- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Watuhumiwa 24 walioshtakiwa kuhusiana na kashfa ya ufujaji
wa pesa katika Shirika la Vijana wa huduma kwa Taifa (NYS) watakaa rumande kwa
wiki moja.
Jaji ameamuru wazuiliwe hadi Jumatano wiki ijayo ambapo
uamuzi wa kuachiliwa kwa dahamana utatolewa.
Miongoni mwa walioshtakiwa jana ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Vijana na Jinsia Lilian Mbogo Omollo na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Richard
Ndubai.
Walikamatwa na wengine wakajisalimisha kwa polisi Jumatatu
wiki hii na kisha kufikishwa kortini Milimani, Nairobi jana.
Kikao cha kusikizwa kwa kesi dhidi yao kiliendelea hadi
usiku wa manane.
Upande wa mashtaka ulikuwa umepinga kuachiliwa kwao ukisema
wanaweza kutoroka au kukosa kurejea mahakamani wakati wa kusikizwa kwa kesi
dhidi yao.
Comments
Post a Comment