- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Rais (mstaafu) Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza na wanafunzi wa ufundi.
Na Daniel Mbega
“VIJANA wetu lazima wapate elimu inayoendana na Afrika. Hii ina maana kwamba, elimu ambayo siyo tu inatolewa Afrika lakini pia inayolenga kukidhi matakwa ya sasa ya Afrika.” Hayo ni maneno aliyoyatoa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Oktoba 25, 1961 akizungumzia kuhusu elimu na sheria.
“VIJANA wetu lazima wapate elimu inayoendana na Afrika. Hii ina maana kwamba, elimu ambayo siyo tu inatolewa Afrika lakini pia inayolenga kukidhi matakwa ya sasa ya Afrika.” Hayo ni maneno aliyoyatoa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Oktoba 25, 1961 akizungumzia kuhusu elimu na sheria.
Elimu ndio msingi wa maendeleo duniani na haijalishi kama elimu hiyo ni rasmi au siyo rasmi.
Ndiyo sababu mara baada ya Uhuru, Mwalimu Nyerere alitangaza
vita dhidi ya maadui watatu: Ujinga, Maradhi na Umaskini.
Wananchi – hata katika kipindi kile cha mwanzo wa Vijiji vya
Ujamaa – siyo tu walihamasishwa kuwapeleka watoto wao shule, bali serikali
ikaanzisha Elimu ya Watu Wazima ili kuwafanya Watanzania wengi wajue kusoma,
kuandika na kuhesabu.
Hii ilisaidia sana, Tanzania ikawa miongoni mwa mataifa ya
Afika yaliyofanikiwa kuufuta ujinga.
Mwalimu Nyerere alisukumwa na taaluma yake ya ualimu, lakini
pia ilikuwa nia yake ya dhati ya kuhakikisha kwamba elimu bora inatolewa kwa
kila mtu, kwani aliamini elimu pekee ndiyo ingeleta maendeleo ya Tanzania, na
hata Afrika kwa ujumla, na ndiyo maana hata katika hotuba zake nyingi
alisisitiza umuhimu wa watoto kufundishwa namna ya kujitegemea na siyo kufaulu
mitihani tu.
Leo hii mwamko wa elimu umekuwa mkubwa, lakini gharama za
elimu zimeongezeka huku ubora wake ukipungua tofauti na ilivyokuwa miaka ya
nyuma. Wanaoweza kumudu gharama hizo ndio angalau wanawapeleka watoto wao
katika shule za binafsi, ambako taaluma iko juu kulinganisha na shule za umma.
Kutokana na ukubwa wa gharama, ndiyo maana mwaka 2016 serikali
ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli, ilitangaza kutoa elimu bure
katika shule za umma kuwanzia msingi hadi kidato cha nne.
Lakini elimu bure ya sasa haiwezi kuwasaidia watoto wetu
kutokana na kuvurugwa kwa mitaala ambayo wakati ule iliwawezesha hata
wanaomaliza elimu ya msingi kujitegemea.
Vipindi vya Elimu ya Kujitegemea (EK) katika shule za msingi
na sekondari viliwapa fursa watoto kujifunza stadi za kazi, kuanzia kilimo,
useremala na mafunzo mengine ya ufundi.
Mwalimu Nyerere aliamini elimu ni ule ujuzi ambao
unamwezesha mtu kujitegemea katika mazingira yanayomzunguka, na siyo fikra zile
za kale za kuona eti mtu mwenye elimu mahali pake pa kazi ni ofisini tu.
Suala hili mwalimu alilikemea kwa kutumia busara, akifafanua
kwa hekima katika hotuba zake mbili alizowahi kuzitoa mjini Tabora (Mei 4,
1967) na mjini Mbeya (Mei 14, 1967) akisema shabaha ya elimu ya msingi lazima
ibadilike.
Mwalimu alisikitika baada ya kubaini kwamba miaka ya nyuma
wakati nafasi za elimu zilipokuwa chache watu waliona kuwa elimu ya msingi
ilikuwa maandalizi siyo ya maisha, bali ya kuendelea zaidi kielimu na kupata
kazi za ofisini.
