Liverpool imekubali kumsajili kiungo
wa Monaco Fábio Henrique Tavares maarufu kama Fabinho kwa ada ya Paundi
Milioni 40 ambayo inaweza kuongezeka kutokana na kiwango cha mchezaji. Fabinho mchezaji wa kimataifa wa Brazil mwenye miaka 24 atajiunga na Liverpool Julai 1. Kiasi
cha ziada cha ada ya uhamisho wake ambacho ni Paundi Milioni 5 kinaweza
kuongezeka kutokana na mafanikio atayoipa Liverpool. Kuwasili kwake ni kwa ajili pia ya kuziba pengo la Emre Can ambaye anatarajiwa kutimkia kwa mabingwa wa Seria A Juventus muda wowote. ''Hiki ni kitu ambacho sikuzote nimekuwa nikikitamani- hii ni timu kubwa, ''alisema Fabinho. ''Nimefurahishwa sana.'' Meneja
wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ''Huyu ni mchezaji ambaye ana faida
sana uwanjani, anaweza kucheza nafasi nyingi, namba sita, nane ama namba
mbili'. Hili ni jambo zuri sana.'' Fabinho ambaye mkataba wake unatarajiwa kuanza Julai 1 amesema Liverpool ni klabu yenye miundombinu mizuri na ya kuvutia.
Comments
Post a Comment