- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
(Mwanaharakati Huru) -
Mwanachama wa JamiiForums ameandika hivi kwenye JF leo majira ya saa 08:31hrs akieleza kwamba, haya ni maneno ya Mwanasheria wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu:
Mimi sio mwanachama wa CCM lakini kwa umuhimu wa hoja hii,
na ukweli kwamba mabadiliko katika siasa za ndani za CCM yanatuathiri wote kwa
njia mbali mbali, naomba kuichangia.
Kwanza, kuna
mambo yanayohitaji uthibitisho wa Katiba na Kanuni za CCM. Je, kwa mfano, bado
Baraza la Ushauri la waliokuwa viongozi wakuu wa CCM na Serikali???
Sina Katiba ya
CCM hapa lakini nimewahi kusoma makala, nadhani ya Fatma Karume, ya mwaka jana
kama sikosei, ambako alidai kwamba Baraza la Ushauri lilivunjwa wakati Kikwete
akiwa Mwenyekiti wa CCM.
Tunahitaji
uthibitisho wa hili ili tuweze kupima hoja ya ole Mushi juu ya majukumu au
umuhimu wa chombo hicho.
Je, kuna
ukweli gani kuhusu maneno yaliyojitokeza mwaka jana wakati wa Mkutano Mkuu wa
CCM kwamba sasa, kwa mabadiliko ya Katiba ya CCM, Mwenyekiti wa CCM atakuwa
automatically mgombea uRais wa CCM kwenye Uchaguzi Mkuu???
I hope umuhimu
wa suala hili ni self-evident for any serious analysis of the current
correlation of power within CCM.
Kama
Mwenyekiti ni mgombea Urais bila kupingwa maana yake ni kwamba vikao vya
maamuzi vya chama vitafanya kazi ya rubber stamp tu.
Eneo la tatu
linalohitaji uthibitisho wa kikatiba linahusu composition ya Kamati Kuu ya sasa
ya CCM. Ole Thadei ametupa composition ya Kamati Kuu ya CCM iliyopita, sio ya
sasa.
Ninafahamu
Kamati Kuu ya sasa ina wajumbe 24, ukilinganisha na 36+ wa iliyopita. Hawa wa
sasa ni akina na, crucially, wanapatikanaje. Umuhimu wa hili nao should be self-evident
kwenye analysis yoyote ya correlation of power within the party.
Baada ya
utangulizi huu, sasa nitoe hoja yangu ya pili ambayo ni evolution ya CCM kama
'chama-dola' na sura yake ya sasa. Nadhani sitakosea nikisema kwamba angalau
tangu mwaka '64/'65, tumekuwa na 'chama-dola', yaani chama cha siasa ambacho
kimeingiliana na vyombo vya dola kwa namna ambayo haviwezi kutenganishwa
kirahisi, hata kwenye uchambuzi wa kitaaluma.
Chama-dola
kilianza kwa wakati mmoja na kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka
'64. Katiba ya kwanza ya Jamhuri ya Muungano ilitamka hivyo wazi kwa mara ya
kwanza: Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar itakuwa nchi ya chama
kimoja, i.e. TANU kwa Tanganyika na ASP kwa Zanzibar.
Mwaka huo huo,
JWTZ ilianzishwa kufuatia maasi ya Tanganyika Rifles ya January '64. Sehemu
kubwa ya Jeshi jipya ilitokana na wanachama wa TANU Youth League. Baadaye kama
inavyojulikana, vyombo vingine vyote vya dola, Utumishi wa umma na hata taasisi
za kitaaluma viliingizwa kwa dragnet kubwa ya chama-dola.
Mageuzi ya
kisiasa ya 92' hayakubadili sana hulka ya CCM kama chama-dola. Makatazo ya
uanachama wa vyama vya siasa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano yaliyowahusu
wanajeshi, watumishi wa umma na wa Mahakama yalificha uchama-dola wa CCM.
Haikuuondoa
kama mifano mingi ya watumishi wa umma au wanajeshi au majaji wanaoacha
utumishi wao halafu mara moja wakateuliwa kwenye nafasi kubwa za kichama,
inavyothibitisha.
Aidha, kuna
nafasi nyingine katika utumishi wa umma ambazo bado zinahusishwa moja kwa moja
na CCM na zinadhihirisha uchama-dola wake. Kwa mfano, Wakuu wa Mikoa na Wilaya,
ambao ni wenyeviti wa Kamati za Ulinzi na Usalama za maeneo yao na wana
residual police powers, bado wanatakiwa na Katiba ya CCM kuwa wanachama na
wajumbe wa vikao vyote vya maamuzi katika maeneo yao.
Sasa kipi
kimebadilika kati ya CCM ya Kikwete na Makamba/Mkapa na Mangula na CCM ya sasa
ya Magufuli??? Obviously, mabadiliko ni makubwa sana na yanakwenda mbali zaidi
kuliko muonekano wa nje.
