Vijana 11 raia wa Tanzania waishio
Johannesburg, Afrika Kusini walioshtakiwa kosa la ubakaji wameachiliwa
huru na hakimu mkazi wa Mahakama ya Johannesburg. Walikuwa wameshtakiwa kwa makosa ya kumteka nyara na kumbaka mwanamke mjamzito Thelma Mondowa raia wa Zimbabwe mwaka uliopita. Waliachiliwa huru na Jaji Metisie kwa kukosekana kwa ushahidi. Wakili
wa upande wa mashtaka wa serikali alikuwa amemfahamisha hakimu kuwa Bi
Thelma Mondowa aliamua kurejea Zimbabwe na wameshindwa kupata anwani
yake. Mwanamke huyo iliarifiwa alikuwa akitoka kazini na
mfanyakazi mwenzake wa kiume pale ghafla walipovamiwa na kundi la
wanaume wenye silaha na wakamvuta mwanamke huyo kabla ya kumpiga
mfanyakazi mwenzake ambae baadaye alifanikiwa kutoroka. Kisa hicho kilitokea mnamo 15 Mei mwaka 2015 katika barabara ya 270 Lilian Ngoyi mjini Johannesburg. Baada ya mfanyakazi huyo kutoroka aliwapigia simu
polisi na wakafanikiwa kufika eneo la tukio na kuwakuta wanaume hao
wakimbaka kwa zamu mwanamke huyo. Polisi wapatao kumi waliingia kwenye jengo ambapo tukio lilidaiwa kufanyika na kumuokoa mwanamke huyo na kumpeleka hospitalini.
Comments
Post a Comment