Meneja
wa Bandari ya Tanga Percival Salama akizungumza na waandishi wa habari
mkoani Tanga leo kuhusu mikakati wa bandari hiyo kulia ni Afisa Mipango
wa Bandari Moshi Mtambalike.
Meneja
wa Bandari ya Tanga Percival Salama katikati akizungumza kushoto ni
Afisa Utekelezaji Mkuu wa Bandari hiyo Donald Ngaire na kulia ni Afisa
Mipango wa Bandari Moshi Mtambalike
PRO wa Bandari ya Tanga,Moni Jarufu akizungumza katika mkutano huo
Mwandishi wa Habari wa Daily News na Habari Leo mkoani Tanga Cheji Bakari akiuliza swali kwenye mkutano huo
Sehemu ya waandishi wa habari wakichukua taarifa kushoto ni Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania mkoani Tanga
MENEJA wa Bandari ya Tanga Privical Salama amewataka wafanyabiashara
nchini kuendelea kutumia bandari ya Tanga kwa sababu ina uwezo mkubwa wa
kuhudumia shehena kwa haraka kutokana na maboresha makubwa
yaliyofanyika. Salama aliyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari
ambapo alisema bandari hatua yao ya kuhudumia mzigo nangani
hakusababishi ikiwa na uwezo mdogo wa kiutendaji . Alisema hata nchini Singapore bado wanahudumia mzigo nangani na baadae
kuleta nchi kavu hivyo wafanyabiashara wanapaswa kutumia bandari hiyo
kusafirisha bidhaa zao. “Bandari ya Tanga kuhudumia mzigo nangani hakusababishi kuwa na uwezo
mdogo wa kiutendaji kwani hata nchi ya Singapore bado inatumia kuhudumia
mzigo nangani kuleta nchi kavu hivyo niwatake wafanyabiashara kutumia
bandari hii kusafirisha mizigo yao“Alisema Meneja Salama. Alisema Bandari hiyo hivi sasa ina uwezo mkubwa wa kuhudumia wateja
ambao watakuwa wakipitisha mizigo kutokana na kuwepo kwa matishari ya
kutosha kuhamisha mizigo kati ya gatini na melini nangani inapofika. “Kwani tunaweza kufanya mzunguko wa nyuzi 360 melini hakuna mashine
itakayosimama gatini hivyo kuongeza ufanisi mkubwa wakati wa kuhudumia
shehena inayowasili “Alisema. Hata hivyo alisema bandari ya Tanga ni bora na ina uwezo wa kutoa huduma
kwa kasi kutokana na uwepo wa vifaa vya kisasa ambacho vinatumika
kufanya kazi hizo kwa wakati (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
Comments
Post a Comment