidane
aliambia mkutano na vyombo vya habari kwamba kila kitu kinabadilika na kwamba
hiyo ndio sababu ya uamuzi wake.
Anaondoka
baada ya kuisaidia klabu hiyo kushinda mataji matatu ya klabu bingwa na taji
moja la ligi ya La Liga tangu achukue hatamu mnamo mwezi Januari 2016.
"Naipenda
klabu hii," aliongezea.
"Kile
ninachofikiria ni kwamba timu hii inafaa kuendelea kushinda ,lakini nadhani
inahitaji mabadiliko, sauti mpya, mbinu mpya. Na hiyo ndiyo sababu ilionisukuma
kufanya uamuzi huu."
Zidane,
45, alichukua uongozi wa klabu hiyo baada ya Rafael Benitez kufutwa kazi na alisimamia
mechi 149 games.
Aliisaidia
Real kushinda mechi 104 kupata sare mechi 29, na kujipatia asilimia 69.8% ya
ushindi mbali na mataji tisa.
Alisema
mnamo mwezi Januari kwamba ataondoka katika klabu hiyo atakapohisi kwamba hana
la ziada kuisaidia timu hiyo.
Hatahivyo
, tangazo linaonekana kuwashangaza wengi kwa kuwa linajiri siku chache tu baada
ya Real kuishinda Liverpool 3-1 katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
"Hii
ni klabu ambayo imeshinda mataji 13 ya Ulaya, kwa hivyo nafurahia kuwa miongoni
mwa historia yake," alisema baada ya ushindi mjini Kiev.
"Tutafikiria
kuhusu kile tulichofanikiwa kufanya. Tufurahie. Huu ndio wakati muhimu zaidi."
Mkufunzi
wa Tottenham, Mauricio Pochettino, amehusishwa na klabu ya Real siku za hapo
nyuma. Raia huyo wa Argentina hata hivyo aliweka kandarasi ya miaka mitano na
Spurs wiki iliyopita.
Mkufunzi
wa Juventus, Massimiliano Allegri, huenda pia akahusishwa kujaza pengo hilo,
huku Arsene Wenger akitaka kuendelea na ukufunzi baada ya kuondoka Arsenal
baada ya miaka 22.
Mkufunzi
raia wa Italia, Maurizio Sorri wa klabu ya Napoli pia anapatikana. Uamuzi wa ni
nani atakayesimamia Real Madrid utatolewa na rais wa klabu hiyo Florentino
Perez.
Aliandamana
na Zidane katika mkutano huo na vyombo vya habari na kusema kuwa angependelea
kumshinikiza mshindi huyo wa Kombe la Dunia mwaka 1998 kusalia katika klabu
hiyo.
"Huu
ni uamuzi ambao hatukutarajia. Zidane aliniambia kuhusu uamuzi wake jana,"
aliongezea Perez.
Kuondoka
kwa Zidane kunajiri baada ya Gareth Bale na Christiano Ronaldo kufichua kwamba
wanafikiria hatma yao katika klabu hiyo.
Mshambuliaji
wa Wales, Bale hakufurahia kushiriki katika mechi ya fainali ya klabu bingwa
dhidi ya Liverpool kama mchezaji wa ziada huku Ronaldo akisema baada ya mechi
hiyo kwamba atafanya uamuzi kuhusu hatma yake.
Alipoulizwa
iwapo uamuzi wake unatokana na Ronaldo, Zidane alisema: Real inatafuta meneja
wake wa tano katika kipindi cha miaka mitano.
Comments
Post a Comment