- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino Athumani Masasi
Jengo la upasuaji linalojemgwa katika kituo cha afya chamwino
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mhe. Deo Ndejembi katika ukaguzi wa miundombinu ya kituo cha afya Mlali wilayani Kongwa.
Baadhi ya majengo mapya katika kituo cha afya Mlali wilayani Kongwa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akifurahishwa na uwekaji wa Tiles katika majengo mapya ya kituo cha afya Mlali Kongwa.
…………………………………………………………………………..
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma kuongeza kasi ya ujenzi katika kituo cha Afya Chamwino.
…………………………………………………………………………..
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma kuongeza kasi ya ujenzi katika kituo cha Afya Chamwino.
Jafo ameyasema hayo alipofanya ziara kituoni hapo kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu unaofanyika katika kituo hicho.
Akizungumza katika ukaguzi huo, Waziri Jafo amefurahishwa na ubora wa majengo yanayojengwa na kwamba ni vyema ikaongezwa kasi ya ujenzi ili yakamilike kwa haraka.
“Mafundi ongezeni kasi ya ujenzi kituo hichi cha Afya kikamilike haraka ili wananchi wapate huduma.
Katika Zara hiyo, waziri Jafo pia amefanikiwa kufanya ukaguzi katika kituo cha Afya chamwino wilayani Chamwino pamoja na kituo cha Afya Mlali kilichopo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
Vituo hivyo viwili ni miongoni mwa vituo vya afya 208 vinavyoboreshwa na serikali ya awamu ya tano.
Comments
Post a Comment