Wamiliki wa vyombo
vya usambazaji habari kama vile blogu, TV na redio za mitandaoni nchini
Tanzania wametakiwa kujisajili na kufuata maadili kwa mujibu wa kanuni
husika.
Hatua hiyo inajiri baada ya serikali kushinda kesi iliofunguliwa na wadau wa habari kupinga kanuni za maudhui mitandaoni 2018. Kulingana
na taarifa hiyo iliochapishwa na mkurugenzi wa idara ya habari na
maelezo na msemaji mkuu wa serikali Daktari Hassan Abbasi, walalamishi
waliwasilisha maombi ya kupata ridhaa ya kufungua shauri la kufanyiwa
marejeo kanuni hizo zilizosainiwa na waziri mwenye dhamana ya habari
ambazo pamoja na mambo mengine zinasimamia zinasimamia usajili na kuweka
mfumo wa uwajibikaji na maadili kwa wamiliki wa mitandao ya kijamii
inayohusika na habari. Katika kesi hiyo, serikali iliweka pingamizi tatu za kisheria
ambapo pamoja na mambo mengine iliomba mahakama kutupilia mbali maombi
hayo kwa kuwa walalamishi hawakuthibitisha kuwa wana haki ya kikatiba
ambazo zitavunjwa na kanuni hizo, hoja ambazo zilikubaliwa na mahakama
kuyatupilia mbali maombi hayo. ''Kwa hukumu hiyo , tunatumia fursa hii kuutarifu
umma kuwa sasa wamiliki wa mitandao ya kijamii inayohusika na usambazaji
wa habari kama blogu, TV na redio za mitandaoni na wengine
walioainishwa katika kanuni wanapaswa kuendelea kujisajili na kufuata
maadili kwa mujibu wa kanuni husika'', ilisema serikali katika taarifa
hiyo. Serikai ilisema kuwa wale wanaotuma maombi watahitajika
kuwasilisha stakhabdhi zao ikiwemo maelezo ya hisa, uraia, kibali cha
kuonesha wanalipa kodi mbali na mipango ya mafunzo. Wanablogu
ambao wataopatikana na hatia ya kutoheshimu sheria hizo mpya
watakabiliwa na faini ya hadi milioni 5 ama kifungo kisichopungua miezi
12 ama zote mbili kulingana na sheria hizo mpya, ilisema taarifa hiyo. Rais
Magufuli alitoa agizo la kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote
atakayechapisha habari za uongozi kuhusu serikali katika mitandao ya
kijamii.
Idadi ya watumiaji wa mitandao nchini Tanzania ilipanda hadi asilimia 16, 2017.
Comments
Post a Comment