- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NA SELINA MATHEW, DODOMA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, amesema kama Serengeti Boys waliweza kushinda
kwenye mashindano yaliyopita na kuleta ushindi nyumbani basi ana uhakika
watashinda hata kwenye Kombe la Bara la Afrika.
Aidha, amewapongeza vijana hao kwa heshima kubwa waliyoipa
nchi baada ya kutwaa ubingwa wa Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA)
nchini Burundi na kuomba malezi ya vijana hao yasimamiwe ili yasiende kupotea
mitaani baadaye.
Jafo aliyasema hayo jana wakati akizindua matangazo ya moja
kwa moja ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari (Umisseta) na ya Umoja wa
Michezo wa Shule za Msingi Tanzania (Umitashumta) yatakayorushwa na kituo cha
Televisheni cha Azam kuanzia Juni 4 hadi 29 mwaka huu katika viwanja vya
Butimba vilivyopo jijini Mwanza.
“Taifa letu limepata heshima kubwa kupitia vijana hawa juzi
juzi waziri aliweza kuwapokea pale uwanja wa ndege, vipaji vya vijana wale
walioweza kucheza mpira na kuzifunga timu zote tokea mwanzo mpaka wamemaliza ubora
wao ni ubora wa hali ya juu.
"Waziri Mwakyembe tuwaatamie vizuri tusiwapoteze vijana
wale, mimi naamini kama tuliweza kuzishinda timu zote tukiwalea vizuri mpaka
mwisho vijana wale nina uhakika tunaenda kushinda kombe la bara la afrika sina
mashaka na nyinyi,” aliongeza Jafo.
Waziri Jafo aliwataka maofisa elimu wa mikoa hasa
wanaosimamia michezo nchini kuhakikisha
wanawapeleka walimu wa michezo waliofundishwa katika shule za michezo ili
wafundishe shule maalum zilizotengwa kuandaa vijana kimichezo.
“Waziri Ndalichako unasimamia sera na umetoa maelekezo kwa
mujibu wa sera na hivi sasa kila mkoa tuna shule zipatazo mbili za michezo, na
bahati nzuri kwa taarifa za wataalam wangu shule zile zimeanza kusimamiwa
vizuri kwa kuinua vipaji vya vijana wetu ndani ya nchi yetu, hivyo naomba
mlisimamie,” alisisitiza.
Aidha, alisema kitendo cha Televisheni ya Azam kurusha matangazo hayo moja kwa moja kitatoa
hamasa kwa vijana wenyewe na wazazi kuona umuhimu wa michezo hiyo na kuruhusu
watoto wao kuweza kushiriki lakini huku akiwataka wadau kuunga mkono jitihada
hizo.
Awali, akizungumza katika uzinduzi huo waziri wa Elimu, Sayansi
na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisisitiza kila mkoa kuhakikisha
wanakuwa na shule mbili mahsusi kwa ajili ya michezo ili kuinua kiwango cha
michezo kwa vijana.
Comments
Post a Comment