- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Na Moses Machali
KWANZA nianze
kwa kusema kwamba uhamiaji kumshuku na kumtuhumu mtu kuwa siyo raia wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na kuamua kumuhoji ni sehemu ya wajibu wao.
Na ni
ujinga kuwaaminisha watu wote kwamba mkazi mmoja au mzawa yeyote wa Mkoa wa
Kigoma akituhumiwa na uhamiaji kuhusu uraia wake au kwa kosa lolote basi tuhuma
hizo ni wazawa wote wa Mkoa wa Kigoma.
Kufanya
hivyo siyo sahihi kwa namna yote iwavyo kwa sababu wapo watanzania wengi
wameowahi kutuhumiwa kuwa siyo Raia kisha wakathibitika ni raia na wakaachwa
huru.
Kwa mujibu
wa sheria ya Uhamiaji ya Mwaka 1995 chini ya kifungu cha 7 (d) “Without prejudice to the generality of
section 6, and for the purpose of the better administration of this Act, any
immigration officer may- if he has reasonable cause to suspect that any person
has contravened any of the provisions of this Act or of any regulations made
here-under or that the presence in Tanzania of any person is unlawful, and if
he is of opinion that in order to prevent justice from being defeated it is
necessary to arrest such person immediately arrest any such person without
warrant, and such person shall be brought before a magistrate as soon as is
practicable.”
Kifungu
hicho kinawapa maafisa Uhamiaji haki ya kumkamata na kumuhoji mtu yeyote ambaye
wana mashaka naye kuwa yupo nchini kinyume cha sheria.
Aidha,
tuhuma za Uhamiaji dhidi ya mtu yeyote kuhusu uraia wake siyo za mwisho bali
raia ambaye ataona kaonewa bado ana nafasi ya kukata rufaa kwa mamlaka nyingine
kwa mujibu wa sheria hii ya uhamiaji, yaani The Immigration Act, 1995.
Kwa hiyo
Zitto na wenzake ambao wanaweza kuwa wanalitumia suala la Abdul Nondo kisiasa
kwa manufaa yao ya kisiasa waache kulifanya kuwa ni dhambi Uhamiaji kumtaka
Nondo kuthibitisha iwapo ni raia au siyo raia wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa sababu ni sehemu ya wajibu wao Uhamiaji kutuhumu kwa haki na
kufanyia kazi tuhuma zote kwa haki.
Iwapo
Abdul Nondo atathibitisha ni raia ataachwa huru kama wewe zitto ilivyowahi
kuachwa huru.
Nondo siyo
wa kwanza kutuhumiwa na wala wewe Zitto haukuwa wa Kwanza Kutuhumiwa na wala
haiwezekani Nondo akawa wa mwisho kutuhumiwa kwa sababu dunia ina watu wengi na
walimwengu hao wanaweza kuhamia ktk nchi yetu kiharamia na kusababisha matatizo
ya kisiasa; kiuchumi; na kijamii na kwa hiyo lazima Uhamiaji wapewe meno ya
ku-dili nao kwa ku- establishi tuhuma dhidi yao kwa haki huku wale
watakaothibitika tuhuma haziwahusu wataachiwa huru.
Sasa Zitto
kwa nini unawapiga mkwara Uhamiaji waache kutimiza moja ya wajibu wao kwa
mujibu wa sheria na kutaka kulifanya suala la Nondo ni issue ya watu wote wa
Mkoa wa Kigoma?
Ningesema
unafanya uzwazwa lakini nakustahi kama kaka lakini siwezi acha kusema ni ujinga
wa kiwango cha juu.
Mhe.
Zitto, mbona haukuwahi kulifanya suala la Bashe kuwa la Watanzania wote mwaka
2010 au kwa sababu Bashe ni mwanachama wa CCM?
Mnamtumia
Nondo vibaya na sasa anaharibikiwa kwa sababu ya uchanga wake kifikra.
Nondo hana
maarifa mapana kuhusu Siasa za Kikanjanja, na hajui kwamba wapo wanasiasa
wanaweza kuwatanguliza vijana mbele halafu watakapoharibikiwa watabakia wao
kama wao na hatimaye future zao zinaenda kombo.
Waswahili
husema kuwa uyaone na akili za kuambiwa changanya na zako. Nondo hajachanganya
na zake bali kaona atapata umaarufu kwa kutumika vibaya kama inavyodhaniwa.
