- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri wa Maliasili
na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha
pili cha wadau wa utalii kutoka nchi mbalimbali zinazohusika na tamasha
la ‘Urithi wa Utamaduni wa Mabara’ Jijini Dar es Saalam jana.
Na Hamza Temba, WMU
TANZANIA ni
miongoni mwa nchi 54 za bara la Afrika zitakazoshiriki katika tamasha la
‘Urithi wa Utamaduni wa Mabara’ linalotarajiwa kufanyika nchini Ufaransa katika
mji wa ‘Cherbourg’ mwezi Julai mwaka huu.
Tanzania
inashiriki tamasha hilo la kihistoria kwa mara ya kwanza ambapo itapata fursa
ya kutangaza utamaduni wake na vivutio vya utalii vya mambo ya kale hivyo
kuongeza idadi ya watalii na mapato.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa kikao cha pili cha wadau wa utalii kutoka nchi mbalimbali
zinazohusika na tamasha hilo Jijini Dar es Saalam jana, Waziri wa Maliasili na
Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, alisema tamasha hilo litatoa fursa pana
kwa nchi kutangaza vivutio vyake ikiwemo vile vya Zamadamu.
“Kimsingi
tamasha hilo linatarajiwa kutoa fursa kwa Tanzania kutangaza vivutio vyake na
hivyo kuvutia watalii wengi kuja nchini, kila nchi itapewa banda lake la
kuonyesha vivutio vyake , Tanzania naamini inakuwa na vivutio vingi vyenye
kupendeza watalii kama vile Zinjathropus, Ngoma za makabila mbalimbali
pamoja na nyimbo.
“Baada ya
tamasha hilo, kutakuwa na ongezeko kubwa la watalii nchini na ninaamini hata
zile nchi ambazo hazina rekodi nzuri ya kuja Tanzania kwa wingi zilizopo Bara
la Asia zitaanza kuja,’’ alisema Kigwangalla.
Alisema
tamasha hilo linalotarajiwa kuhusisha takriban nchi zote za bara la Afrika,
zaidi limelenga kutangaza tamaduni na vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo
katika mataifa yote yatakayoshiriki huku likitajwa kuwa tamasha bora na
kubwa la utalii pengine kuliko matamasha mengine yote kutokana na kila
nchi kujitokeza kuonyesha vivutio vinavyopatikana katika mataifa yao.
“Tanzania
tunavyo vivutio mbalimbali tunavyotarajia kwenda kuvionyesha katika tamasha
hilo, ukiacha vivutio vya mambo kale, tuna bonde la Olduvai Gorge na mengineyo,
tunayoamini kuwa kupitia tamasha hilo tutaweza kuyatangaza na hivyo
kuvutia watalii wengi kuja nchini” alisema Dkt. Kigwangalla.
Hata hivyo,
alisema baada ya kukamilika kwa tamasha hilo, Septemba mwaka huu hapa nchini
kutakuwa na tamasha la ‘Urithi wa Mtanzania’ linalotarajiwa kufanyika kwa mara
ya kwanza na litakuwa likifanyika kila mwaka kuadhimisha urithi wa Mtanzania.
Alisema
tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika kwa kipindi cha mwezi
mzima, pia
litatoa fursa kwa kila wilaya kutangaza vivutio vyake, huku akizitaka kila
wilaya kujiandaa na tamasha hilo, litakalotoa fursa pia kwa mikoa na wilaya
hizo kukuza utalii wa maeneo yao.
Comments
Post a Comment