- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI (MOCU) PROF ,FAUSTINE BEE AZINDUA NA KUONGOZA WATUMISHI WENZAKE WA CHUO HICHO KATIKA ZOEZI LA UPIMAJI WA HOMA YA INI
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Mosi (MoCU) Prof ,Faustine Bee akizungumza wakati wa uzinduzi wa Upimaji wa Homa ya Ini kwa Watumishi wa Chuo hicho pamoja na Wategemezi wao, zoezi ambalo linafanyika katika kituo cha Afya kilichopo chuoni hapo.
Baadhi ya Wauguzi wanaohudumu katika kituo hicho fcha Afya pamoja na Watumishi wa Chuo hicho wakifuatilia hotupa ya Uzinduzi wa zoezi la Upimaji wa Homa ya Ini iliyotolewa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU)
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) ,Eustace Ng'weshemi akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji wa Homa ya Ini katika Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi .
Baadhi ya Watumishi wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi ,wakiwa katika uzinduzi huo.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) Dkt , Eustace Ngw'eshemi akimuonesha Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi ,Prof Faustine Bee namba ya siri itakayotumika wakati wa kupokea majibu baada ya zoezi la upimaji kukamilika.
Mkuu wa kitengo cha Maabara katika Kituo cha Afya cha Chuo Kikuu cha Ushirika (MOCU) Aniseth Malenga akivuta Damu katika mkono wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Prof Faustine Bee alipoongoza zoezi la upimaji wa Homa ya Ini kwa watumishi wa chuo hicho.
Mkuu wa Kitengo cha Maabara katika kituo cha Afya cha Chuo Kikuu cha Ushirika (MoCU) Aniseth Malenga akivuta Damu katika mkono wa Mmmoja wa watusmihi katika Chuo Kikuu cha Ushirika ,Julieti Bee wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji wa Homa ya Ini chuoni hapo.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) Dkt , Eustace Ngw'eshemi akizungumza na mmoja wa watumishi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi kabla ya kumfanyia vipimo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .
CHUO kikuu cha Ushirika
,Moshi (MoCU) kimezundua zoezi la upimaji wa Homa ya Ini kwa Watumishi
,Wategemezi wao pamoja na majirani wa cuo hicho ikiwa ni njia ya tahadhari
licha ya kutokuwepo ushahidi wa mlipuko wa ugonjwa huo nchini.
Serikali inatambua
umuhimu wa afya bora kwa watumishi wake kwani afya bora ni rasilimali muhimu
kwa maendeleo na maenedeleo ya Taifa yataletwa na wananchi pamoja na watumishi
wenye Afya na wenye uwezo wa kuzalisha mali na kutoa huduma stahiki kwa umma wa
Tanzania.
Katika kuzingatia sera
na miongozo ya Afya ya mwaka 1990 iliyopitiwa mwaka 2007 ,Chuo Kikuu cha
Ushirika Moshi (MOCU) kama mdau imeanza kutoa huduma ya upimaji wa Ini kupitia
Kituo chake cha Afya kilichopo chuoni hapo.
Makamu Mkuu wa Chuo
Kikuu cha Ushirika (MoCU) Prof Faustine Bee akatumia zinduzi huo kutoa wito kwa
watu wengine waishio nje ya mazingira ya Chuo hicho kutumia kituo hicho pindi
wanapohitaji huduma za matibabu.
Zaidi ya watumishi 456
wanashiriki katika zoezi la Upimaji wa Ini chuoni hapo huku Menejimenti ikiwa
katika mazungumzo na Hospitali ya Rufaa ya KCMC ukiona uwezekano wa Wagonjwa
wanaohitaji rufaa kwenda moja kwa moja KCMC badala ya kupitia Hosptali ya Mkoa
ya Mawenzi kama ilivyo sasa.
Mwisho.
Comments
Post a Comment