Vijana
kama akina Philipo Mwakibinga ni maadhura wa siasa kanjanja kama anazofanyiwa
Nondo leo hii. Mwakibinga na wengine wengi waliokuwa wakisoma vyuo vikuu
mbalimbali walipoteza fursa za kuhitimu masomo yao ya chuo kikuu huko UDOM;
UDSM, NK.
Hata mimi
niliwahi kunusurika nikiwa nafanya shahada yangu ya kwanza kule SAUT mwanza,
bahati nzuri niliachwa kwa kuwa nilikuwa nimebakiza mtihani mmoja wa
kuhitimisha muhula wa mwisho kabisa wa elimu yangu ya shahada ya kwanza.
Ilibakia
Kidogo Cahdema iniponze. Vinginevyo kwa mujibu wa Mwadili wa wanafunzi yaani Dean
Of Students kwa zama zile ningeonja joto la jiwe kama walivyoonja akina Philipo
Mwakibinga kule UDOM.
Ndiyo maana
nasema kijana kama Nondo anaponzwa na ufinyu wa maarifa kuhusu wanasiasa
makanjanja ambao huwatumia wakati wakiwa na shida nao lakini dude likiamshwa
hubakia peke yao na janga watalikabili wenyewe vijana kama Nondo.
Vijana
acheni kuvimbishwa vichwa halafu mnajiona wanasiasa kanjanja wanawajali kwa
sababu mwisho wa siku watawaacha solemba yaani mtabikia na majanga yenu huku
wakiishia kusema poleni sana na ndiyo harakati za ukombozi. Kijana jiulize hayo maneno yanakusaidia nini?
Mhe.
Zitto, Historia inaeleza kuwa hata Jenerali Ulimwengu aliwahi kuhojiwa na
Uhamiaji.
Wengine ni
akina Husein Bashe Mbunge wa Nzega; Wallace Karia Rais wa sasa TFF; wewe
Mwenyewe Zitto Kabwe; Hezekia Wenje aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana; na watu
wengine mashuhuri na wasio mashuhuri wana CCM na wasio wana CCM wamekuwa
wakituhumiwa na kuhojiwa na mamlaka za nchi.
Haikuwahi
kutokea mtu yeyote kutaka kuzifanya tuhuma hizo kuwa ni za wakazi wote wa mkoa
wowote ule au ni tuhuma na dharau kwa watu wa mkoa wowote ule au dharau kwa
wananchi wote wa taifa hili.
Ndiyo
maana nasema ni ujinga wa kiwango cha juu kwa mtu mweledi na mjumbe wa Bunge
linalotunga sheria unayeelewa fika kwamba sheria inawapa haki maafisa wa
uhamiaji kumuhoji na kumtaka mtu yeyote kuthibitisha au kutoa taarifa zake
kuhusu uhalali wa uraia wake.
Kwa hiyo
Nondo ni mtu kama watu wengine ambao wamewahi kutuhumiwa.
Hakuna
sababu ya kulifanyia siasa suala la Bwanamdogo huyo ili kujipatia kiki kisiasa.
Kama anaonewa itafahamika tu na ataachiwa huru.
Waache
Uhamiaji wafanye kazi yao. Nawe kama una maelezo ya ziada kuhusu uhalali wa
Nondo basi saidia kuthibitisha hilo badala ya kutaka kwamba kila mtu wa Kigoma
aone tuhuma za Nondo ni za kwake wakati sivyo ilivyo.
Nondo
amaetuhumiwa yeye kama yueye na hivyo sisi wazawa wengine wa Kigoma
hatujatuhumiwa kama unavyotaka ionekane.
Aidha,
usitake kuaminisha watu kwamba wanaothumiwa ni wazawa wa Kigoma tu. Jiulize
Hivi Bashe ni mzawa wa Kigom? Wallace Karia Rais wa sasa wa TFF ni mzawa wa
Kigoma? Sijui mkoa aliozaliwa Mzee Jenerali Ulimwengu lakini nafikiri siyo
mzawa wa Mkoa wa Kigoma, nk.
Je, kwa
nini unafanya propaganda kwamba wanaotuhumiwa ni watu wa kigoma pekee?
Unawakosea
Uhamiaji kwa kutaka kuwazuia wasifanye kazi yao jambo ambalo linaweza kuwa kosa
kisheria pia.
Nakutakia
kazi njema na busara itamalaki kichwani mwako na katika roho yako kaka na
wengineo wanaopotosha suala hilo.
Comments
Post a Comment