- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Kamishna wa Usalama dhidi ya moto wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Jesuald Ikonko.
TAARIFA KWA UMMA
Kufuatia uwepo na muendelezo wa mvua kubwa, ambazo
zitaambatana na upepo mkali katika maeneo mbalimbali hapa nchini kama
ilivyolitolewa taarifa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA). Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara, linawatahadharisha
wananchi kuwa makini katika suala zima la Kuokoa Maisha na Mali zao.
Kutokana na mvua hizo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
linawataka wananchi wote wanaoishi kwenye mazingira hatarishi (Mabondeni) kuwa
makini na kuchukua hatua mapema ya kuyahama maeneo hayo kabla mvua hizo
zinazotabiriwa hazijaanza kuleta madhara makubwa.
Hata hivyo, Jeshi lipo timamu na tayari kwa
kukabiliana na majanga yoyote yatakayotokana na mvua hizo. Tunawaomba wananchi
wote kuwa wepesi katika kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vya mafuriko au
mtu kuzingirwa na maji.
Aidha, tunawaomba wananchi kutumia namba ya simu
ya dharura 114 (bure) kutoa taarifa za
matukio ya Moto, Mafuriko, Ajali za barabarani, Tetemeko la ardhi na majanga
mengine kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Imetolewa na;
Kitengo cha Habari na Elimu kwa
Umma
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji-Makao
Makuu.
Comments
Post a Comment