- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Aidha wameambiwa kwamba kwa kuwa Redio ina nguvu kuliko chombo chochote kingine duniani kwa kuwafikia watu wengi zaidi hivyo basi wanatakiwa kuwa makini wanapowafikishia wananchi taarifa.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Juliana Shonza katika maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika Dodoma ambaye alitaka taarifa kwa wananchi kufikishwa bila ushabiki, chuki au kupiga chuku (kuongeza chumvi).
Alisema tasnia ya uandishi wa Habari ni tasinia adhimu sana, hivyo Waandishi wote wa Habari wanalo jukumu kubwa la kuzingatia misingi ya uandishi ambayo ni mizania (balancing), kutofungamana na upande wowote (impartiality), kutenda haki (fairness), Utu (humanity), na mwisho kabisa kuzingatia ukweli (truthness).
Siku ya Redio Duniani huadhimishwa kila mwaka duniani kote Tarehe 13 mwezi Februari ili kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Redio mahali pote duniani.
Aliwakumbusha waandishi na wageni historia ngumu na mbaya ya namna redio zilivyotumika vibaya katika baadhi ya nchi duniani na kuleta machafuko hadi umwagaji damu.
“Hivyo niwaase tena kutumia redio hizo na vipaza sauti kwa ajili ya kutoa taarifa muhimu juu ya masuala ya kilimo na ufugaji, majanga mbalimbali, elimu juu ya sera na sheria mbalimbali za nchi, masuala ya afya kwa jamii na elimu. Na kwa kufanya hivyo tu, ndipo tutakuwa tumeitendea haki tasnia hii.” alisema Dk. Shonza.
Waziri Mwakyembe alishukuru Shirika la UNESCO na Mtandao wa Redio Jamii Tanzania (TADIO) kwa kuwezesha siku ya redio na kusema atatafakari hoja zote zilizowasilsihwa kwake.
Naye Katibu wa Mtadao wa Radio Jamii (TADIO), Marco Mipawa akisoma hotuba kwa niaba ya Mwenyekiti wa mtandao huo, Prosper Kwigize alitaka serikali kuhakikisha kwamba urasimu unaondolewa kwenye utoaji wa taarifa kwa umma ili kuwezesha kufanyika kwa vipindi mbalimbali vya habari.
Aidha maafisa habari walioajiriwa wapewe mamlaka na wawezeshwe kufahamu kinachofanywa na serikali na wawe na ruhusa ya kutoa taarifa kwa vyombo vya habari katika maeneo yao.
Alisema kutokana kutokuwa na vyanzo vya mapato ya uhakika serikali ingeangalia suala la kodi na ushuru mbalimbali ili kusaidia Redio za Jamii kutolipia huduma za Radio.
Pia amesema sheria zilizopo ukilinganisha na mazingira halisi ya kazi ya mwanahabari, mfano sheria ya Takwimu, sheria ya huduma za habari, sheria ya makosa ya mtandao kumeshabibisha tasnia ya habari na utangazaji kuwa katika mashaka zaidi kuliko kipindi kilichopita.
Ameitaka Serikali kutoa Ruzuku ya elimu au mafunzo ya kitaaluma kwa wanahabari ili kuwawezesha kukidhi vigezo vya kisheria ifikapo 2021 Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo amewataka waandishi na watangazaji kutumia redio kwa manufaa ya taifa kuleta mshikamano na pia kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Awali akimkaribisha Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari Mh. Shonza, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge amesema Unesco inafanya kazi nzuri sana kwa kuwekeza kwenye vyombo vya Habari na kuvitaka vyombo hivyo kuitangaza Dodoma na fursa zake kwa sababu ndio makao makuu ya nchi.
Alitaka vyombo hivyo kuvutia wawekezaji ili mji huo uwe kweli katika karne ya 21 na makao makuu ya nchi.
Comments
Post a Comment