- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Rais Dkt. John Magufuli
Yatoa
msaada wa magari 181 kwa Tanzania bila masharti
·
Yaahidi
kuendeleza ushirkiano na Tanzania
Na Jonas Kamaleki
Serikali
ya Awamu ya Tano imejipambanua kitaifa na kimataifa kwa uwajibikaji uliotukuka
na vita dhidi ya rushwa na ufisadi wa kila namna.
Kutokana
na utendaji huu unaozingatia sheria,kanuni na taratibu, mashirika ya kimataifa
zikiwemo nchi zilizoendelea na zinzoendelea zimeonyesha dhahiri kupendezwa na
kazi nzuri zinzofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Hii
imedhihirika hivi karibuni pale ambapo Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi,
Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund), Linden Marrison Global Fund kutoa msaada wa magari 181 kwa
ajili ya kusambaza dawa za binadamu katika vituo vya afya na hospitali zilizopo
nchini.
Hii
ni mara ya kwanza tangu Tanganyika (Tanzania) ipate uhuru kupata msaada wa
magari mengi kwa pamoja kwa ajili ya Bohari ya Dawa (MSD). Jambo hili limefanyika
kutokana na umakini wa Serikali ya Rais Magufuli ambao umejenga imani kubwa
ndani na nje ya nchi.
Magari
haya 181 pamoja na mengine yaliyokuwepo yatatumika kusafirisha dawa katika
mikoa yote ya Tanzaniaili kurahisisha upatikanaji wa dawa hadi vituo vya afya
vya vijijini ambavyo awali ilikuwa ni shida kuvikia kwa wakati.
Mwakilishi
wa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi, Kifua kikuu na
Malaria (Global Fund), Linden Marrison anaisifia Serikali ya Awamu ya Tano kwa
kazi nzuri inazofanya na kuahidi kushirikiana nayo.
Marrison
anasema uwazi katika kuendesha serikali na vita dhidi ya rushwa vinaifanya
Global Fund kuiamini Tanzania na kuendelea kushirikiana nayo na ndiyo maana
wamekubali kuipa msaada wa magari 181 bila masharti.
Upatikanaji
wa dawa kwa sasa nchini unaridhisha, na hii ni kwa sababu ya juhudi za makusudi
zilizofanya na Serikali ya Rais Magufuli kuongeza bajeti ya dawa toka shilingi
bilioni 31 hadi bilioni 269. Haya ni mabadiliko makubwa ambayo yameondoa dhana
iliyokuwa imejengeka kuwa hospitali za serikali zinatoa tu Panadol na Asprin.
Rais
Magufuli anadhihirisha hili anaposema kuwa bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekuwa ikiongezeka na kwa mwaka wa fedha
2017/18 imefikia shilingi trilioni 2.2.
Jitihada
hizi za kuboresha sekta ya afya nchini zinashuhudiwa na Waziri mwenye dhamna ya
Afya, Ummy Mwalimu ambaye anampongeza Rais Magufuli kwa kulipa kipaumbele suala
la afya.
Ummy
Mwalimu anamshukuru Rais Magufuli kwa kuongeza bajeti ya Wizara yake hadi
kufikia trilioni 2.2 kwa mwaka wa Fedha 2017/18, jambo ambalo Waziri anasema
halijawahi kutokea tangu nchi hii inapata uhuru takriban miaka 57 iliyopita.
Suala
la kununua dawa kwa wingi toka nje, ni jambo ambalo linamkera Rais Magufuli.
Hivyo wito wake kwa wawekezaji wa ndani ni kujenga viwanda vya dawa hapa nchni
ili kupunguza uagizaji wa dawa hizo.
"
Tanzania tuna wasomi wengi, tuna waandisi wengi , pamba za hospitali tunaagiza
China wakati sisi ndio wakulima wa pamba, maji ya dripu tunaagiza Uganda, hivi
Profesa Janabi wanafunzi wako hakuna ambao wanaweza kutengeneza maji hayo",
anashangaa Rais Magufuli.
