- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NA CONGES MRAMBA, MWANZA
APRILI tulikumbuka
vifo vya watu mashuhuri sana hapa duniani wenye nasaba na Bara la Afrika.
Ndiyo mwezi aliokufa
Hayati Edward Moringe Sokoine, William Tolbert wa Liberia, Martin Luther King
Jr, na mashujaa wengine wengi.
Nianze na kifo cha
Tolbert huko Liberia.
Samuel Kanyon Doe alizaliwa Mei 6,
1951, akaja kuuawa kinyama Septemba 9, 1990.
Aliongoza Liberia
kuanzia mwaka 1980 hadi 1990.
Alizaliwa katika mji
mdogo wa Tuzon, katika Kaunti (County) ya Grand Gedeh, Kusini Mashariki mwa
Liberia.
Wazazi wake walikuwa
fukara wasio na elimu kama ilivyo watu wengi wa vijijini huko Liberia au hata
hapa kwetu Tanzania.
Alikuwa kutoka kabila
la Krahn, watu maskini na wasio na elimu.
Wakati huo, ni yeye
pekee aliyehitimu shule ya msingi, akaingia jeshini kwa kuwa hakukuwa na nafasi
nyingine ya kazi.
Oktoba 1979 ndipo
alipopata cheo cha ‘Master Sergeant’ katika Jeshi la Liberia.
Akawa anajisomea usiku
masomo ya ‘High School’ ndipo wakati huo yeye na vijana wenzake 17
walipompindua Rais.
Huu ndio ulikuwa
mwanzo wa mapinduzi dhidi ya William Tolbert.
Walimkamata Rais
William R. Tolbert Jr, wakasimika utawala wa kijeshi, hiyo Aprili 12 mwaka
1980.
Tolbert na Sokoine
walikufa Aprili 12.
Sokoine alikufa kwa
kile kinachosemwa ajali ya gari mwaka 1984, wakati Tolbert aliuliwa Aprili 12
mwaka 1980 na wanajeshi waliopindua serikali.
Rais Tolbert (66)
aliongoza Liberia iliyokuwa tulivu sana, “The Model of Peace in Africa” zama
hizo.
Alikuwa Mwenyekiti wa
Umoja wa Nchi huru za Afrika (OAU) wakati anapinduliwa.
Uenyekiti huo
alipewa wakati wa Mkutano wa 16 mjini Monrovia.
Mauaji ya Tolbert
yalifanyika Aprili wakati wa Pasaka, ndiyo maana yanaitwa “Blood Easter”.
Wenzake, Brigedia Jenerali
Abraham Kollie, Tom Quiwonkpi, Thomas Weh Sen (alikuwa Makamu Rais wa Doe) alichinjwa
mwaka huo huo, Nicholas Podier alitimuliwa jeshini!
Maiti ya Tolbert na watu wake 27 waliouawa
wakati wa mapinduzi hayo ya kijeshi, zikazikwa katika makaburi mawili ya pamoja
mjini Monrovia. Maiti zote zilisombwa kwa lori!
Kwa hiyo, Doe yeye
alikuwa msomi miongoni mwa vijana 18, akawa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
la Ukombozi, lililoitwa People’s Redemption Council (PRC).
Tunajua licha ya
kumuua Rais, aliwachinja wafuasi wake baada ya mapinduzi hayo. Katiba
ikabadilishwa, ukawa utawala wa kijeshi, yaani "military junta.”
DOE KIBARAKA WA
MAREKANI
Doe wakati huo
alihitilafiana na msimamo wa Rais wetu, Mwalimu Nyerere juu ya Ukombozi Kusini
mwa Afrika, na siasa zetu za kutofungamana na upande wowote katika Vita Baridi (Cold
War), ila sisi vijana tulimhusudu tu Doe.
Liberia ina watumwa wa
zamani huko Marekani, wanajiita, “Americo-Liberian elites” waliorejea kuanzisha
taifa hilo mwaka 1847, sasa yeye alitoka kabila dogo tu.
Doe, aliwaruhusu
Wazungu kufanya lolote Liberia, hata makampuni na mimeli yao haikutozwa kodi.
Wazungu walishiriki
misamaha ya kodi Liberia, walishiriki ufisadi mkubwa, mimi na vijana wenzangu
tukiihusudu tu picha ya Doe.
Shirika la Ujasusi la
Marekani (CIA) ndilo liliwasaidia kufanya unyama mkubwa Liberia, na inasemwa
alikuwa shushushu wa CIA aliyemlipua Tolbert.