Lakini akasema, kwa kuupanua mfumo wa elimu kwa wote
(Universal Primary Education – UPE), elimu ya msingi inaweza kuwa maandalizi ya
maisha kijijini na siyo kazi za ofisini tu.
“.. Elimu ya primarykama mnavyojua walimu
wenzangu, mimi sikuwahi kufundisha katika primary kwa hiyo sijui matatizo yake
ya kufundisha. Nimefundisha katika sekondari tu na nimeanzia hapa hapa Tabora.
Kwa hiyo najua matatizo ya sekondari skuli lakini siyo haya ninataka
kuzungumza; wala si matatizo ya walimu ninataka kuzungumza; ni matatizo ya nchi,”
alisema wakati akiwa Tabora Mei 4, 1967.
“Primary, kama mnavyojua kwanza mpaka sasa ni nusu tu ya watoto wetu ambao wanapata nafasi ya kusoma. Kabla ya uhuru tulikuwa tuna ngazi mbili za shule za primary. Tunayo ile miaka minne ya kwanza, halafu wachache hupenya wakaingia katika miaka minne mingine inayofuata ambayo tunaita middle school. Halafu wachache hupenya wakaingia katika miaka miwili inayofuata iliyokuwa ya standard nine na standard ten ya sekondari skuli. Halafu tena tunachuja chuja.
“Tulikuwa na ngazi nyingisana
za kuchuja chuja. Sisi tukaahidi katika Tanu. Tukaahidi kwamba tutafanya mambo
mawili. La kwanza, tutajitahidi kuondoa ngazi hii hapa ya baada ya miaka minne.
Pili, kwamba primary nzima tutaifanya miaka minane. Miaka minane ile tukaijaribu
ikatushinda. Tukaona mirefu. Tukaipunguza tukafanya kwamba elimu ya primary
tutaifanya iwe miaka saba tu basi.”
“.. Elimu ya primary
“Primary, kama mnavyojua kwanza mpaka sasa ni nusu tu ya watoto wetu ambao wanapata nafasi ya kusoma. Kabla ya uhuru tulikuwa tuna ngazi mbili za shule za primary. Tunayo ile miaka minne ya kwanza, halafu wachache hupenya wakaingia katika miaka minne mingine inayofuata ambayo tunaita middle school. Halafu wachache hupenya wakaingia katika miaka miwili inayofuata iliyokuwa ya standard nine na standard ten ya sekondari skuli. Halafu tena tunachuja chuja.
“Tulikuwa na ngazi nyingi
Mwalimu alisema walikuwa wanaogopa kutokana na wingi wa
watoto wanaomaliza shule halafu hawana mahali pa kwenda, yaani wanakosa nafasi
za kwenda sekondari wakati huo, kutokana na uhaba wa shule za sekondari
uliokuwepo.
“Wazee wanauliza; “Mwanangu nitamfanyaje? Sasa mtoto wangu
ameshindwa kwenda darasa la nane, form one. Mimi nitamfanyaje mwanangu?” miezi
ya nyuma nilipopita katika mzunguko ule nilioutaja hapa nilikuwa Musoma, wazee
wangu kule wakataka kunikabidhi watoto wao. Wanasema:- “Nenda nao huko huko Dar es Salaam . Mimi
nitawafanyaje watoto hawa. Wameshindwa! Nenda nao huko wewe utajua la kufanya.”
Nenda nao watoto wenu? Mimi watoto wote hawa wa standard seven nitawabeba! Wa
Tanzania nzima nitakwenda nao wapi? Mzee anauliza: Sasa mtoto huyu ana miaka 13
tu, 14 tu, mnasema eti alime? Atalimaje mtoto wa miaka 13 tu, 14 tu, atawezaje
kulima?
