- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AHUDHURIA MKUTANO MAALUM WA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC) UNAOFANYIKA KAMPALA NCHINI UGANDA
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akihutubia katika Mkutano huo Maalum wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) unaofanyika Kampala nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wakielekea kwenye
ukumbi wa Mkutano Maalum wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC
unaojadili masuala mbalimbali ikiwemo Maendeleo ya Sekta ya Miundombinu na Afya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
amesimama pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda
Yoweri Museveni wa nne kutoka kulia, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na
Rais wa Sudani ya Kusini Salva Kiir wakati Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulipokuwa ukipigwa katika
ukumbi wa mkutano uliopo katika eneo la
Munyonyo Kampala nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
amekaa pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda
Yoweri Museveni wanne kutoka kulia, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Rais
wa Sudani ya Kusini Salva Kiir wakati wa mkutano huo Maalumu wa Wakuu wa nchi za
Jumuiya ya Afrika Mashariki unao endelea jijini Kampala.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri
Museveni akifungua Mkutano huo maalum wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Kampala nchini Uganda.
Wajumbe kutoka nchi mbalimbali za Jumuiya a Afrika Mashariki
wakifatilia hotuba mbalimbali katika Mkutano huo maalum.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri
Museveni katika picha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli wa kwanza kulia, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, pamoja na Rais wa
Sudan ya Kusini Salva Kiir mara baada ya Mkutano Maalum wa 19 wa Jumuiya hiyo uliofanyika Kampala nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Rais wa Sudan ya Kusini Salva Kiir kabla ya kuanza kwa mkutano
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa
19 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Kampala Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akifurahia jambo na Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta mara baada ya kupiga picha ya pamoja katika eneo la Munyonyo Kampala
nchini Uganda. PICHA NA IKULU
Comments
Post a Comment