Ilitangazwa mwaka 1989
kwamba Doe alihitimu Shahada ya Kwanza (BA) hapo Chuo Kikuu cha Liberia.
Doe alikuwa mtambo wa
kuwakata kilimilimi waliounga mkono Ukomunisti wa Kirusi na Cuba zama hizo.
CHARLES TAYLOR
Aliyeondoa mzizi wa
fitina ni Charles Taylor (sasa mfungwa wa maisha) aliyeingia kutoka Ivory Coast
na wapiganaji wa msituni Desemba 24, 1989.
Taylor alitoroka jela
Marekani (wakati mwingine inasemwa alitoroshwa na CIA) akaenda Libya kwa
Gaddafi, akafundishwa vita, akaja sasa kumpinga Doe, maana Marekani wakikutumia
sana wanakuua kwa kukugonganisha vichwa na wenzako, wao wakiwa pembeni
wanatazama!
Mwaka 1990 nchi
ilikuwa msambweni, Doe alikamatwa mjini Monrovia na Prince Y. Johnson
Septemba 9, 1990.
Alikuwa akihudhuria
mkutano wa ECOMOG, Jeshi la Kulinda Amani huko Magharibi mwa Afrika.
Makao Makuu yalikuwa
Monrovia, sasa Johnson alikuja na majeshi yake, akamkamata Doe, baada ya vita
kali ya bunduki. Ilikuwa ‘Ambush’.
Jamaa alichukuliwa
mateka, akapelekwa katika ngome ya Johnson, akateswa sana; alitembezwa uchi wa
mnyama mjini Monrovia akiwa uchi wa mnyama, watu wakishangilia sana kutokana na
unyama wake.
Ni hawa hawa Marekani
waliomuua Mweusi mwingine, Malcolm X na Martin Luther King Jr.
El-Hajj Malik El Shabazz, ni Mwanaharakati maarufu wa Haki
za Weusi wa Marekani, ambaye wakati dunia inapojadili ukandamizaji wa Weupe
dhidi ya Weusi wa Marekani, hatasahaulika.
Malik El-Shabazz, ambaye ni maarufu sana duniani kama
Malcolm X alikuwa Mwamerika Mweusi, tena Kiongozi wa Dini ya Kiislam
aliyezaliwa Mei 19, 1925 Kaskazini mwa Omaha, Nebraska, Marekani.
Mwanaharakati huyu aliuawa Feburuari 21, 1965 huko New York.
Aliwahi kumwoa kidosho mmoja aitwaye Bety mwaka 1958 hadi
alipofariki mwaka huo 1965, akazaa watoto Qubilah, Ilyasah, Malikah, Malaak, Gamilah,
Lumumba na Atallah.
Familia ya mtu huyu iliishi katika vitisho na majaribio ya
mauaji ya kila mara.
Feburuari 14, 1965 familia hii ilinusurika kuuawa mjini New
York, lakini hakuna mtu aliyeshitakiwa kwa kosa la jaribio la mauaji ya watu
hawa.
Hatimaye, siku saba baada ya jaribio hili yaani Feburuari 21
huko Manhattan, wakati Malcolm akihutubia, watu watatu wakiwa na silaha
walikuja upesi wakampiga risasi huku wakiwa karibu naye.
Walimfyatua risasi mara 15.
Alipelekwa Hospitali ya Presbyterian akafariki baadaye akiwa
na umri wa miaka 39.
Ibada ya mazishi yalifanyika Feburuari 27, 1965 katika
Hekalu la Kikristo na yalihudhuriwa na jumla ya watu 1,600 akazikwa makaburi ya
Femcliff huko Hartsdale, New York.
Baadaye mwaka huo, mkewe Betty alizaa mapacha wawili.
Inakisiwa, mtu huyu aliuawa na vikosi vya Usalama, hususan
Federal Bureau of Investigation (FBI), na miaka mitatu baadaye, Aprili 1968,
Martin Luther King Jr, naye aliuawa na Makao Makuu ya Jeshi la Marekani, The
Pentagon.
Mtu huyu alizaliwa
Januari 15, 1929, akaja kuuawa Aprili 4, 1968.
Alikuwa Mweusi, ndugu
zetu waliopelekwa Marekani kama watumwa ili kulima mashamba ya mabwana wakubwa.
Alikuwa mwanaharakati
aliyepinga ubaguzi na dhuluma.
Huyu ndiye aliyeiona
ndoto ya Mweusi kutawala Marekani, “I Have A Dream” mwaka 1968, kabla ya kifo
chake, na miaka 40 baadaye, Barack Obama akaja kuwa Rais mwaka 2008.