“Swali hilo anayejiuliza si swali la kweli. Upande mmoja si
swali la kweli hata kidogo. Ni swali la mazowea tu. Anasahau mzee huyu huyu,
ama mwalimu, wakati mwingine mtu mwenye akili nzuri kabisa anakuuliza swali
hili… anasema umri wake mdogo mno hawezi kulima. Upande mmoja ni kweli, watoto
hawa wana umri mdogo lakini si umri unaoleta problem. Tatizo ni kwamba wamesoma
watoto hawa. Maana swali hili haliulizwi kwa mtoto mwenye umri kama huo ambaye hakusoma. Haliulizwi. Wanasaga watoto
wale nyumbani, wanaleta kuni… wanalima… wanachunga ng’ombe… wanavuna. Haliulizwi
swali hili juu ya watoto ambao hawakupata nafasi ya kwenda shule. Wao wanasema
atalimaje na mwanangu kasoma? Kusoma huko kwa kulima ni kusoma gani? Maana nia
ya kusoma, madhumuni ya kusoma ni kuepuka jembe. Anasoma mtu aepukane na maisha
haya ya vijijini ya majembe majembe haya.
“Elimu ilikuwa ni utaratibu wa kuhama vijijini… ukianza
kumsomesha mtoto unajua safari yake ya kuhama imeanza. Ilikuwa inaanza hivi
unaiona. Na hasa kwa sababu shule tulikuwa hatuna nyingi, watu waliweza kujua
kwamba anakwenda huyu sasa. Halafu baada ya hapo tena nimefanya safari na
kumaliza standard four. Kwangu standard five nimekuja Tabora. Kutoka Musoma
unakwenda kuifuata standard five Tabora. Ndio unakwenda hivyo! Sasa ikawa ndio
mazowea kwamba mtoto akishapata nafasi ya kusoma, kusoma ni kutokana na kilimo.
Anakuwa kalani na kalamu anaiweka hapa kichwani. Lazima awe ana kalamu msomaji
huyu na shughuli zake hazitokani na kilimo kilimo. Hata unaporudi nyumbani…
wanakufanyia kazi wale wa nyumbani. Binti aliyesoma debe kichwani si mahala
pake.
“Haya ndio mawazo yetu. Na hii ni kwa sababu siku zile elimu
ndivyo ilivyokuwa. Ilikuwa ni kitu cha bahati bahati. Anakipata mtu mmoja kwa
bahati, na makusudi yake ni hayo, unampata mtu akawatumikie wakoloni wanaomtaka
kwa shughuli fulani fulani… Elimu haikuwa ni haki ya kila mtu.
“Elimu ikishakuwa ni haki ya kila mtu, lazima iwe si elimu
ya kuhamisha mtu. Lazima iwe elimu ya kumwezesha mtu yule mahali pake alipo,
maisha yake yanakuwa mazuri zaidi.”
Ingawa maneno haya aliyasema Mwalimu Nyerere miaka 57
iliyopita, lakini bado yangali vichwani mwa watu wengi, kwa sababu tunashuhudia
kiwango cha elimu kinachotolewa sasa shuleni hakikidhi haja kwa mtoto
kujitegemea hapo baadaye.
Maadamu tumekusudia kuwafundisha na kuwaelimisha watoto wetu,
ni lazima tuondokane na mawazo kwamba elimu ni ya kuwahamisha wasomi kutoka
vijijini.
Lazima tufike mahali tuone kwamba shule zetu zinatoa elimu bora ya kumwandaa mtoto kujitegemea, hatakama hakupata nafasi
ya kuendelea na masomo ya juu.
Lazima tufike mahali tuone kwamba shule zetu zinatoa elimu bora ya kumwandaa mtoto kujitegemea, hata
Ikibidi, lazima tuzibadili – kama inawezekana – shule zetu
za Sekondari za Kata ziwe za ufundi stadi ili hata watoto hao watakapomaliza na
kushindwa kuendelea na kidato cha tano, basi waweze kujitegemea.
Tukiweka mazingira mazuri ya elimu, tukajenga shule nzuri,
madawati ya kutosha, walimu bora wa kutosha, nyumba bora za walimu, tutapeleka
na huduma muhimu za kijamii huko vijijini, na kubadilisha mitaala yetu ya elimu
kuwa ya kumfanya mtoto ajifunze elimu bora ya kujitegemea, hakika tutakuwa
tumetimiza malengo ya Azimio la Musoma – Elimu ni Kazi!
Kila kitu kinawezekana tukiwa na malengo, na tukisimama
imara kwa pamoja kushirikiana na wadau kuhakikisha tunayatimiza kwa vitendo
malengo tuliyojiwekea, na kisha kutathmini kama tumefanikiwa au la.
0656-331974
Comments
Post a Comment