Kwanza, tangu
Magufuli aingie madarakani na kuwa Mwenyekiti, 'udola' ndio umekuwa na nguvu
zaidi kuliko 'uchama' wa CCM. Hili ni badiliko kubwa na la msingi.
Tangu miaka ya
mwanzo ya chama-dola, 'uchama' wa CCM ulikuwa na nguvu na ulionekana wazi zaidi
kuliko 'udola' wake. Vyombo vya dola vilikuwa 'subsumed' kwenye vyombo vya
chama.
Maamuzi
makubwa ya nchi yalifanywa kwanza na chama na baadae kutekelezwa na vyombo vya
dola ambavyo na vyenyewe vilikuwa sehemu ya vyombo vya chama. CCM ya aina hiyo
iliisha na Urais wa Ali Hassan Mwinyi, lakini mabaki yake yaliendelea hadi CCM
ya Kikwete na Makamba.
CCM hiyo
ilikuwa bado inafanya kazi ya siasa autonomously of vyombo vya mabavu vya dola;
hata kama jambo hilo lilififia sana mpaka ikabidi Kikwete awaambie wanaCCM
wafanye kazi ya siasa badala ya kutegemea kubebwa na vyombo vya dola.
CCM hiyo
ilikuwa inaendeshewa Dodoma au Lumumba na Katibu Mkuu wake, whether Mangula wa
Mkapa au Makamba/Mukama/Kinana wa Kikwete. CCM hiyo ilikuwa na uwakilishi mpana
wa constituencies mbali mbali na ndio maana ya factionalism iliyokuwepo ndani
yake.
CCM ya
Magufuli ni tofauti kabisa. Hii ya sasa inaendeshewa Ikulu na Magufuli
mwenyewe, sio Dodoma au Lumumba na Katibu Mkuu wake.
In fact,
tukiweka ushabiki pembeni, ni sahihi kusema kwamba CCM ya sasa imekuwa haina
Katibu Mkuu tangu Magufuli aingie madarakani.
Mnaweza
kulinganisha tu tofauti kati ya Kinana wa Kikwete na Kinana wa Magufuli; au
kati ya Nape Nnauye wa Kikwete na Humphrey Polepole wa Kikwete. Nape alikuwa
Msemaji Mkuu wa CCM, sasa haijulikani kama Msemaji Mkuu ni Polepole wa Lumumba
au Gerson Msigwa wa Ikulu.
Na haijulikani
tena kama Ikulu ni Makao Makuu ya Rais, au nayo imegeuka kuwa Ofisi Ndogo ya
CCM badala ya Lumumba au White House ya Dodoma. Ndio maana hata ole Thadei
amechanganyikiwa.
Mabadiliko
haya yamekwenda hata mikoani na wilayani. Huko CCM ya sasa inaendeshwa na Wakuu
wa Mikoa na Wilaya, wakiwatumia au kusaidiwa na ma-RPC na ma-OCD.
Hii ndio maana halisi ya haya tunayoyaona ya
akina Bashite, Gambo, Mnyeti na Malima na wengineo wengi. Kauli zao sio za
bahati mbaya au za watu wasiojua wanachokifanya. Ni kauli zinazoonyesha uso
halisi wa CCM ya sasa.
CCM hii
haijishughulishi tena na kazi ya kawaida ya chama cha siasa: kushawishi
wananchi kwa kutumia hoja za kisiasa. CCM ya Magufuli inakataza kazi ya kawaida
ya chama cha siasa. Haina ushawishi wa wanasiasa, ina amri ya watawala.
Kwa sababu ni
CCM ya amri, ndio maana vyombo vya mabavu vya dola sasa vimekuwa na umuhimu
mkubwa katika siasa zetu. Badala ya hoja za kisiasa kujibiwa kwa hoja za
kisiasa, sasa zinajibiwa kwa risasi za moto, mabomu na magereza.
Sasa majasusi
wa polisi na Usalama wa Taifa wako kila mahali mitandaoni wakiwinda watu
wanaofanya siasa za kawaida kabisa mitandaoni za kukosoa serikali au viongozi
wake. Sasa tuna kosa jipya la jinai ambalo halipo kabisa kwenye Sheria zetu:
'kumtukana Rais.'
Tumeingia kwenye
giza nene katika siasa za nchi yetu kwa sababu ya mabadiliko haya katika siasa
za CCM.
Kwa hiyo,
suala muhimu sasa sio akina nani wako kwenye vikao vya juu vya CCM au kuna
mikutano mingapi ya CC au NEC kwa mwaka. Suala muhimu zaidi ni vikao hivyo vina
maana gani tena katika mazingira ambayo CCM 'chama' imefunikwa kabisa na CCM
'dola.'
CHANZO: JAMIIFORUMS
Comments
Post a Comment