Ni maarufu kwa hotuba
yake hii ya Ndoto ya Mweusi wa Afrika kutawala Marekani, akipanga vita dhidi ya
Vietnam na umaskini wa Weusi na dhuluma waliyofanyiwa na ‘Magabacholi’ Wazungu.
Alitunukiwa tuzo ya
Nobel Oktoba 14, 1964 kwa mtindo wake wa kupinga ubeberu bila kulipa kisasi,
‘nonviolence’.
Aliuliwa na Pentagon
huko Memphis, Tannessee.
LINCOLN
Abraham Lincoln, Aprili 14, 1865 alipigwa risasi
na John Wilkes Booth, mcheza sinema katika jumba la sinema, Ford’s Theater, Washington,
akaja kufa Aprili 15.
Kawaulize waandishi wa habari waliandika nini
kama siyo kwamba hawa viongozi walikufa kwa risasi na wauaji wakatajwa?
J.F. Kennedy alipouawa alisingiziwa Lee Harvey
Oswald ambaye naye aliuawa na Jack Ruby wakati akisubiri kusikilizwa kesi yake.
Lincoln aliuawa na
mashushushu wa Marekani, kama wengine, tena mwezi huo Aprili.
Martin Luther, yule
Kasisi wa Katoliki, aliuliwa huko Ujerumani zama za Matengenezo ya Kikristo (Christian
Reformation), yupo Martin Luther King Jr wa Marekani, Malcom X (Malik al
Shabaaz) alipigwa risasi na Ma-Jesuits mwaka 1963, Bruce Lee, mcheza filamu maarufu aliuliwa huko Hong Kong.
TITANIC
Nikusimulie kidogo
kuhusu meli ya Titanic, ambayo hata BCBG wameimba juu yake.
Ilianza kujengwa 1909
huko Belfast, Ireland chini ya kampuni ya White Star.
Ilianza safari zake
Aprili 10, 1912 iliongozwa na Kapteni E.J. Smith ambaye alipewa maelekezo
kwenda Atlantiki kwenye mabonge ya barafu ili kuigongesha meli hiyo na kuua
watu.
Tazama ni mwezi
Aprili.
Nataka nikwambie
msomaji. Kulikuwa na matajiri wenye mali, wenye fedha nyingi. Mali zao
zilikuwa za thamani ya Dola bilioni 12 ambao wote wangezamishwa Aprili 1912.
Hawa ni Benjamin
Giggenheim, Isidor Strauss ambaye alikuwa Meneja wa Marcy’s Department Store, na
John Jacob Astor.
Hawa walikuwa matajiri
wa Kimarekani na walikuwa wapinzani wakubwa wa Ajenda ya Siri ya kuitawala
dunia kwa nguvu ya pesa, nguvu ya utajiri, kupitia mabenki makubwa kama Benki
ya Dunia (WB) na Fuko la Kimataifa la Fedha (IMF).
Nahodha wa Meli ya
Titanic, E.J. Smith, alielekezwa kuizamisha meli ili kuwaulia mbali matajiri
waliokuwemo.
Matajiri hawa
walioangamia katika ajali hiyo ni John Jacob Astor,Archibald
W.Butt,Charles M. Hayes,na mkewe na binzi zao, W.T.Stead,Benjamin Guggenheim,
F.D. Millett na G.D. Widher.
Wengine walioangamia ni
Isidor Strauss, na mkewe, J.B Thayer, J. Bruce Ismay, Henry B. Harris na mkewe
na Washington A. Roebling.
Sababu za kifo cha Rais
J.F. Kennedy, ilikuwa Vita vya Vietnam, na siri waliijua Federal Reserve Bank.
Rais J.F. Kennedy
alituma wapelelezi Vietnam, akina McNamara na Taylor, wakaleta Ripoti
iliyomshauri Rais kuondoa majeshi Vietnam, akawakosea hawa mabeberu wa Ulaya na
Marekani!
Waliazimu J.F. Kennedy
aondoke wao waendeleze vita vya maslahi yao Vietnam.
Mwezi Aprili
hutufundisha mengi, ila nimeorodhesha wachache hawa ili tukumbuke unyama wa
jamaa hawa ambao siku hizi tunawaona kama wahisani, na wana waandishi
waliojivika maofisa habari wa Marekani hapa!
Kama wanaweza kuua
hata rais wao, wewe Mweusi mbona wajipendekeza?
CHANZO: FAHARI YETU
Comments
Post a Comment