Rais
Magufuli anasema Serikali iko tayari kuwawezesha watanzania kuwekeza katika
viwanda vya dawa hapa nchini. Amasema kuwa asilimia 94 ya dawa zinazotumika
hapa nchini zinatoka nje na ni asilimia 6 tu zinanunuliwa nchini.
Mkurugenzi
Mkuu wa MSD, Laurean Rugambwa Bwanakunu anasema kuwa mchakato wa kununua dawa
nje ya nchi pamoja na kupunguza kutoka miezi 9 hadi wastani wa kati ya miezi 6
na 4 kulingana na aina ya dawa na kifaa tiba kinachonunuliwa, muda huu bado
anaona ni mrefu na unaligharimu taifa
fedha nyingi.
"
Kwa mwezi tunaagiza na kuleta makontena karibu 50 ya maji na makontena 20 ya
pamba, Tanzania ina viwanda 13 tu vya dawa, vyenye mkataba na MSD ni vitano tu,
hii haikubaliki kabisa", anasema Bwanakunu.
Rais
Magufuli amewahikikishia watanzania kuwa soko la dawa hapa nchini ni la kutosha
kwani Tanzania imepewa jukumu la kuuza dawa katika nchi zote za Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Ametoa
wito kwa wawekezaji hasa sekta binafsi kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya
dawa ili fedha nyingi za kununulia dawa zibaki humu humu nchini na kutoa ajira
kwa watanzania.
MSD
inahudumia vituo vya afya zaidi ya 7,309 nchini, hili ni soko tosha kwa yeyote
anayetaka kuwekeza katika viwanda vya dawa.
Watanzania
ni wakati mwafaka kuweza kutembea na maono ya Rais magufuli ya kupunguza
kuagiza dawa toka nje na badala yake kutenegeza dawa wenyewe kwa kuanzisha
viwanda hapa nchini.
Ujenzi
wa viwanda vya dawa utawezesha watanzania kuokoa fedha za kigeni ambazo
zinaweza kutumika kwa masuala mengine ya maendeleo nchini Tanzania.
Kupitia
viwanda hivyo, ajira hasa kwa vijana zitaongezeka, jambo ambalo litaongeza
kipato cha mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kwani kodi ya Serikali
itakusanywa kutoka kwenye viwanda hivyo.
Mazingira
ya uwekezaji nchini yameboreshwa kwa kupunguza ama kuondoa vikwazo katika
vibali vya uwekezaji.
Kwa
mujibu wa Mkurugezi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Geofrey Mwambe,
Tanzania imebadilika kwa kuweka pamoja watoa vibali vinavyohusika na uwekezaji.
Kimetengenezwa kituo cha pamoja kilichopo TIC.
Katika
kituo hicho, taasisi zinazohusika na kutoa vibali vya uwekezaji zina
wawakilishi katika kituo hicho. Ofisi za Uhamiaji, Wakala wa Usajili wa
Biashara na Leseni (BRELA), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Shirika la
Viwango Tanzania (TBS), Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na
Idara ya Kazi, zina maafisa kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa vibali kwa
wawekezaji akiwemo afisa toka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
"Mwekezaji
akiwasilisha maombi yake ya kibali, yanashughulikiwa ndani ya siku tatu na jibu
linapatikana kwa sababu taarifa nyingi kuhusu matakwa ya vibali vya uwekezaji
yako kwenye tovuti ya TIC", anasema Mwambe.
Ikumbukwe
kuwa kabla ya kuwa na kituo kinachojulikana kama One Stop Centre usumbufu ulikuwa mkubwa kiasi kwamba baadhi ya
wawekezaji walikatatamaa ya kuwekeza nchini.
Juhudi
za Serikali ya Awamu ya Tano za kuondoa ukiritimba zimezaa matunda hasa katika
eneo la uwekezaji. Hivyo wenye nia ya kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza
dawa wafanye hivyo kwani mazingira wezeshi yako tayari.
Comments
Post a Comment